Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Yaliyojiri VPL: Simba SC vs Yanga SC - 20 October 2013

Status
Not open for further replies.
Nadhani wewe umeanza kushanbikia juzi.....Una habari Yanga wamewahi kuchomoa mechi na Simba Sheikh Amri Abeid Arusha matokeo yakawa 4-4......

Simba bana, badala ya kujiuliza ni kwa nini mliruhusu ba0 3-0 1st Half mnaanza kuiponda Yanga kwa kuruhusu magoli matatu......Ulitaka Yanga ishinde???/
Wamejiuliza ndo maana wamezirejesha kiulaini kama kumtawaza mtoto aliejinyea [yanga].
 
Mkuu hii sare ingekuwa ya funga nikufunge ningeona sawa tu lakini nakwambia mashabiki wote wa timu zote mbili baada ya Kiiza kufunga goli la tatu tulijua Simba ndo basi tena lakini kurudisha magoli yote matatu lazima nifurahi aise.
I see.....

Hongereni sana kwa ushindi mkuu......

Kiukweli mlipaswa kusikitika kwa kukosa ushindi na kusindwa kurudi kileleni na kubaki nafasi ya 3 hasa ukizingatia mna mechi 2 ngumu za mfululizo, dhidi ya Coastal Union(inayofuata) na dhidi ya Azam(baada ya kucheza na Coastal.....

Yanga wana mechi rahisi ambazo zitawaezesha kuwashusha Simba kwenye msimamo wa Ligi......

Na hii ni mara ya kwanza kuona Simba wanashangilia sare dhidi ya Yanga.....Kipindi kile Yanga wamechomoa sare ya 4-4 Jangwani bado hakukukalika......Walijiuliza ni kwa nini wameruhusu magoli yale manne....Lakini kwa Simba ni burdaaaaaani.....

Hongereni tena wakuu kwa ushindi huu mnono....
 
Mkuu....mimi ni Yanga
lakini imefika mahali nimenyoosha mikono juu na kusema msimu huu Simba
ni bora kuliko Yanga na ubingwa utakwenda Msimbazi, thanks to the genius
of King Kibadeni.

Timu yoyote yenye uwezo wa ku-cancel a 0-3 deficit hiyo ni championship
material. Simba msimu huu the championship is yours to lose!

Kwa Yanga, msimu huu timu hakuna but it is a bunch of expensive players
with full of ego ambao hawaichezei timu yetu kwa kujituma - labda Ngasa
tu.

sio mnaandika tu, hizo 3 za YANGA zimetoka wap? au zmeshushwa tu?
 
Balantanda, Mandieta, BabaV, Wabhejasana, naomba mkubali kuwa Yanga mmepoteza hii mechi kwa Simba.
 
Mkuu....mimi ni Yanga lakini imefika mahali nimenyoosha mikono juu na kusema msimu huu Simba ni bora kuliko Yanga na ubingwa utakwenda Msimbazi, thanks to the genius of King Kibadeni.

Timu yoyote yenye uwezo wa ku-cancel a 0-3 deficit hiyo ni championship material. Simba msimu huu the championship is yours to lose!

Kwa Yanga, msimu huu timu hakuna but it is a bunch of expensive players with full of ego ambao hawaichezei timu yetu kwa kujituma - labda Ngasa tu.

Mkuu Kiiza alivyofunga goli la tatu nikajua kabisa leo ni siku yenu ya kulipa zile sita, lakini kwa wana Simba walio wengi wameona hii droo imekuja kama kibahati ndo maana wengi wetu tunafurahi lakini wenzako wa Yanga wanatubeza na kutuuliza kwa nini tunashangilia droo hawatazami hata mazingira ya droo yenyewe ilivyokuja.
 
Wamejiuliza ndo maana wamezirejesha kiulaini kama kumtawaza mtoto aliejinyea [yanga].
I see.......

Simba kweli raha.....Hongereni sana kwa ushindi huu......Coastal na Azam nao lazima wapate kichapo kama hiki cha leo mlichoipa Yanga kwenye mechi hizi mbili zinazofuata
 
Teh teh bike la miti bhana a.k.a madingi dk ya 57 hoi pumzi ishaisha .....
 
I see.......

Simba kweli raha.....Hongereni sana kwa ushindi huu......Coastal na Azam nao lazima wapate kichapo kama hiki cha leo mlichoipa Yanga kwenye mechi hizi mbili zinazofuata

Mkuu pole tumekunyang'anya tonge mdomoni.
 
247686_1425543747658697_1996950327_n.jpg
 
cha kushangaza mabao yote 6 yameingia upande mmoja wa uwanja

Walisahau kuhamisha vile vimiziz vyao. so simba wakaponea hapo hapo.
KUANZIA KESHO SIGNATURE YANGU ITAKUWA... simba mnyama mtembea pekee porini. Ukimwona mjini kaja tu kufanya mishemishe
 
mkuu hii mechi hata imekuaje kuaje yani

Watu (back four yote ya Yanga) wapigwe bench hadi waaanze kupigania namba upya. That was schoolboy defending from Yanga defence!

Wakati wenzetu Simba sasa wana timu na wanacheza kitimu, sisi tumebakiwa na club ya wachezaji waliolewa umaarufu wa magazetini na kutukuzwa kusikostahili!
 
