Yaliyotokea UDA ndiyo yatakayoipata Simba.

Yaliyotokea UDA ndiyo yatakayoipata Simba.

Nyie watu mna fikra za kijamaa kwenye hela za watu. Yaani huwa mnataka Klabu iwe na "Mfadhili" ila huyo mfadhili akitaka awe mmiliki mnaanza gubu. MO anavyotoa hela alizopata toka kwenye biashara zake huwa mnadhani anatoa kwa kuwa hana kazi nazo?

Tatizo la Simba ni "Uswahili". Unaposema unampa mtu hisa si lazima zikokotolewe toka kwenye thamani ya rasirimali zilizopo. Leo hii nani anajua thamani ya Simba?

Mnataka MO atoe bilioni 20 kwa yale Majengo yenu mawili pale Msimbazi na ule uwanja wa Bunju ambao haujaendelezwa?
Kwanini alikabidhiwa timu kabla ya mchakato haujakamilika wa kuhakiki mali za simba? Kwanini ilitangazwa atatoa 20b kabla ya tathimini ya mali za simba? Huo uharaka wa kupewa timu ulitoka wapi?
 
Uwekezaji isiwe chanzo cha kuwauzia timu watu
Hata Huyo unayempigia vigelegele aliwekeza African lyion yakamshinda akatimua mbio
Ebu jitangaze kwanza kama ni mwana simba au mwana yanga, duniani kote tumeona mchezo wa mpira wa miguu ukipiga hatua kubwa kwa kupata uwekezaji mkubwa. Kama unataka tembeza bakuli endelea tu lakini kama wapo wanaojua mpira ni biashara wapewe nafasi, yote ni kukuza uchumi na kuongeza ushindani. Nakushauri ukatafte hata timu ya kijiji ujaribu kuwasaidia ili uwe na uelewa mpana wa unachokisema
 
Wao wako Bize wanataka atoe hela, lakini swali rahisi la thamani ya Klabu ya Simba ni shilingi ngapi wanashindwa kulijibu. Wanaishia kusema wana hati ya Klabu inayoitwa Sunderland!!
Kama MO aliaminiwa akapewa timu bila tathini basi naye atoe mpunga kwanza
 
Timu hapewi mtu km chips, timu inaruhusu watu wanaokidhi vigezo wafuate sheria kuwekeza
Walijitokeza wengi tu waliotaka kuwekeza simba, ila kuna mtu alihonga sana
Hivi hata wewe ukipewa timu ya Simba unaweza ukaiendesha?
 
Huyu Mr MO amekabidhiwa simba bila hata kutoa fedha ambazo zinampa share anazo miliki.

Sinahakika kama huyu bwana anahitaji simba zaidi ya kutaka raslimali za simba kwa ajili ya biashara zake na matangazoya biashara zake kwa kupitia simba.

Tunaomba vyombo vya usalama wekeni macho yenu karibu. Hatutaki mambo ya UDA yatupate club kwongwe na yenye heshima kama simba.

Yangu macho.
Unasema hajatoa kitu wakati habari za kitaa zinasema yeye ndio mlipa mishahra na mtoa fedha za usajili?
 
Wao wako Bize wanataka atoe hela, lakini swali rahisi la thamani ya Klabu ya Simba ni shilingi ngapi wanashindwa kulijibu. Wanaishia kusema wana hati ya Klabu inayoitwa Sunderland!!
Wacha hizo bwana, kwani wkt analeta zabuni yake ya 20b alikuwa hajui afanyalo? Tuanzie hapo
 
Akili za wabongo! yaani upigwe kivip? hiv pale simba ww unamiliki nn? au na ww nishabk tu kama tulivyo wengine
Sisi tunataka maendeleo ya timu yaani timu ifanye vizur Lig kuu bongo na mashindano mengine na kufanikisha hli nilazia timu iwe na pesa zakutosha sasa kati ya kilomoni na mo nani anaweza kua pesa za kuweka pale simba?
Mkuu hawa mashabiki wa yanga msipoteze muda kubishana nao...washachelewa sana
 
Mi mshabiki Furaha yangu ni kuona simba inafanya vyema
 
kiukweli huu mchakato uliendeshwa haraka na kihuni wengi wanaangalia mafanikio ya Simba msimu ulioisha lakini hawataki kuzungumzia kabisa jinsi gani mchakato ulivyotakiwa uwe.Simba ilifanya mchakato bila thamani yake halisi kujulikana ukitaka kujua thamani ya Simba haikujulikana bei ya kununulia hisa 51 na hisa 49 ni ileile.
Simba ilianza kupokea pesa ya Mo kabla hata ya kuanza mchakato wa kugeuza mfumo wa klabu kitendo hicho kiliondoa ushindani wa watu wengine kujitokeza.Anachotaka kufanya sasa hivi Mo dewji cha kujua hesabu za Simba pamoja na madeni kilipaswa kufanywa kabla mchakato haujaanza mtashangaa Mo hatatoa bilioni 20 akiweka madeni na peza alizotoa sanasana mnaweza kuambulia milioni 200.Mwisho thamani ya Simba haihusishi uwanja wa bunju au jengo la msimbazi bali na idadi ya washabiki ilionao ndio maana alishindwa kuziendesha African Lyon na Singida United ,
Mwisho zinahitajika busara za pande zote mbili ili kutovuruga kila kilichoanzishwa,
 
Nimekuuliza club ya Simba na mzee kilomoni wametoa shilingi ngapi?
Maana moo sio mmiliki wa SIMBA.
Ana shareholder na simba sports club.
Thamani ya majengo pamoja na mashabiki na wanachama wa simba ndio thamani yao ni 51%.
 
Makwasukwasu fc,wana wivu sana,wameshupalia masuala ya Simba mpaka wanasahau kutembeza bakuli!!!kazi yote wamemuachia yule mbunge wa Dodoma mjini.ukiuliza mbona bakuli mmelitelekeza kwa yule mgogo,wanaishia kusema yule anauzoefu na kuomba omba.
 
kiukweli huu mchakato uliendeshwa haraka na kihuni wengi wanaangalia mafanikio ya Simba msimu ulioisha lakini hawataki kuzungumzia kabisa jinsi gani mchakato ulivyotakiwa uwe.Simba ilifanya mchakato bila thamani yake halisi kujulikana ukitaka kujua thamani ya Simba haikujulikana bei ya kununulia hisa 51 na hisa 49 ni ileile.
Simba ilianza kupokea pesa ya Mo kabla hata ya kuanza mchakato wa kugeuza mfumo wa klabu kitendo hicho kiliondoa ushindani wa watu wengine kujitokeza.Anachotaka kufanya sasa hivi Mo dewji cha kujua hesabu za Simba pamoja na madeni kilipaswa kufanywa kabla mchakato haujaanza mtashangaa Mo hatatoa bilioni 20 akiweka madeni na peza alizotoa sanasana mnaweza kuambulia milioni 200.Mwisho thamani ya Simba haihusishi uwanja wa bunju au jengo la msimbazi bali na idadi ya washabiki ilionao ndio maana alishindwa kuziendesha African Lyon na Singida United ,
Mwisho zinahitajika busara za pande zote mbili ili kutovuruga kila kilichoanzishwa,
Ww jamaa ni kiazi kabisa,kipindi mchakato unaanza hadi kupitishwa ulikuwa wapi kutoa haya maoni yako?!!au ulikuwa kwenye "coma".
 
Back
Top Bottom