Mbegu nzuri tayari imekwisha pandwa katika maeneo yote walikokwisha pitia CHADEMA. Kilichobaki ni kumwagilia tu maji ili iweze kuota vizuri na kustawi.
Huko kumwagiliwa na kutunzwa vizuri hakuhitaji tena viongozi wakuu wa chama kufanya mikutano ya majukwaani.
Sasa inabidi wajikite kwenye mikakati ya kuhakikisha mbegu hiyo inasambaza mizizi yake kila mahali.
Ili kuepuka hayo mnayo yaeleza kwenye mada; sasa CHADEMA wabadili mbinu.
NORNOE imekwisha jijengea nguvu yake ya kutosha kuendelea kusambaa kama moto wa nyika. Viongozi sasa wakae na kupanga namna ya kui-'manage'; ili kufikia lengo lake.
Hakuna sababu ya kuwapa mwanya Samia na Genge lake kuivuruga juhudi hii ambayo sasa ipo kwa wananchi wenyewe.
Mkuu , CCM kwa sasa wanaishi katika denial.
Mbinu za enzi za TANU ndio wanaziapply wakifikiri kwamba zitafanya kazi.
Nani alitarajia CHADEMA hii ingekuwepo leo hii kama 2016 -2023 ilizuiwa kufanya mikutano?
Aliyesema angeifuta aliishia kufutika mwenyewe.
March 2020 , katika lindi zito la giza wanamabadiliko waliwachangia hawa hawa CHADEMA milioni 300+ ndani ya saa 24 kulipa faini na kuwaepusha viongozi na kifungo batili.
Lissu kamiminiwa risasi 36 ila bado yupo hai na hakuna kilichomrudisha nyuma kupigania haki.
Japo katika msafara wa mageuzi wasaliti hawakosekani ambao tayari wamejiuza kwa CCM kutengeneza upinzani feki na kuonyesha kuwa 2025 kuna uchaguzi na hadi chopa wamepewa ila bado watanzania wamegoma kununua maigizo hayo .
Watu wasichokijua January 2021 nchi iliingia katika phase mpya kimageuzi ya kutoka kutegemea watu hadi kutegemea wananchi.
Kwa sasa CHADEMA sio ya wanachama ni sauti ya mwisho kwa wapenda mageuzi ambao kwa sasa ni wengi ,kile kizazi cha 1960 na 1970 kinaishia na wao pia wapenda mageuzi wapo .
CCM imebaki kutumia machawa mtandaoni kumuuza mgombea wao asiyeuzika kama uchaguzi huo ulioopuuzwa na wengi maana n8 hadaa ya wazi
Kitendo cha kumkamata Lissu kiliikuza NO REFOMRS NO ELECTION maradufu, hata sasa kuzuia mikutano ndio kutachochea moto.
NO REFORMS NO ELECTION naona ikipaa zaidi kidijitali maana upepo wa dijitali ndio kitu cha mwisho ambacho CCM hawajawahi kukiweza na hawatowahi kuweza kushindana na teknolojia maana mbinu za 1970 wanazo kwenye makabrasha yao ila teknolojia hapa asubuhi ni 1 usiku ukifika ishabadilika kuwa 2 .
Kwani wao si ndio walifungia mtandao wa X kwa Tanzania ,je ukijiuliza hiyo ilipunguza watumiaji na kuzima mijadala ?
Jibu ni la hasha ni kwmaba ndio kwanza mijadala imeongozeka na watu wakiingia kwa kujichagulia VPN na hata wao CCM wanaomsifu mama yao wanaingia na VPN na serikali bado inapost kule na inapata spana za kutosha kama kawaida mpaka wanafunga comment section.
Upepo wa mabadiliko ukifika hauzuiliki ni suala la muda tu.