Aahahahahaha umenichekesha kama si kunifurahisha looh
Kwanza jiulize kwanini uliamua kuwaiga hao unaowaita matajiri, na jiulize kwanini wao matajiri wanakula matunda mchana??!!! ulichunguza kwamba labda ni wagonjwa na sehemu ya tiba ya ugonjwa wao ni kula matunda tuu mchana?
Well kuna kipindi nilifanya majaribio na mwili wangu nikagundua mwili wa binadamu una uwezo mkubwa sana wa kuhimili vitu vingi unavyovikabili. Binafsi pia ni muasisi wa kula matunda, kipindi flani kuna hawa watu wa dini wanitwa mashahidi wa Yehova walinipa vitabu vyao wakanielimisha kuhusu yao na kusema kwa upana kuhusu bustani ya eden na mpango wa Mungu juu ya mwanadamu ulikuwaje.
Nikaanza kujiuliza je nikiishi kwa kula matunda tuu ntapata madhara yeyote, ntadhoofika? ntakuwa kama zamani?
nikajipa wiki moja ambayo sigusi chakula cha kiwandani au kilichochakatwa kwa asilimia 90. Maana yake ntakula chakula kilichochakatwa kwa asilimia 10 ambayo madhara yake hayataonekana. Maji nilikuwa nayanywa sana, matunda aina zote nakula kuanzia zambarau hadi mastafeli, na nakula mengi hadi nasikia hakuna nafasi tumboni. Matunda yanaisha haraka tumboni na baada ya hapo nikisikia njaa ni maji hadi mlo unaofuata. Sikuwa na mid snack na nilitaka kufanya hivi ili kujihakikishia immunity yangu na mwili uta respond vipi na nnchokifanya.
Niliona mabadiliko kwenye mwili wangu ila sikuwahi kuugua wala kuumwa wala kudhoofika sana sana nguvu ziliongezeka mara dufu nyege zikawa zinanipanda kila siku, ila sijajsema kama matunda yanaongeza nyege aahahahahaa
Pia shughuli unazozifanya ni zipi? ngumu au za kukaa kwenye kiti kuanzia saa 2 hadi saa kumi na moja jioni? kama unafanya kazi za kutumia nguvu kuliko akili ni wazi hili zoezi litakunyong'onyeza. Ila kama shughuli zako ni za kukaa kwa asilimia 90, endelea. Matunda ni chakula kizuri sana.