Yaliyoko Simu2000 yanaumiza na kuhuzunisha sana

Kule Morogoro akili ni hiyohiyo, walifunga stand ya daladala ikageuzwa sehemu ya kuuzia dawa za nguvu za kiume
 
Waliofanya maamuzi hayo ni madiwani fikiria madiwani wa jiwe 2020 upeo wao.. wengi walikuwa waganga wa kienyeji.
 
Ngozi nyeusi ukichanganya na uchadema matokeo yake uwendawazimu! Kwaakili yako eti kisa ulikua unauzia maembe hapo sokoni ndio unataka BRT isijengwe? Foolish
 
Kwani hii mwendo kasi ya tegeta itakuwa na karakana mbili au? Maana pale mbuyuni yanapopaki malori ya mchanga na maeneo wanapojaza mchanga wa kuuza hadi kule kwenye makazi ya watu,nilisikia wanataka kulipwa ili pajengwe karakana ya mwendokasi,


Ila wananchi walifungua kesi kupinga kiasi cha pesa wanachotaka kulipwa,serikali ilipanga kuwalipa elfu arobaini kwa kila Square metr ya eneo,na na jengo pia linalipwa kwa bei yake kwa square metr na valuation nyingine,
 
Watu gani waliathirika kituo kikuu cha mabasi ya mikoani kilipohamia Mbezi Luois?

Si kituo kilijengwa kikakamilika ndio uhamisho ukafanyika?

Tusitetee upuuzi penye makosa ya wazi kwa sababu ya tofauti za kiitikadi
Mkuu, acha watu wapigike ili akili ziwakae sawa. Mwanzoni walipoambiwa watahamishwa walijaribu kupinga halafu nikamsikia kiongozi wao anasema wanaomba rais msikivu asikie kilio chao, na wameshaamua kumpa tena miaka mitano. Eti ''mitano tena kwa mama''. Mijitu mizuzu inayojipendekeza kama hii hamna namna nyingine ya kuifundisha.
 
Inasikitisha mno!
 
Pale manapageuza maegesho.. Simu 2000 wanataka kuweka karakana

Ile ilikuwa stand ya muda tuu. Japo huo muda umekuwa mrefu kuliko ilivyo tarajiwa
Sio kweli,stand ya makumbusho ilikuwa ya kudumu,ya mwenge ndio ilikuwa ya muda enzi zile
Sasa sijajua nn kimefanya stand ya Mwenge irudi na Kama kweli ya makumbusho inaondoshwa Basi utakuwa ni muendelezo ya mipango ya kukurupuka iliyozoeleka nchi hii
 
Maandiko matakatifu yanasema heri kijana masikini mwenye hekima kuliko mfalme mpumbavu.... Kwa Dunia ya sasa unaweza sema "heri kijana mwenye maarifa asiye na elimu ya darasani kuliko kiongozi mwenye elimu ya darasani asiye na maarifa...

Itoshe tu kusema Elimu yetu inafanya Viongozi wetu wazidi kuwa wajinga tena mbaya zaidi pale wanapo ongeza degree master nakuendelea..
 
Huu ujinga wameufanya pia kituo cha kivukoni (feri)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…