Waafrika wengi wanakufa sana kutokana na uzembe, ujinga na upumbavu.
Kwenye barabara za Afrika kuna makosa mengi sana ambayo watu wanaya fanya na wanayachukulia poa, Halafu ajali ikishatokea ndio wanakurupuka huko kuchukua hatua.
Mfano ni kawaida kukuta mtu anatembeza biashara yake kwenye barabara. Unakuta mama na beseni lake anatembeza matunda kwenye barabara. Halafu wanaachwa tu.
Kwenye hii barabara ya Mandela kwanzia hapa Buguruni Bakhressa. Wafanyabishara wanauza biashara zao barabarani kabisa. Malori, daladala, treni, pikipiki, bajaji vyote humohumo.