Yaliyomfika Rais Ali Hassan Mwinyi katika utawala wake 1985 - 1995

mlimtetea Mwinyi kisa OIC sio jambo lolote la kisiasa;

Mzee katika jukwaa hili udini wako uonekana waziwazi,huo ni mfano wa mawazo finyu!

Yaani Mwinyi hakuwa na issue ngumu za kumtetea hadi OIC?,
 
Ahahahahaha! Umeeudi tena. Kwakuwa Laigwanan Mzee Lowassa sio Mwislamu hata kutoa pole hapana, bali unamzunguzia Mzee Sykes wa miaka dahali! Haya bwana!
 
Nimeshaelewa kwa nini Nyerere aliivunja EAMWS.
 
Nimeshaelewa kwa nini Nyerere aliivunja EAMWS.
Yoda,
Mtihani mkubwa aliokuwanao Nyerere ilikuwa atatatua vipi tatizo la Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.

Alikuwa keshafanikiwa kuivunja EAMWS kilichobaki ni kuitisha mkutano wa masheikh vibaraka waunde jumuiya mpya ya Waislam na ufanyike uchaguzi wa viongozi.

Masheikh vibaraka wakawa katika mtanziko.

Vipi tuitishe uchaguzi wa viongozi wa Waislam ilhali miongoni mwao hayuko Sheikh Hassan bin Ameir?

Hili litawezekana vipi?

Sheikh gani atakuwa na ujasiri kukubali uongozi wa Waislam wakati Sheikh Hassan bin Ameir yuko Tanganyika na anasomesha darsa zake misikitini?

Kizingiti hiki kilikuwa kikubwa.

Madam Mufti Sheikh Hassan bin Ameir yuko Dar es Salaam hilo halitawezekana.

Waislam wakapanga kuitisha mkutano Ukumbi wa Arnautoglo wawajadili masheikh vibaraka wanaotaka kuvunja umoja wa Waislam.

Hizi zilikuwa juhudi za vijana wa Sheikh Hassan bin Ameir Mussa Kwikima na Bilal Waikela.

Allah kwa rehema zake amejaaliwa kuwepò mapenzi makubwa baina ya yangu na Mzee Waikela na Kwikima pamoja na Hamza Aziz.

Tukawa pamoja hadi wote walipotangulia mbele ya haki wakiniacha mpweke.

Wote hawa nimewaandikia taazia huku nikimwagikwa na machozi ndani ya moyo wangu.

Mzee Waikela na Wakili Msomi Mussa Kwikima juu ya udogo wangu wa umri na kila kitu wakija Dar-es-Salaam lazima watakuja nyumbani kwangu kunisalimu.

Mimi na Hamza Aziz tulikuwa na Majlis yetu nyumbani kwake kibandani ufukweni.

Nimechota mengi kutoka kwao.
Alhamdulilah.

Vipi utapatikana uongozi nje ya Sheikh Hassan bin Ameir?
Nyerere akawa kapwelewa.

Akamwagiza Said Ali Maswanya Waziri wa Mambo ya Ndani ampe amri Hamza Aziz amkamate Sheikh Hassan bin Ameir kwa tuhuma za kupanga kupindua serikali.

Hamza Aziz akakataa kutii amri ya kumkamata Mufti.

Maofisa wa Usalama wa Taifa ndipo wakaenda wao nyumbani kwa Sheikh Hassan bin Ameir Magomeni usiku kumkamata.

Nyumba hii haipo mbali na nyumba ya Maalim Matar.

Kwa miaka mingi mimi nikiamini kuwa Sheikh Hassan walimtoa kitandani amelala.

Mwanafunzi wa mwanafunzi wa Sheikh Hassan bin Ameir simjui hanijui aliniona nje ya Msikiti wa Kichangani akanieleza kuwa amenisikia mara nyingi nikisema kuwa Sheikh Hassan alikuwa kavamiwa usiku.

Yule kijana akaniambia kuwa mwalimu wake amemweleza kuwa Sheikh Hassan alikuwa anajua kuwa usiku ule atakuja kukamatwa.

Sheikh alivaa nguo zake vizuri akakaa nyumbani kwake akiwasubiri huku anavuta uradi.

Walipogonga mlango wake akawatokea kuwakabili.
Ndege ilikuwa tayari imetayarishwa.

Sheikh Hassan hakurudi tena Tanganyika hadi umauti ulipomfika.

Baada ya kuwa sasa Sheikh Hassan bin Ameir hayuko tena kwenye ardhi ya Tanganyika ndipo masheikh vibaraka wakafanya mkutano wao Iringa na BAKWATA ikaundwa.

