Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Status
Not open for further replies.
Yanga hamjanitendea haki kabisa siku ya leo.
 
Wale waliokuwa wanasema Yanga asiposhinda wanameza kisu nataka niwatafute nina visu kama vitatu, na yule aliyesema kila goli moja Simba ikipata ban siku tatu, Invisible wale wote waliotaka kufungiwa endapo Simba itapata goli bila kujali kama itashinda au la, naomba utekelezaji wa ombi lao.
Hahaa mkuu wasamehe bure, utaua!!
 

Attachments

  • simba-mnyama tisha.jpg
    simba-mnyama tisha.jpg
    63.8 KB · Views: 73
Wachezaji wa yanga wamekimbia,hawataki kabisa kuzungumza na media!du aibu sana.kiufupi simba ndo wameshinda hii mechi.
 
na kinyume chake.

Ki ukweli nyie mna huzuni zaidi kwa sasa kuliko sisi, yaani ni kama Simba tumeshinda kwa jinsi tulivyokuwa tumenyong'onyea wakati mnaongoza tatu bila,na mlijua mechi ishaisha, wewe unafikiri kurudisha goli tatu kazi ndogo? ukuta wa zege unazidi kutobolewa tu bora sisi na timu yetu ya kuunga unga tunazidi kuweka rekodi ya kuwa miongoni mwa timu tatu ambazo hazijafungwa hadi sasa.
 
...ngoja tusubiri, tuone HEMED KIVUYO atakuja na kauli gani kupitia ITV michezo.

ha ha ha!huyu jamaa huwa ananichekesha sana,ngasa angetamba leo,na vumbi lingetimka,kumbe ameshakuwa kijeba!
 
Huwezi kunielewa, yupi wa maana kati ya aliyepata mali mapema na kushindwa kuzilinda na kufuja ovyo na yule aliyehangaika akaja akapata uzeeni na kuzilinda?

Tuna safari ndefu sana kama tuna mazuzu kama wewe kushangilia droo badala ya kuona timu zote mbili zina defense mbovu kabisa kwa kuruhusu magoli matatu katika mechi moja.

Halafu kwa akili hizi ukwaju ndio mnafikiria kucompet na timu kama TP Mazembe! Wewe kweli ni boya.
 
Yeboyebo mnabahati sana, mnajisifia timu nzuri mnashindwa kulinda goli tatu ndani ya dak 45, Beki ya Yanga ovyo kweli na kama hawa vijana Ndemla na Lucian wangeanza toka mwanzo tungekuwa tunaongea mengine hadi sa hivi.
Naona uliingia mitini mtani.......Shabiki lazima ukomae mwanzo mwisho.....

Mkuu, wanaojisifu wana timu mwaka huu ni Simba, kulikoni mkaruhusu bao 3 kipindi cha kwanza mtani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom