Yametimia: Hatimae Kibu Denis azungumzia sakata lake na Klabu ya Simba

Yametimia: Hatimae Kibu Denis azungumzia sakata lake na Klabu ya Simba

Simba haijawahi kumwekea ngumu mchezaji yoyote aliyepata timu nje ya nchi, waliuzwa wachezaji wengi tu tena wakiwa kwenye viwango vya juu kabisa vya ubora hivyo hawawezi kumzuia Kibu aliyefunga goli moja tu msimu mzima, afuate sheria tu lakini siyo uhuni anaofanya atajikwamisha mwenyewe.
 
Nadhani tatizo sio kupata timu nje na mkataba unavyosema..shida ilikuwa kwanini hakuwepo kambini kabla hajatoa hii sababu, ilihisiwa ni utoro kazini, na si vinginevyo..hii sasa hata simba wenyewe wamekuwa surprised kuona ni deal la pesa hivyo wanaachana na tuhuma za utoro wake
 
Kibu kaharibu sana
Mi naona amefanya vizuri! Kwani, atauzwa kwa bei kubwa, kuliko ungefuatwa utaratibu. Hapo, ni kama binti mwanafunzi ametoroshwa, hivyo, jamaa atapigwa faini, pili atafungishwa ndoa ya mkeka. Jamaa akijifanya mjanja, atatishiwa kushtakiwa Serikalini (FIFA) ambako kwa kosa alilofanya, atajuta kwa adhabu atakayopata!
Sina shaka, hao Simba wamepata nguvu ya kurudi huko Congo kwa AS VITA, kwa kiwango kikubwa cha fedha, wakitegemea "mahali na faini" kutoka kwa Kibu!
 
Mi naona amefanya vizuri! Kwani, atauzwa kwa bei kubwa, kuliko ungefuatwa utaratibu. Hapo, ni kama binti mwanafunzi ametoroshwa, hivyo, jamaa atapigwa faini, pili atafungishwa ndoa ya mkeka. Jamaa akijifanya mjanja, atatishiwa kushtakiwa Serikalini (FIFA) ambako kwa kosa alilofanya, atajuta kwa adhabu atakayopata!
Sina shaka, hao Simba wamepata nguvu ya kurudi huko Congo kwa AS VITA, kwa kiwango kikubwa cha fedha, wakitegemea "mahali na faini" kutoka kwa Kibu!
Ngoja tuone itakuaje mkuu
 
BADO HAJASEMA.
Si niliwaambia huyu ATARUDI mwenyewe Simba,kama sio kuche basi kuomba kuondoka
 
Kwani Kibu aliongea na Simba wakagoma kumruhusu?

Tff ndio wanaomlipa mshahara Kibu? Mbona maajabu haya.

We Tangu uzaliwe uliwahi kuona wapi mchezaji kauzwa na shirikisho?😀
Ndo hata mimi nashangaa...cz kumruhusu kama shrikisho maana yake hata thaman yake ya kumuuza wanalijua sasa
 
Madai ya kibu ni kwamba,hapo awali Kuna ofa kadhaa zilitoka Ulaya na zilipofika Kwa Simba ikawa Uongozi unambania kuondoka,na ndipo baada ya kufahamu ukweli huo kama unakumbuka ndipo drama zikaanza Kwa jamaa ya kwamba Kama wanataka abaki inabidi wamuongezee pesa!

