Tajiri wa kusini
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,079
- 2,947
Maneno ya mwisho niliyomwambia ni kuwa, "Huwezi kupata mwanaume mwingine kama mimi, ondoka, lakini najua utarudi, mjinga wewe!" Miaka miwili iliyopita nilifunga ndoa na mke wangu wa sasa. Kipindi hicho nilikuwa nimetoka kuachana na mpenzi wangu wa muda mrefu ambaye tuliishi naye kama mke na mume kwa miaka 12, lakini hatukufunga ndoa.
Ni mwanamke ambaye tulianza naye mahusiano tangu kipindi tumemaliza chuo, yeye alikuwa akifanya kazi ya mama lishe, akilipwa shilingi elfu mbili na mia tano kwa siku. Biashara yetu ya kwanza kufungua pamoja ilikuwa ni kutengeneza ice cream. Wakati tunakutana, tuliamua kuanza maisha pamoja. Mimi nilikuwa na friji, nikamchukua na vitu vyake kidogo tukaanza pamoja.
Tulianza kwa kuuza barafu, kwani mahali alipokuwa akifanya kazi kulikuwa na wateja walionunua barafu. Tulipoanza kutengeneza ice cream, biashara hiyo ndiyo iliyotutoa. Yeye aliacha kazi ya mama lishe, na mimi nikaacha kuokota vyuma chakavu.
Tulijikusanya, na baada ya muda tukapata mtaji wa laki saba. Tukakubaliana kununua bodaboda used ambayo mimi ndiyo nilikuwa naendesha, naye akaendelea na biashara ya ice cream. Ilitusumbua sana, mpaka tukaiuza ile bodaboda kwa bei ya hasara laki tano. Rafiki yake, mwalimu, alihitaji mtu wa kumuandeshea pikipiki yake kwa mkataba, akaniunganisha naye.
Tulianza kulipa mkataba wa elfu kumi kwa siku, lakini sisi tulifanikiwa kupeleka elfu ishirini. Yeye alikuwa anajikusanya hela za ice cream, na mimi upande wa bodaboda. Tulihangaika sana mpaka tulipopata mtoto wetu wa kwanza, tulikuwa na pikipiki tatu. Mungu akatujalia, tukaacha biashara ya pikipiki na ice cream, tukafungua duka la spea. Hapo ndipo nilianza kujihisi kama mwanaume. Ndugu waliokuwa wananiona kama mtu wa kawaida tu, walianza kuniheshimu. Nakumbuka wakati mke wangu alipojifungua mtoto wetu wa pili, mama yangu alikuja kwa mara ya kwanza kutembelea, lakini hakuna ndugu hata mmoja aliyejua kuwa tuna nyumba yetu.
Baada ya hapo, ndugu walikuwa wanakuja kuomba ada, sijui matibabu, mitaji na kila kitu, na mke wangu alikuwa anazungumzwa vibaya, wakisema hataki ndugu, ananiloga. Tulipambana, tukafanikiwa kununua gari. Hapo ndipo ndugu walipozidi kunipa heshima, lakini nikaanza kumdharau mke wangu. Nilianza kumwona kama vile hana mchango wowote kwenye mafanikio yetu, kama vile alikuja bila chochote. Ilikuwa ngumu kwangu kuendelea kumheshimu.
Kweli, niliacha kumpenda mke wangu, na niliacha kumjali. Kuna kipindi nilikua naongea na wanawake wengine mbele yake na kumtu*kana mke wangu, lakini sikujali. Mwisho mama yangu alinitafutia mwanamke mwingine na akaniambia, "usipomuoa huyu, basi mimi si mama yako." Nilifunga ndoa ya kanisani kimya kimya bila mke wangu kujua, lakini baadaye ndugu zangu walimtumia picha zangu kumtukana, ndipo alipoamua kuondoka.
