kiukweli huu mchakato uliendeshwa haraka na kihuni wengi wanaangalia mafanikio ya Simba msimu ulioisha lakini hawataki kuzungumzia kabisa jinsi gani mchakato ulivyotakiwa uwe.Simba ilifanya mchakato bila thamani yake halisi kujulikana ukitaka kujua thamani ya Simba haikujulikana bei ya kununulia hisa 51 na hisa 49 ni ileile.
Simba ilianza kupokea pesa ya Mo kabla hata ya kuanza mchakato wa kugeuza mfumo wa klabu kitendo hicho kiliondoa ushindani wa watu wengine kujitokeza.Anachotaka kufanya sasa hivi Mo dewji cha kujua hesabu za Simba pamoja na madeni kilipaswa kufanywa kabla mchakato haujaanza mtashangaa Mo hatatoa bilioni 20 akiweka madeni na peza alizotoa sanasana mnaweza kuambulia milioni 200.Mwisho thamani ya Simba haihusishi uwanja wa bunju au jengo la msimbazi bali na idadi ya washabiki ilionao ndio maana alishindwa kuziendesha African Lyon na Singida United ,
Mwisho zinahitajika busara za pande zote mbili ili kutovuruga kila kilichoanzishwa,