Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Alafu utasikia ohhh sijui Mo na Bakresa ni vichwa vya biashara,wakati ni wanyonyaji wakubwa.Utajiri wao unatokana na dhuluma na jasho jingi sana la walalahoi.
 
Baada ya kumaliza chuo 2018, nlikua na jamaa angu tumemaliza wote, tukashauriana tutafute vibarua vya kusogeza maisha ,tukaingia keko pale lilipo Go-down la Monalisa,

Adse sio mchezo pale kibarua kwa siku unapewa 4000, hizo kazi zao km una roho ndogo unaweza ukazima

Wana kawaida yao asubuhi kabla hamjaanza kazi mnaenda kupanga mstari
Kiongozi anasema

"Good one Good" wafanyakazi mnaitikia "Good"

Baada ya hapo ni kupigika mpaka jioni
 

mkuu wale wabangladesh pale deira ni hatari sana kwa kushona, yani zaidi ya hatari. Jamaa wanapiga kazi si mchezo.
 
Muhimu tujiulize matajiri wakubwa tanzania wanawalipaje wafanyakazi wao. Kuanzia Dewji, Bakhresa, Rostam, Manji na Marehemu Mzee Mengi. Unataka kuniambia Twiga cement inaingiza hela kuliko Bakhresa ? Cocacola Tanzania inaingiza hela kuliko Dewji ? Hii ni mifano ya makampuni machache ambayo yanalinda haki za mfanyakazi japokuwa hazina mapato makubwa kuliko kampuni za Matajiri wa Tanzania. Wafanyakazi hawathaminiwi kwa sababu matajiri wanawahonga watu wachache ili waishi bila kufuata sheria.
 
Aisee umenikumbusha SBL iliopo nyakato mwanza waliingiza magari mawili yamejaza sukari tukapewa kibarua cha kushusha sukari kwa malipo ya 6000 tu, aisee mimi nilitoka niliwambia siwezi[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] kazi za viwandani.ni.ngumu baraa afu.malipo ni.kiducho yaani toka asbh hadi jioni unashusha makereti ya soda kwa malipo ya 6000 [emoji16]
 
Duh ni noma sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…