Kwahiyo unataka kusema from 2015 (bila shaka unataka kumaanisha from December 2015) to early 2021, yaani zama za Shujaa... Tanzania hapakuwa na matatizo ya umeme, sio?!
Hivi nyie watu wakati huo mlikuwa mnaishi Tanzania au ndo ile ya kusifia kila kitu?
Hebu tuangalie kwa kwa
haraka haraka tu---
View attachment 2015547
Fuatilia huo uzi uone watu walivyokuwa wanalalamika kuhusu umeme, tena February!!
Nyuzi nyingine....
1.
Kuna mgao wa umeme wa kimya kimya December 05, 2020
2.
Mgao mkali wa umeme Morogoro mjini - December 21, 2020
3.
Wilaya ya Ubungo kuna mgao wa umeme? Mpaka sasa hakuna umeme March 01, 2021
4.
TANESCO tutangazieni kama kuna mgao wa umeme nchini March 04, 2021
Kwahiyo tafuteni wa kuwaeleza hizo porojo zenu kwamba wakati wa JPM hapakuwa na matatizo ya umeme!! Na hapo nimechukua kipindi kifupi tu!!
Tulikuwa tumejipanga kwa lipi?!
Kuanzia 2015 hadi 2021 ni mradi upi mpya wa umeme ulioanzishwa na kuwa operational ukiacha Kinyerezi I and Kinyerezi tu ambayo ilikuwepo kabla ya 2016?
Wewe ndo unatakiwa kunielewa...
Serikali iliingia gharama kubwa kujenga bomba kutoka Mtwara hadi Kinyerezi
Watu ilikuwa tukihoji how come tunakimbilia miradi mingine wakati tulishaingia gharama za kujenga bomba, na gesi tayari ipo... Praise Team wenyewe mnajua mlichokuwa mnafanya!
Mbali na 7.5 Trillion Cubic Feet from Songosongo (2.5 TCF) na Msimbati (5 TCF), kuna zingine almost 50 Trillion Cubic Feet of gas HAZIJAGUSWA...
Sasa huko kujipanga unakosema tulijipanga ni kupi?!
Huko kwa kuanzisha mradi upya wa Bwawa la Nyerere ili uonekane umeweza miradi ambayo wengine walishindwa wakati tayari kuna gas ya Msimbati ilishajengwa bomba, na kazi ambayo ilibaki ni kujenga just power plants?
Angalia ule mradi wa Kinyerezi II ambao JPM alikuta umeshasainiwa, naye akaanza kuujenga tu! By 2015 tayari mradi ulikuwa umeshakamilika! Ulishawahi kujiuliza kama tungeelekeza priority pale Kinyerezi penye Kinyerezi I na II, hivi sasa tungekuwa na Kinyerezi ngapi?!
Angalia hata ile gesi ya deep sea ambayo haijaanza kuchimbwa, na kwavile nawe nimeshawahi kuona ukiandika kuhusu gas though una matatizo ya mahaba... je, ulishajiuliza nguvu ambazo Magu aliziweka kwenye madini ndo ingekuwa ameziweka kwenye gesi, hivi sasa tungekuwa wapi?!
Matokeo yake, tukakimbilia kwenye Bwawa la Nyerere ambalo tunalazimika kuhangaika kutafuta pesa wakati gas industry tayari kuna wenye pesa zao waliokuwa wanasubiria tu green light, shughuli za uchimbaji zianze!!
Matokeo yake, "oh... gesi yote imeuzwa" na Praise Team wanapiga makofi! Fikisheni basi mahakamani hao waliouza hiyo gesi, hakuna hata mmoja aliyefikishwa japo kwa Mjumbe wa Nyumba 10 let alone mahakamani!!
Mkurugenzi wa TPDC, James Mataragio nae akatumbuliwa kwa tuhuma za ufisadi... Praise Team mkapiga makofi!
Baada ya muda, Mataragio akarudishwa kwenye nafasi yake ile ile... tena mkapiga makofi!!
Sasa hao waliouza hiyo gesi ni akina nani?! Cha ajabu, wakati wanadanganya wananchi kwamba gesi yote imeuzwa ili wahalalishe ujenzi wa Bwawa la Nyerere, behind the curtain wanaendelea mazungumzo na kampuni zilizotaka kujenga Kiwanda cha Usindikaji Gesi pale Lindi...
Hapo ndipo mtu unajiuliza, kama gesi yote ilishauzwa, sasa haya mazungumzo ni ya nini tena!!