Yaliyoko Simu2000 yanaumiza na kuhuzunisha sana

Watu waandamane
 
Ehee.
Sasa wewe niliposema jangwani eneo la wazi lipo.wewe ulidhani jangwani gani?
Nlikuuliza Jangwani mtu mwenye akili timamu anaweza kwenda jenga yard ya magari hapo? Hakuna mwenye akili timamu anaweza enda pale Jangwani kujenga karakana ya Magari. Only a fool.
 
Kule Morogoro akili ni hiyohiyo, walifunga stand ya daladala ikageuzwa sehemu ya kuuzia dawa za nguvu za kiume
Hasa pale morogoro walichemka mazima. Hadi sasa hapaeleweki.. stand ya kule cjui wapi mafiga haitumiki kabsa.. kuna muda ile stand mpya iligeuzwa eneo la mnada wa nyama choma za kimasai
 
Nlikuuliza Jangwani mtu mwenye akili timamu anaweza kwenda jenga yard ya magari hapo? Hakuna mwenye akili timamu anaweza enda pale Jangwani kujenga karakana ya Magari. Only a fool.
Samia alitaka kujenga mradi wa nyumba elfu 14,000 na daraja Jipya la jangwani na yeye hana akili?
 
Samia alitaka kujenga mradi wa nyumba elfu 14,000 na daraja Jipya la jangwani na yeye hana akili?
Ujenge nyumba Jangwani? Una akili kweli? Yale maji yanayojaa pale unapeleka wapi? Jamani nyie kwa nini hampendi kutumia akili? Imeiona karakana ya magari ya mwendokasi? Ikinyesha mvua inakuaje?

Daraja BIG YES. MAKAZI NI KUTOTUMIA AKILI. THEN MAJI YA MTO MSIMBAZI YAENDE WAPI?
 
Kwa hyo wewe una akili sana kushinda benki ya dunia na watu wake?
Na mkopo walishatoa kuijenga jangwani uwe mji wa kisasa.na fidia walishaanza kulipwa watu.unaishi wapi?
Shida mradi umekufa samia kala hela.
 
Huu ndio ufujaji wa mali za umma mkuu,gharama iliotumika kutengeneza eneo lile ni kubwa sana na sasa wanaenda mwaga petrol na diesel chafu,huyo muwekezaji km sio muarabu sijui imeikosakosa atakua mchina,hii nchi mpk waliopo sasa wakiondoka tutauzwa mpk sisi wenyewe hawaachi kitu
 
Mwekezaji how? Mradi wa mwendokasi si mradi wa serikali?
 
Katakana ilikuwa iwe ubungu bus terminal(stendi ya mkoa zamani)
Walipompa mchina ndiyo wakaamua kuwaondoa watu sm2000

Ova
mmmh mkuu hakiki taarifa zako...Leo nimeenda kupiga picha za gari la kuuza pale ubungo, jengo la mchina lipo kwa mbele na pakin ya mwendokasi ipo kwa nyuma tena kuna Barabara kabisa inatenganisha, una hoja lakini unachanganya changanya mambo ,hakiki chanzo Cha taarifa zako
 
Kwanini mwananchi mwenye nchi yake anayepaswa kupewa heshima, thamani na kipaumbele namba moja anageuzwa kama raia wa daraja la pili?

Hawa raia nao tunawahitaji wajitokeze kwa uwingi wao tarehe 23 September 2024 kwa maandamano kupeleka ujumbe kwa watawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…