Siku ya jana haikua nzuri kwa
Shilole na Nuh Mziwanda
baada ya kugombana sana hadi
Nuh Mziwanda akaamua
kuchukua vitu vyake na kuhama
Kwa Shilole, Gazeti la
Makorokocho imezipata taarifa hizi
za motomoto kupitia
kwa mtu
aliyekuepo eneo la tukio aliyedai
kuwa yeye alishangaa
kuskia mikikimikiki ndani ya Harrier
na baadae milango ya
gari ikafunguliwa
wakatokeza wasanii wawili wa
bongo flava
ambao ni Shilole na Nuh Mziwanda
na walikua
wakirushiana maneno ghafla
wakatokeza watu
wengine wakiongozwa na Msanii
Chege
Chigunda wakaamulizia ugomvi huo
bila Mafanikio
kwani Nuh Mziwanda alikua
anamuambia Shilole
amrudishie simu yake lakini Shishi
alishindwa kufannya
hivyo kwa madai eti ufunguo upo
nyumbani.
Kweli? wakati
dakika chache zilizopita walikua
ndani ya Gari.
Nilipomtafuta Nuh Mziwanda
hakutaka kubisha na akatiririka
A to Z ya sakata hilo,
Nuh
Mziwanda: Jana Usiku tulialikwa
Chakula Usiku kwa Producer
Dibanjo, mitaa ya
Mango Garden Kinondoni, mimi na
Shilole tulipofika
pale tukamkuta mwenyeji wetu
pamoja na wasanii wengine
Chege, Julio, Dully Sykes na
wengine, ikafika muda nikawa
sijiskii vizuri nikamuomba Shishi
funguo ya gari ili
nikapumzike kwenye gari, kufika
kule nikazikuta simu za
Shilole zikiwa na missed call nyingi
pamoja na msg,
nikazikagua na kukuta msg ya
mwanaume akimwambia
Shilole "Nimeingia Dar" .... ikabidi
nimuite Shilole
na kumkaripia sana Shishi
akajitetea kuwa yule si bwana
wake, Nikamwambia sawa mpigie
niskie maongezi yenu,
lakini Shishi alipompigia sikuelewa
maongezi ndo
nikamzaba kibao cha nguvu na
Shishi akajibu mapigo kwa
kuning'ata mwilini pamoja na
kidole changu
kimevimba mpaka wakati huu, watu
wakajaa eneo la
tukio hadi kina Chege wakafika na
kuanza kuamulizia
kupigana lakini mwisho wa siku
Shilole alikua amenipokonya
simu yangu
nilipomuomba akakataa kuirudisha
na kuondoka eneo la tukio,
Ikabidi na mimi nisepe kwenda
Nyumbani kwa Shilole
ambako nilikua naishi nae ila nia
yangu ilikua ni kwenda
kuchukua vitu vyangu ili
nihame nyumba ile, njiani karibu
nafika nikakutana na vibaka
wakaniibia mpaka viatu,
nikaendelea na safari lakini
nilipofika pale kumbe Shishi
alikua amempigia simu Dada wa
Kazi asinifungulie mlango,
ikabidi nikae hapo nje weeee mida
mida Shilole akafika na
kupitiliza ndani akajifungia mimi
nikiwa nje, asubuhi
wakajisahau na kuacha mlango
wazi ndipo nilipopata
upenyo nikaingia na kuchukua
laptop, guiter pamoja na
nguo vyote vyangu na kumwachia
nyumba yake.