Yanayojiri ajali ya Lori Stop Over-Kimara: Miili 3 na bodaboda 6 zatolewa, zoezi la kuondoa lori linaendelea

Nasema kila siku humu,madereva wapumbavu wengi sana. Wanaendesha kama mbuzi tu hawafuati utaratibu hata wa kusubiri taa.
Waafrika hasa watanzania hakuna wanacho tii barabarani.

Mijitu inajiendea tu pakachu pakachu kama mapanya.
 
Poleni Sana wana kimara-stopOver,
Hapo jirani Kimara Suka ndo home nilikokulia mpk Nmefika kutoka home kwenda kujitegemea😢

maisha ya mwanadamu huwa ni kitu kidogo sana, sometimes!

Ee Mwenyezi Mungu tunaomba utujalie mwisho mwema!
 
Hivi hakuna uwezekano wa kuchonga barabata ipite huko pugu pembezon mwa reli ikatokee morogoro huko...ili malori yawe yanapita huko jamano...
Upo sana pugu hadi mlandizi huko juu kwa juu
 
hatari tupu. naishi pale, huwa nasema kila siku kuwa mbio hizi za magari , pikipiki , mabasi etc kuna siku zitaleta maafa! spidi huwa ni kubwa mno mpaka unashangaa kuwa huyu si amefika spidi za hivi za nini?
Baadhi ya madereva vichwa ngumu.
 
Ukiniuliza malori yanatoka bandarini yanakuja mjini huku kutafuta nn. Ni Ujinga wa CCM huu. Yan lory litoke kurasini lije ubungo then liende chalinze 😂😂 akili za CCM wanazijua wenyewe
Sasa mkuu yangepita njia gani? Sema mkombozi atakuwa sgr kile kituo cha Kwala kikikamilika! Kwa sasa hivi hakuna mbadala!
 
Hii ajali inasemekana wamekufa watu 17 lakini habari zinaripoti watatu something doesn't add up.
 
Kuna siku nilikuwa hapo ubungo Riverside.

Lori lika angusha kontena, Bahati nzuri kontena hilo lilianguka chini kwenye ule uwazi unaotenganisha barabara mbili.

La sivyo lingeanguka upande wa pili, lingeponda magari na kuua watu.
Hii kama ni mwakajana naikumbuka hii
 
Lori lina breki tatu

Engine Brake
Air Brake
Spring Break

Zinafelije zote ?
Mosi Engine brake sio practical at high speed,
Spring brake ni redundancy system kwenye air brake na inatumia same component za air brake, kwa hiyo kama ni kifaa chenyewe kimefeli (brake chamber drum, disc etc) spring brake na air brake haiwezi kufanya kazi n zitafeli kwa pamoja
Engine brake na air brake zote zinategemea air pressure, kama gari lililkuwa na shida ya ait pressure basi engine brake na air brake zote zinafeli kwa pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…