Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Status
Not open for further replies.
Ulaya hakuna hata mwehu mmoja mwenye kuweza kushangilia kushushwa kileleni mwa ligi only in Simba Sc ndio utakutana na majinga hayo.

Fanya Cost Benefit analysis ya kikosi chenu na cha Simba, linganisha resources mlizozitumia kutaka kurudisha zile 5 ila kimebuma. Jipangeni tena.
 
Fanya Cost Benefit analysis ya kikosi chenu na cha Simba, linganisha resources mlizozitumia kutaka kurudisha zile 5 ila kimebuma. Jipangeni tena.

Wachezaji wa kimataifa wametoa droo na watoto wa mchangani.
 
Waiter upo wapi leta kinana nyingine, saa ngapi jamani lakini sina hofu boss naye ni simba damu kama mimi

Ulikunywa ngapi?

Vp umewahi kazini leo au hang over imechyua nafasi yake umeshindwa kuamka.

Chezeya mahaba na simb
a
 
We mama wewe. We njoo tu nikuoe. baaas. Haka ka Heaven on earth kamenipa tabu sana jana. Yani shenzy zake chapchap sana. Hii hangover sijui kama ntaenda kwa mkoloni.

Ha ha haaa, babu unazeeka vibaya...yaani furaha hadi unataka kuoa mjukuu????

By the way pole na hangover ila jitahidi tu uende kwa mkoloni ili upate za kuzimua.

Jana ulimtaja hadi Mungu...kufungwa si kwa kuombea
 
Katika siku ambazo nilikuwa na tension ya mpira ni jana. Maana nilianza kupata sms za kubezwa kuanzia saa 12 ahsubuh, yaami ilikuwa taabu sana.

Muda wa mechi sikuwa na raha yalemaneno niliyobezwa yalikuwa yanaring in my brain na mapicha ya kumdhalilisha mnyama yaani hata mlo wa mchana sikula.

Niliamua kutouangalia neikaenda zangu vikobaaa....niko njiani nasikia goooo...ikabidi nisogee tumefuungwa, niko kwenye kikao nasika tena gooo tumefungwa, nikachungulia JF na kisimu changu laaaa nikakuta wakina Heaven on earth, na webzake ndo wanashindilia mwiba moyoni nika log out fastaa. Nimeamini nina mapenzi makubwa na SIMBA

Naanza safari ya kurudi home shosti ananipigia simu eti cha tatu hicho kaoge....yaani nusu nimtukane. Mwingine tena haloow leo lazima uumwe..nikamwambia mmpira ni 90min, akasema mmeshapigwa v3 unaongea dkk 90.

Njiani tena nikakutana na mwenye kiredio chake ile napishana nae tuu nasikia gooo, yaani nilihisi mapigo ya moyo yana potea..nasikilizia la nne au? Aaa kumbe MNYAMA ameanza kuchomoa, baada ya muda tena nasikia gooo chapili. Nakaribia home nasikia tena gooo afu watoto wananilaki mama mama simba wamesawazisha matatu mama timu yako. Kajasho kembaba kalinitoka kafuraha lakini na kushushia punzi maana.

Nimetumia almost masaa mawili kufuatilia thread, kwa nionavyo yaani kweli kipindi cha kwanza SIMBA tulikuwa na simanzi sana. Nina furaha ya ajabu si kwa sbb ya droo but kwa simba kucheza mchezo wa maana na kuweza kurudisha mabao ma 3 kwa staili ya aina yake.

Kwa upande mwingine nijambo lisilofichika kuwa pamoja na droo YANGA wameaibika.....POLENI

Salamu kwa wazalendo wa ukweli wa SSC Ndeticha, @Exellent Katavi, Asprin, Masuke, Filipo, KakaKiiza, Mzee wa Rula, stevoh na all SIMBA SPORTS CLUB Fans...pamoja sana.

Yanga SIMBA mtaipenda tu.... Balantanda nimekukubali sana..thumb up for you mkuu

Hivi sasa ni saa 01:54 tukutane baadayeee....kwa heri kwa sasa.
Kula tano mwanamsimbazi, acha watubeze na kututukana wanaosema tunashangilia droo hawajui ni kwa nini tumefurahi maana pia hawajui hali tuliyokuwa nayo wakati wanaongoza zile tatu, wangejua hali tuliyokuwa nayo wasingetubeza na kututukana.
 
Last edited by a moderator:
Ha ha haaa, babu unazeeka vibaya...yaani furaha hadi unataka kuoa mjukuu????

By the way pole na hangover ila jitahidi tu uende kwa mkoloni ili upate za kuzimua.

Jana ulimtaja hadi Mungu...kufungwa si kwa kuombea

Si unajua Mungu ni shabiki wa Simba?
 
Kitenge mwenyewe haamini yanayotokea, anakwambia Kocha wa Yanga naye ameingia kwenye mtego wa mashabiki wa kuona walivyoongoza tatu bila wakaona wamemaliza kila kitu walisahau kwamba mpira ni dakika 90.
Basi yeye akaombe ukocha wa Yanga
 
Club bingwa Afrika fainaly ni Al Ahaly vs Orlando Pirates. Nyinyi endeleeni na ushabiki wenu maandazi wa kombe la mbuzi.
Mkuu naona unajidai kutoa ushauri kumbe unahangaika kama Kitenge
 
Mkuu naona unajidai kutoa ushauri kumbe unahangaika kama Kitenge
Huyu jamaa toka jana nimeshamwona ukiendelea kujibizana naye huchelewi kuswekwa lupango ya JF maana anapenda
sana kuprovoke watu sijui hajiamini, sentensi moja ya pili tusi.
 
247686_1425543747658697_1996950327_n.jpg

Hahahahahahahaahahah hahaahahahha....hii kitu imenichekesha sana...Ila kiufupi Simba Kiboko
 
Kula tano mwanamsimbazi, acha watubeze na kututukana wanaosema tunashangilia droo hawajui ni kwa nini tumefurahi maana pia hawajui hali tuliyokuwa nayo wakati wanaongoza zile tatu, wangejua hali tuliyokuwa nayo wasingetubeza na kututukana.

Ahsante sana mwanamsimbazi mwenzangu. Hali ya dkk 45 za kwanza jana haikuwa nzuri kabisa. Yaani wengine tulikuwa ICU.

Kw kweli nina raha hadi sasa inabubujikia chini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom