Yanayoendelea sasa yanakumbusha (1995–2005) kilishuhudia baadhi ya matukio ya kutisha ya kisiasa

Yanayoendelea sasa yanakumbusha (1995–2005) kilishuhudia baadhi ya matukio ya kutisha ya kisiasa

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,749
Reaction score
37,420
Kama mnakumbuka

Kipindi cha utawala wa Rais Benjamin Mkapa (1995–2005) kilishuhudia baadhi ya matukio ya kutisha ya kisiasa na kijamii nchini Tanzania, ikiwemo Zanzibar. Mojawapo ya matukio yaliyotia doa historia ya kisiasa ya Zanzibar ni yale yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2000.

Mauaji ya Januari 2001 – Zanzibar

Baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2000, ambapo chama tawala (CCM) kilitangazwa kushinda visiwani Zanzibar, chama cha upinzani cha CUF (Civic United Front) kililalamikia wizi wa kura na kudai uchaguzi haukuwa huru wala wa haki. CUF walitangaza maandamano ya amani ya nchi nzima kupinga matokeo.
Mnamo Januari 26–27, 2001, maandamano hayo yaliyopewa jina la “Operesheni Dhoruba” yaligeuka kuwa ya machafuko hasa Pemba, ambako jeshi la polisi na vikosi vya usalama walikabiliana kwa nguvu na waandamanaji.

Matokeo ya Machafuko
• Watu takribani 23 waliripotiwa kuuawa, wengi wao wakitokea kisiwani Pemba.
• Mamia walijeruhiwa na wengine wengi kukamatwa au kufungwa.
• Baadhi ya watu walikimbilia nchi jirani kama Kenya, kwa hofu ya kushambuliwa.
• Ripoti mbalimbali za haki za binadamu, kama vile za Human Rights Watch, zilieleza kwamba kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu kupita kiasi na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Ila kumbuka alipopata uraisi alikwenda kwa wajomba zake nao ambao waliondoka kwa mapinduzi tukisema shereee.

Dot to dot hata adolf uwongozi wake ulikuwa na historia ya nyuma kulipa kisasi.
 
GT

Kwa watoto wa juzi huenda hamjui miaka.2000 mwanzoni ilikuwa michungu sana kwa wazanzibar hasa wa CUF na Lipumba wao. Kwa kweli hakuna mateso ambayo Lipumba hakuwahi kuyapata.

CUF walikuwa na kauli mbiu yao ngangali jino kwa jino. In short walikuwa jeuri kwelikweli unaweza sema chadema cha mtoto. Tofauti kwa kipindi kile ilikuwa ni kipigo na kufungwa jela haya ya sasa mauaji na kutekana kwa kweli ni mapya.

Sasa kipindi cha uchaguzi zilikuwa zinapelekwa feed force kutoka.bara kutembeza kichapo balaa
aisee wazenji walipigwa sana enzi hizo.
Haya yanayotokea bara kwa sasa naona kama Samia kaamua kulipiza kisasi zenj kuko shwari wanachapa kazi huku bara vurugu tupu..

Enzi za Mkapa alikuwa anakubalika sana bara huku zenji wakiwa jeuri..kwa sasa Samia Bara ni non Presidential materia na ndo kwenye watu wengi kwa hiyo bila nguvu ya ziada ya vyombo vya dola kutumika hawezi kutoboa.hata kwa nusu kura kila mtu analijua hilo.
 
Mwisho wa yote haya huyu bibi sijui kama ataishi kuandika tawasifu yake.

Mwenzie alikiri lile tukio la 2001 ni doa kubwa kuliko yote katika uongozi wake.

Huyu bibi ana madoa mengi makubwa kuliko ni sawa na madoa ya chui.
 
Mwisho wa yote haya huyu bibi sijui kama ataishi kuandika tawasifu yake.

Mwenzie alikiri lile tukio la 2001 ni doa kubwa kuliko yote katika uongozi wake.

Huyu bibi ana madoa mengi makubwa kuliko ni sawa na madoa ya chui.
Madoa ya chui tunayaita madoadoa![emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom