Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Haya mambo yakiendelea hivi na kwingine ni wazi Tanganyika inarudishwa utumwani
Mwanzoni mwa wiki hii kituo kizuri cha daladala cha Mawasiliano Simu 2000 kilifungwa rasmi na fremu zote zinazohudumia kutoka ndani ya kituo kuvunjwa ili kumpisha mwekezaji mpya anayetaka kuweka karakana ya mabasi ya mwendokasi
Kwa siku tatu mfululizo pale Simu 2000 ilikuwa ni zogo hasa nyakati za jioni kwakuwa magari ya abiria toka kona zote za jiji yalikuwa yanasimama barabarani kupakia na kushusha abiria
Sasa zimechukuliwa hatua sijui ni za dharura ama la, 'kutengeneza kituo kipya' ndani ya soko la vyakula na matunda lililoko pembeni ya kituo
Imagine sehemu ya soko hilo ilivyo ndogo na isiyo na miundombinu ya magari hasa ya abiria sasa ni sehemu ya kupakia na kushusha abiria 🤔😭
Mahali palipokuwa panafanyika mnada wa mahindi, miwa nk sasa ni maegesho ya daladala kupakia na kushusha abiria
Hapana zege, hapana lami, hapajasindiliwa ni mavumbi kwenda mbele na zile vurugu za daladala
Usalama na usafi wa vyakula vinavyouzwa hapo sasa uko shakani kutokana na miundombinu hafifu, vurugu za daladala na wingi wa watu
Wafanyabiashara waliokuwa ndani ya kituo nao sasa wanabanana na wengine hapo sokoni
Sasa hivi hali ni hiyo ya vumbi je ikinyesha mvuta patakuwaje?
Dhana ya maendeleo na maamuzi kengeufu
Sijui huyo mwekezaji ana nguvu kiasi gani na sina hakika walioruhusu kituo kigeuzwe karakana kama waliwaza kwa weledi, hekima na uzalendo.. Kuondoa watu wote wale na uwekezaji wote ule na kusababisha adha ya usafiri na ongezeko la gharama kwa abiria na usumbufu mwingine mwingi ni maamuzi yenye kutatiza mno na shaka kubwa juu ya hekima ya waliobariki hilo zoezi!
Hata hivyo kama ilibidi kupisha maendeleo mengine basi haya yaliyokuwepo tayari yangetafutiwa mbadala mapema na kabla ya haya mapya. Nina hakika mwekezaji mpya kalipa pesa kulipata lile Eneo, sasa kwanini pesa hizo zisitumike kutengeneza mbadala wa kilichokuwepo ili kuepusha usumbufu, hasara na adha kwenye maisha?
Kwanini mwananchi mwenye nchi yake anayepaswa kupewa heshima, thamani na kipaumbele namba moja anageuzwa kama raia wa daraja la pili? Mtumwa anayepaswa kutii kila agizo bila kuhoji hata kama haki zake za msingi zinapokwa? Aende wapi sasa🥺
Pale Simu 2000 kuna kila aina ya harufu ya uvundo mkali wa maadili na uzalendo.. Waliofanya hiyo dili wakakubali sijui walipewa nini huko na walisainishwa mikataba ya aina gani huko! Maana ni wazi mwenye eneo kacharuka anataka eneo lake na wao walikuwa bado hawajajiandaa kulikabidhi kwake!
Soma Pia:
Je wametishwa? Na nani?
Kama mwekezaji kafaulu kufanya hivyo pale Mawasiliano Simu 2000 tujiandae kwa machungu mengi zaidi.
Tanganyika...!🤔🙇🏿♂

- Stendi Simu 2000 yafungwa rasmi kupisha ujenzi karakana ya mwendokasi
- Machinga wa Soko la Simu2000, Dar es Salaam wagoma na kufunga barabara asubuhi ya leo, Julai 8, 2024