Kweli, ingawa nilimfanyia vituko, sikutaka aondoke. Nilipenda aendelee kubaki kwenye ile nyumba kama mke wangu ili aweze kulea watoto wetu watatu. Aligoma, na alipogundua kuwa nilifunga ndoa ya kanisani wakati yeye ilikua sogea tuishi tu, aliniambia anaondoka. Ndipo nilipomtukana nikijua kuwa, "Watoto watatu, hawezi kupata mwanaume wa kukuoa, utarudi kwangu tu." Nilimuondoa dukani na kuhakikisha hachukui hata shilingi. Nyumba na kila kitu niliandika jina la mama yangu nikijua kuwa hata akidai mali, haitawezekana.
Aliondoka na watoto, hakudai chochote. Nilipoona yuko kimya, nilidhani kuwa ana kiburi. Nilijaribu kumnyanyasa zaidi kwa kunyang'anya watoto, lakini watoto waligoma kuondoka nami. Akili yangu iliniambia kuwa amewajaza sumu, lakini bado nilijaribu kumlazimisha mtoto mkubwa aondoke namimi. Watoto wadogo nilikataa kuwahudumia, nikiamini maisha yakimshinda, atarudi kwangu.
Nilikata mawasiliano naye kabisa. Hata aliponipigia kuhusu matatizo ya watoto, sikumsikiliza. Niliishia kumtukana, nikimwambia, "atajua mwenyewe." Mwaka wa kwanza wa ndoa mpya ulikuwa mzuri; mke mpya alinisikiliza, alinijali, na nilijiona kama malaika. Ndugu walimpenda sana, lakini mwaka wa pili mambo yalibadilika. Mke wangu mpya hana mkono wa biashara, hajui pesa zinavyotafutwa. Matumizi yalikuwa makubwa sana. Nikaamua kumuondoa dukani nikamchukua mdogo wangu kumuweka dukani. Hapo ndipo niliharibu zaidi, kwani ndugu wengine walikuwa wanakuja dukani na kuchukua pesa kama kwao. Sikuweza kuzuia.
Baada ya muda, kelele zikaanza. Ndugu hawamtaki mke wangu mpya, wanataka nioe mwanamke mwingine. Wakanishauri nirudiane na X wangu. Nikawaambia, "hapana, sitaki." Lakini nilipobanwa na madeni benki, biashara ikawa ngumu sana. Fundi aliyekuwa tegemeo la biashara aliondoka na wateja. Nilijikuta nashindwa kuendelea.
Niliamua kuanza kufuatilai nikagundua kumbe X wangu amefunga duka la spea. Nilipofika pale, fundi wangu wa zamani amabye ndiyo alikua na wateja alikuwa amehamia kule, akachukua wateja wangu. Tuligombana sana, lakini haikusaidia. Sasa hivi nina mawazo mengi, kichwa hakitulii. Nimesikia kuwa X wangu anaolewa, nilizidi kuchanagnyikiwa zaidi kwani nilishapanga kumaucha mke wangu ili kuruidiana naye. Nilipata hofu hadi nikatafuta anayemuoa na kumwambia kuwa X wangu alikuwa mke wangu.
Nina watoto watatu, na nilimwambia mwanaume anayemuoa kuwa nina watoto naye na siwezi kumuacha ni mke wangu. Lakini alinijibu kuwa anajua na atasaidia kulea, usijali. Hilo jibu lilinikera sana, kwani niliamini kuwa mwanaume anayemuoa si mtu wa maana. Nilifikiri kuwa anampenda tu kwa sababu ana akili. Nilijaribu hadi kanisani kuweka pingamizi, lakini waliniambia, "wewe si ulioa? Ulizaa naye lakini si mke wake."
Alifunga ndoa, na sasa hivi niko tu. Kila nikiangalia maisha yake naona yanastawi. Nimepoteza mwanamke wa maisha yangu kwa sababu ya ujinga wa ndugu zangu. Natamani hata siku moja aachike nimrudie na kumuoa tena!