Wakiwa wamemuongeza pesa alizohitaji,ndipo ofa nyingine kutoka Norway ya Kristiansund ikatua Kwa wakala wake,Kwasababu kabla ya Timu husika kufanya mazungumzo na Simba ilifanya mazungumzo na Kibu,ndipo jamaa baada ya kuona hiyo ofa akawazuia Kristiansund kufanya mazungumzo na Simba kwasababu alijua viongozi watamtilia ngumu kwasababu hapo awali zilishakuja ofa kadhaa wakamtilia ngumu


Jamaa baada ya kuona hivyo,akaamua kutoushirikisha Uongozi wa Simba hadi jambo lake litakapotimia,maana alijua akiwashirikisha Uongozi wa Simba,wangemwambia atumikie mkataba wake aliokwisha Saini wakati yeye ndoto zake ni Kucheza Ulaya,Hivyo baada ya kufika Ulaya ndipo Sasa wakakubaliana na Kristiansund wauandikie Uongozi wa Klabu yake ya Zamani (Simba) kuhusu ku-negotiate !

Kwa mantiki hiyo,Jamaa ameamua Kutoroka kwasababu hizo nilizotaja hapo juu!

Hii Taarifa nilisikiliza pale Wasafi wakati wakimuhoji huyo Meneja wake (Carlos Mastermind)
Kwa maelezo haya, basi viongozi wa simba, ulikosea saana.
 
Kwenye mkataba wa Kibu Denis na SimbaSC kuna kipengele walichokubaliana kuwa, akipata timu Ulaya aruhusiwe kuondoka.

Kipengele hicho ndicho kinampa uhakika na jeuri ya kuondoka katika klabu ya Simba.

ℹ️ Klabu ya Kristiansund BK imeandika barua rasmi kwenda Simba SC ili kumnunua mchezaji huyo kwa kuzingatia kipengele hicho kilichopo kwenye mkataba.

Kibu akizungumza na kituo cha Crown fm amemkataa Rashid Yazidi aliyekuwa akifanya interview na media mbalimbali akisema kuwa yeye ni msimamizi wake.

"Rashid sio meneja wangu wala sio chochote, nilimkaribisha nikampa kazi kama mwanasheria ila hakuwa mwanasheria wangu nilimwita ili afanye kazi ila tulimalizana, simdai wala hanidai, simjui"

"Wakala wangu ni Carlos Mastermind"

©️ Kibu Denis Prosper

View attachment 3053076
Streka la bao moja mechi 50 linawapeleka puta makolo.
 
Kutoroka ni kosa linalo angukia katika ukosefu wa nidhamu kwaiyo timu inaweza kumpa adhabu ila si kuzuia yeye kuuzwa nje kwakua ni makubaliano ya ki mkataba.

Hata Simba wakigoma kumruhusu, Tff wata mruhusu kwakua nakala za mikataba wanazo na icho kipengele kita mbeba Kibu.

Ubaya Ubwela.
Kwani wewe umeuona mkataba wake?..........au ndio habari ya kusikia 😀
 
Yanga walikuwa na haki ya kumlilia Feisali maana kiwango kilikuwa kinaonekana ila Simba kumlilia Kibu daaaah ki ukweli ni kujishusha hadhi.
Hata walomchukua sijui waliangalia impact yake kwa msimu 2023/2024 au waliangalia nini.
Sema kila mtu na bahati yake
 
Ukweli upi huo zaidi ya huo kuwa ye ni mchezaji mzuri? Unadhani hiyo team ya Norway ni wakurupukaji kama wewe mpaka wamtumie barua ya mwaliko!? Wenzetu wanafatilia nyendo za mchezaji hata miaka mitatu kabla ya kufanya maamuzi, huo mwaliko wa kutrain na kikosi cha kwanza inakuwa ni hatua ya mwisho kabisa katika kujiridhisha. Anyway, tufanye Kibu siyo mchezaji mzur, tutajie wachezaji wako wazuri then utuambie wanahitajika wapi.
Timu Norway bhana.....ebu tuache 😀 😀
 
Kiwango hichohicho ndo kilifanya mchanganyikiwe na kuweka mezani mamilioni kupata saini yake.
ni kwa kuwa tulipata tetesi kuwa kuna timu inamuhitaji. Hata Jobe tulichelewa kumuaga bure kwa kuwa tulisikia kuna timu zinataka kumnunua
 
Back
Top Bottom