Yaliyompata Pinokyo: Inasikitisha kuwa kuna watu wazima bado wanatapeliwa namna hii.

Yaliyompata Pinokyo: Inasikitisha kuwa kuna watu wazima bado wanatapeliwa namna hii.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Nchi ingekuwa na utaratibu wa kusoma soma toka watu wakiwa wadogo, watu wengi sana wangeepuka kuishi Mji wa Mtego wa Wajinga.

MBWEHA: Na fedha zako je?

PINOKYO : Ninazo. Niliziweka mfukoni. Inakosekana pauni moja tu, niliyotumia kumlipa Bwana-hoteli.

MBWEHA: Lakini niambie: umekwisha fahamu kwamba pauni hizo chache zingeweza kuzidishwa, hata kupata kama pauni elfu moja-mbili hivi? Kwa sababu gani hutaki kufuata shauri langu? Kwa nini hutaki kwenda kuzipanda katika Shamba la Miujiza?

PINOKYO: Leo siwezi, siwezi kabisa! Nitakwenda siku nyingine.

MBWEHA: Siku nyingine? Namna gani tena? Ukichelewa, shauri lako. Naam yakupasa ujue kuwa shamba hilo limekwisha uzwa kwa bwana mwingine; amelinunua leo hivi. Kesho watu watakatazwa wasipande tena fedha za kuzidishwa.

PINOKYO: Nasikitika sana. Lakini . . . . shamba hilo ni mbali kiasi gani?

MBWEHA: Aha! Ni karibu tu. Tuseme kama maili moja hivi. Wataka kusindikizwa nasi? Tutalifikia Shamba la Miujiza katika muda wa nusu saa. Nawe utapanda fedha zako. Kitambo kidogo utachuma pauni zilizozidishwa, ukajaze mifuko yako kabisa. Basi wataka? Wapenda? Unakubali?

Pinokyo alikuwa akisitasita asiweze kujibu kitu, kwani alikuwa akikumbuka Jini Mwema na baba yake mzee, na mashauri ya Chenene-Msemaji. Hatimaye lakini alikata shauri la kushika njia ya watoto wasio na akili wala moyo, maana alitikisa kichwa, akamwambia Mbweha na Paka: "Haya twendeni! Nawafuateni tu.!"

Wakatembea sana kama saa nne, tano hivi. Wakaufikia mji uitwao Mtego-wa-wajinga. Alipokwisha ingia katika mji huo Pinokyo aliwaona Mbwa wengi wenye madonda- donda, nao walikuwa wakipiga miayo kwa ajili ya njaa kali. Hata alikutana na kondoo waliokatwa manyoya na kutetemeka kwa baridi. Vile vile aliona jogoo waliopotewa undu. Wote walikuwa wakiomba yala maskini kwa watu, kipande kimoja cha chakula cho chote, watulize njaa yao. Vipepeo wengi walikuwapo, wasiweze kurukaruka, kwani walishurutishwa kuyauza mabawa yao ya rangi rangi. Tausi wengi walipotewa na mkia. Umati huu wa maskini ulikuwa ukiangalia gari nzuri sana zilizokuwa zikipita mbele yao: ndizo gari za Mbweha, Paka, au ndege fulani wa usiku. Pinokyo akamwuliza Mbweha.

PINOKYO: Shamba la Miujiza liko wapi?

MBWEHA: Ni hapa, karibu sana.

Wakapita mjini kwenda nje ya ukuta uliozungushwa mji. Wakasimama . . . . Wakasimama katika shamba lililokuwapo, mbali na watu. Shamba hilo lilikuwa sawa sawa kama vile mashamba mengine.

Hapo Mbweha akamwambia Pinokyo:

MBWEHA: Tumekwishafika. Sasa inama, kachimbe shimo.

PINOKYO: Lo! liko wapi jembe?

MBWEHA: Aha! Jembe si lazima! Sharti utumie mikono mitupu. Chimba shimo dogo basi, kaweke pauni zako.

Pinokyo akamtii Mbweha, akachimba shimo, akaziwekapo pauni zake alizo nazo, akafunika shimo kwa udongo. Mbweha akaendelea: "Sasa nenda chemchemuni, kateke maji kidogo, umwagilie pauni ulizopanda".

Pinokyo akafanya hivi. Lakini hakuwa na ndoo wala sufuria. Basi akashika kiatu kimoja na kuchota maji kidogo. Akamwagilia pauni alizopanda. Mwishowe akamwuliza Mbweha:

PINOKYO Sasa! Nifanyeje?

MBWEHA: Sasa? . . . . Sasa basi. Hakuna neno jingine la kufanya. Sasa tunaweza kwenda. Wewe lakini, kitambo kidogo, tuseme kama dakika kumi hivi, rudi hapa. Utaona! Utapata mti mdogo uliokwisha kua, ukaona matawi yaliyojazwa na pauni zisizohesabika.

Mwanasesere mjinga sana akamshukuru Mbweha na Paka pia kwa moyo, akawaambia.

PINOKYO: Nitakapovuna shilingi na pauni zilizozidishwa, nitawapa zawadi kweli kweli.

MBWEHA: Sisi hatutaki zawadi yo yote. Tunaridhika kwani tumekufundisha njia ya kujitajirisha pasipo kushughulika mno.

Walipokwisha sema maneno hayo, wakamwambia Pinokyo kwa heri ya kuonana, wakaenda zao.
 
Back
Top Bottom