Yametimia: Hatimae Kibu Denis azungumzia sakata lake na Klabu ya Simba

Simba haijawahi kumwekea ngumu mchezaji yoyote aliyepata timu nje ya nchi, waliuzwa wachezaji wengi tu tena wakiwa kwenye viwango vya juu kabisa vya ubora hivyo hawawezi kumzuia Kibu aliyefunga goli moja tu msimu mzima, afuate sheria tu lakini siyo uhuni anaofanya atajikwamisha mwenyewe.
 
Nadhani tatizo sio kupata timu nje na mkataba unavyosema..shida ilikuwa kwanini hakuwepo kambini kabla hajatoa hii sababu, ilihisiwa ni utoro kazini, na si vinginevyo..hii sasa hata simba wenyewe wamekuwa surprised kuona ni deal la pesa hivyo wanaachana na tuhuma za utoro wake
 
Kibu kaharibu sana
Mi naona amefanya vizuri! Kwani, atauzwa kwa bei kubwa, kuliko ungefuatwa utaratibu. Hapo, ni kama binti mwanafunzi ametoroshwa, hivyo, jamaa atapigwa faini, pili atafungishwa ndoa ya mkeka. Jamaa akijifanya mjanja, atatishiwa kushtakiwa Serikalini (FIFA) ambako kwa kosa alilofanya, atajuta kwa adhabu atakayopata!
Sina shaka, hao Simba wamepata nguvu ya kurudi huko Congo kwa AS VITA, kwa kiwango kikubwa cha fedha, wakitegemea "mahali na faini" kutoka kwa Kibu!
 
Ngoja tuone itakuaje mkuu
 
BADO HAJASEMA.
Si niliwaambia huyu ATARUDI mwenyewe Simba,kama sio kuche basi kuomba kuondoka
 
Kwani Kibu aliongea na Simba wakagoma kumruhusu?

Tff ndio wanaomlipa mshahara Kibu? Mbona maajabu haya.

We Tangu uzaliwe uliwahi kuona wapi mchezaji kauzwa na shirikisho?πŸ˜€
Ndo hata mimi nashangaa...cz kumruhusu kama shrikisho maana yake hata thaman yake ya kumuuza wanalijua sasa
 
Kwa maelezo haya, basi viongozi wa simba, ulikosea saana.
 
Streka la bao moja mechi 50 linawapeleka puta makolo.
 
Kwani wewe umeuona mkataba wake?..........au ndio habari ya kusikia πŸ˜€
 
Yanga walikuwa na haki ya kumlilia Feisali maana kiwango kilikuwa kinaonekana ila Simba kumlilia Kibu daaaah ki ukweli ni kujishusha hadhi.
Hata walomchukua sijui waliangalia impact yake kwa msimu 2023/2024 au waliangalia nini.
Sema kila mtu na bahati yake
 
Timu Norway bhana.....ebu tuache πŸ˜€ πŸ˜€
 
Hatimae Kibu Dee aka Mkandaje awakanda waajiri wake
 
Kiwango hichohicho ndo kilifanya mchanganyikiwe na kuweka mezani mamilioni kupata saini yake.
ni kwa kuwa tulipata tetesi kuwa kuna timu inamuhitaji. Hata Jobe tulichelewa kumuaga bure kwa kuwa tulisikia kuna timu zinataka kumnunua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…