Chuo Kikuu kilichokuwa kinajengwa na EAMWS ndiyo ukawa mwisho pamoja na miradi yote ya elimu.

Inatosha.
Nimekuongezea ili somo hili ilijue vyema.
 
Hii [emoji115] sababu ina mashiko zaidi.
 
Mikadala ya kuheshimiana mzee wangu wewe binafsi huiwezi.

Na ndio mada ziko Zina elements za udini.

Unachokoza mada unajua kabisa content yake italeta mihemko na kuvunjiana heshima. Kujimwambafy na Kila upande kuvutia kwake. Hio kuheshimiana itatoka wapi.

Mwinyi kwa nafasi yake sidhani kama alihitaji msaada wenu

Sema nyie wanaharakati wa kidini mliiona fursa na mkaitumia barabara!
 

Sema nyie wanaharakati wa kidini mliiona fursa na mkaitumia barabara!
Mangungo...

Mimi ningekuwa si muungwana na kalamu yangu nisingetunukiwa Mwandishi Bora Jukwaa la Historia kwa miaka miwili mfululizo.

Mimi ningekuwa naandika dini ya Kiislam kuwalingania watu nisingezungumza University of Iowa, Northwestern University, University of Johannesburg, University of Ibadan, Kenyatta University, University of Dar-es-Salaam, Sokoine University, State University of Zanzibar, Zentrum Moderner Orient na kwengine kwingi.

Mimi sijachokoza mtu yeyote niko hapa nasomesha historia ambayo nyie wote hamkupata kuifahamu hadi kilipochapwa kitabu cha Abdul Sykes London 1998.

Hili la kuwa nina heshima katika uandishi si mimi wa kukueleza wewe hilo.
Iulize nafsi yako itakupa jibu.

Na wala sina uwezo wa kukuzuia kukejeli.

Unaweza kuendelea kufanya hivyo nami nitaendelea kusomesha historia hii.

Niko hapa huu mwaka wa 16 nasomesha historia ya uhuru wa Tanganyika kama ilivyokuwa na nimeelimisha wengi.
 
Shida ya mleta mada ni udini, karibu kila kitu anakileta na kukitetea kwa mrengo wa dini ya kiislamu. Hii sio sawa na sio sahihi. Leo anamzungumzia Mwinyi hapa kwa misingi ya kidini, hivyo atampamba kwa lolote kwa sababu Mwinyi ni muislamu.
Ndioo,udini,udini, udini,hilo ndio tatizo kubwa,ila mleta mada akivua hiyo miwani ya udini,kuna mengi atayaona.
 
Shida ya mleta mada ni udini, karibu kila kitu anakileta na kukitetea kwa mrengo wa dini ya kiislamu. Hii sio sawa na sio sahihi. Leo anamzungumzia Mwinyi hapa kwa misingi ya kidini, hivyo atampamba kwa lolote kwa sababu Mwinyi ni muislamu.
Wakati yeye analalamika na kuwamezesha wenzie sumu.Wengine wako busy kujiimarisha kitaasisi kuanzia ngazi ya Jumuiya hadi jimbo.Ifikapo 2035 kila jimbo la kanisa Katoliki litakuwa na chuo kikuu.Usimwamshe aliyelala!
 
Nimekuja gundua sumu yako inaenea sana kwa waislamu.Juzi moja nimekutana na mtu ana chuki ya waziwazi kwa Wakristu na anaelezea kile unachokihubiri humu.Baada ya kumchallenge siku hizi hanisalimii.Kinachofurahisha ni jobless anayeshinda misikitini akipiga mazoezi ya Karate
 
Nyerere alikuwa na akili mingi muno
 
Porojo as usual
 
MJOMBA SAID BILA KUMTAJA HUYO MZULU SYKES BASI UZI HAUKAMILIKI.......NA BILA KUSIFIA WABANTU WALIOCHUKUA TAMADUNI ZA KIARABU UZI HAUKAMILIKI 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 HAPO BADO HUJATUDANGANYA KUHUSU JIHAD YA MAJIMAJI............SASA TUKUAMINI WEWE AU BABU ZETU WALIOPIGANA NA WAJERUMANI 🤣🤣🤣
 
WEWE UNAMCHUKIA NYERERE NA KARUME SABABU WALIWAONDOA WAKOLONI WA KIARABU NA VIZAZI VYAO VYA MACHOTARA KATIKA UONGOZI.........!!!
😂🤣🤣🤣🤣�
Mjomba nadhani ww mpaka leo upo radhi kua mtumwa wa waarabu wa Oman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…