Balantanda, Mandieta, BabaV, Wabhejasana, naomba mkubali kuwa Yanga mmepoteza hii mechi kwa Simba.
Unaelewa maana ya kupoteza mechi?....Ama matokeo ya 3-3 kwa Simba dhidi ya Yanga siku hizi yana tafsiri mpya?.....

Simba hampaswi kushangilia 'ushindi' huu dhidi ya Yanga.....Mlipaswa kujiuliza kwa nini mmeshindwa kuifunga Yanga na kurudi kileleni mwa ligi....Matokeo ya leo hayana faida yoyote kwenu zaidi ya kuwabakisha nafasi ya 3 ambayo mlishushwa jana na Azam na Mbeya City.....Haya ni matokeo mabaya kwenu kutokana na mechi mbili zinazofuata dhidi ya Coastal Union( Itachezwa Tanga Jumatano hii) na Azam(Itachezwa Chamazi Jumamosi)....Yanga wao wana mechi na vibonde Rhino Rangers na Mgambo JKT ambazo zote zinachezwa Uwanja wa Taifa.....

Baada ya mechi hizi ndio mtakumbuka umuhimu wa mechi ya leo ambayo nyinyi ndio mlikuwa wenyeji....Yanga walikuwa ugenini leo.....

Ni shabiki maandazi pekee wa Simba ndio atashangilia sare ya leo.....
 
Mkuu pole tumekunyang'anya tonge mdomoni.
Binafsi siyasikitikii matokeo ya leo ambayo tulikuwa ugenini.....Ni kama vile Man Utd atoe sare Etihad kwa Man City.....Ni matokeo ya kawaida kabisa kwa mtu anayelijua soka na ambaye haendekezi ushabiki wa kizamani/ushabiki maandazi wa akina mzee Ibrahim Akilimali ambao Yanga kumfunga Simba kwao ni kama Yanga kuchukua ubingwa.....

Simba hampaswi kushangilia 'ushindi' huu dhidi ya Yanga.....Mlipaswa kujiuliza kwa nini mmeshindwa kuifunga Yanga na kurudi kileleni mwa ligi....Matokeo ya leo hayana faida yoyote kwenu zaidi ya kuwabakisha nafasi ya 3 ambayo mlishushwa jana na Azam na Mbeya City.....Haya ni matokeo mabaya kwenu kutokana na mechi mbili zinazofuata dhidi ya Coastal Union( Itachezwa Tanga Jumatano hii) na Azam(Itachezwa Chamazi Jumamosi)....Yanga wao wana mechi na vibonde Rhino Rangers na Mgambo JKT ambazo zote zinachezwa Uwanja wa Taifa.....

Baada ya mechi hizi ndio mtakumbuka umuhimu wa mechi ya leo ambayo nyinyi ndio mlikuwa wenyeji....Yanga walikuwa ugenini leo.....

Ni shabiki maandazi pekee wa Simba ndio atashangilia sare ya leo.....
 
I see.....

Hongereni sana kwa ushindi mkuu......

Kiukweli mlipaswa kusikitika kwa kukosa ushindi na kusindwa kurudi kileleni na kubaki nafasi ya 3 hasa ukizingatia mna mechi 2 ngumu za mfululizo, dhidi ya Coastal Union(inayofuata) na dhidi ya Azam(baada ya kucheza na Coastal.....

Yanga wana mechi rahisi ambazo zitawaezesha kuwashusha Simba kwenye msimamo wa Ligi......

Na hii ni mara ya kwanza kuona Simba wanashangilia sare dhidi ya Yanga.....Kipindi kile Yanga wamechomoa sare ya 4-4 Jangwani bado hakukukalika......Walijiuliza ni kwa nini wameruhusu magoli yale manne....Lakini kwa Simba ni burdaaaaaani.....

Hongereni tena wakuu kwa ushindi huu mnono....

Mkuu nadhani huamini kilichotokea, na ile 4-4 kama ni ile ya mwaka 1996, sare haikuwa ya mazingira kama ya leo maana ile mechi Simba ndo walisawazisha, alianza akafunga Kipese dak ya 7, Edibilly Lunyamila (penalti) dk. 28, Ahmed Mwinyimkuu dk. 43 akaipatia Simba bao la pili, Mustafa Hozza alijifunga dk 64 hivyo Yanga ikapata bao la pili, Dua Saidi dk. 60 akaifungia simba goli la tatu, Said Mwamba 'Kizota' dk. 70 akaandika goli la tatu kwa Yanga na dak ya 75 Sanifu Lazaro akafunga la nne kwa Yanga lakini dakika ya 90 Dua Said kwa mara ya pili akaifungia Simba goli la nne na matokeo kuisha 4-4. hivyo sare ile bado Simba ndo waliosawazisha kwa matokeo ya mwisho.
 
Walisahau kuhamisha vile vimiziz vyao. so simba wakaponea hapo hapo.
KUANZIA KESHO SIGNATURE YANGU ITAKUWA... simba mnyama mtembea pekee porini. Ukimwona mjini kaja tu kufanya mishemishe
walisahau kuhama na mzizi wao
 
Ila wana Simba tusisherehekee tu ushindi wa leo tuliomfunga Yanga bali ni sahihi sasa wa kuwakumbusha wale vibosile wetu wa Msimbazi ile ahadi ya kununuwa kila goli kwa cash, ahadi ni deni. Wawape vijana mpunga wao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom