Saa 10 Usiku: Zoezi la kuondoa lori lililoparamia watu linaendelea
Your browser is not able to display this video.
Bado vyombo vya uokoaji vinapambana kulinyanyua lori lililoacha barabara na kuparamia abiria na baadhi ya madereva bodaboda katika eneo la Kimara Stop Over jijini Dar Es Salaam.
=====
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni RPC Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kuwa bodaboda sita zimetolewa chini ya lori ambalo liliacha njia na kuparamia abiria na madereva wa bodaboda katika eneo la Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya awali iliyothibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila ilieleza kuwa miili ya watu watatu ilitolewa chini ya lori hilo wakati hadi kufikia saa 9:00 Usiku wakati zoezi la uokoaji likiendelea.
=====
Saa Tisa Usiku: Chalamila athibitisha ajali kutoke, Mili 3 yatolewa
Your browser is not able to display this video.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amethibitisha kuwa miili mitatu imetolewa chini ya lori lililoacha barabara na kuanguka katika eneo la Stop Over Usiku wa kuamkia leo
Zoezi la kuliondoa lori hilo lenye namba za usajili T 908 BYM limeendelea ambapo kwa mujibu wa Chalamila hadi kufika saa 9 Usiku lilinyanyuliwa kwa zaidi ya asilimia 95%.
Pamoja miili hiyo mitatu jumla ya pikipiki Sita zimetolewa baada ya lori hilo kunyanyuliwa kwa asilimia hizo.
=====
Saa saba usiku
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia, baada ya lori kuacha njia na kuparamia waendesha bodaboda eneo la Stop Over, Kimara jijini Dar es Salaam.
Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo iliyotokea usiku wa leo Ijumaa, Februari 14, 2025 wamesema huenda lori hilo limefeli breki.
Hadi muda huu ndo police wamefika wanafanya jitihada za kuokoa baadhi ya boda boda waliofunikwa na gari.
Aidha Polisi wametoka hapa kwenda kwa mchina kuomba gari lije lisaidie kuitoa hii gari maana kuna watu chini
Ukiniuliza malori yanatoka bandarini yanakuja mjini huku kutafuta nn. Ni Ujinga wa CCM huu. Yan lory litoke kurasini lije ubungo then liende chalinze 😂😂 akili za CCM wanazijua wenyewe
Ukiniuliza malori yanatoka bandarini yanakuja mjini huku kutafuta nn. Ni Ujinga wa CCM huu. Yan lory litoke kurasini lije ubungo then liende chalinze 😂😂 akili za CCM wanazijua wenyewe
Hakika mkuu,pale kwa msuguri round about kama unatokea bochi hospital kona ya kuingilia mbezi,bajaj na boda boda zimegeuza kituo,na wamachinga wameanza kuweka meza zao barabarani kabisa,so ukiwa unatokea bochi kuingia moro road inabidi utoke nje ya barabara kuwakwepa wao,siku ikitokea ajali pale mamlaka ndio zitashtuka
hatari tupu. naishi pale, huwa nasema kila siku kuwa mbio hizi za magari , pikipiki , mabasi etc kuna siku zitaleta maafa! spidi huwa ni kubwa mno mpaka unashangaa kuwa huyu si amefika spidi za hivi za nini?