Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Ni Pandu huyuhuyu aliesimamia yale mabadiliko maarufu ya Katiba ya Zanzibar ambayo kwa kiasi kikubwa ndio yaliyochagiza mchakato huu wa sasa wa KATIBA mpya. Sifa mnazompa Pandu huyu wala hazimstahili. Keshakuwa "senile".

Saa hii wamerudi tena wanajidai kuelewana.
 
Huyu mwenyekiti Pandu ni mtu muungwana sana tena sana. Tatizo anaongoza watu ambao hawana maadili na wengi wao hawajui ni kwa nini wakobpalr mjengoni. Bila shaka Sam Six atawaweza. Myu unaweza kudhani kuwa wengi wao hawajawahi kuona mlango wa darasa. Wengine wanafanya upuzi ili waonekane kwenye TV pasipokujua wanakera huku tukikumbuka kwa usanii wanaofanya wanalipwanlaki 3. Hovyo kabisa.
 
Wadau, katika hali inayotoa muelekeo mzuri, mvutano uliojitokeza leo asubuhi baina ya Christopher Ole Sendeka, Mbunge wa Simanjiro na Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Hamisi Bakari, umemalizika kwa wawili hao kupatana na kuzika tofauti zao. Pongezi ziende kwa waliosuluhisha mgogoro huo wakiwemo James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI, Prof Mark Mwandosya na wengineo.
 
Hivi rais hawezi kutengua ujumbe wa hawa wajumbe wa bunge la katiba?
 
Mchakato wa KWANZA kule Kenya ulishindwa kwenye hatua ya kura za wananchi. Huu wetu unaishia humu Bungeni.
 
Wehu wanatupotezea muda , Sendeka hana ufahamu / weledi kuhusu masuala ya sheria yeye hatumii busara ila nguvu........ndio CCM hao..
 
Wait a minute Chabruma
Kwani was this a mano-a-mano issue? was it drawn to personal level carrying grudges and blames?

I thought pipo were talking and discussing about kanuni, sasa hili la kuelewana na kuzika tofauti latoka wapi?

kama wana ugomvi binafsi sawa lkn kama ni kutofautiana kwa hoja sioni mantiki ya kusema wamepatana
 
Last edited by a moderator:
Kwani waligombana au kupigana?
 
Wadau hii thread ni maalum kwa ajili ya updates za bunge la jioni tar 6.3.14!

Plz mods msiunganishe na thread zingine!
 
Ni maneno ya Prof huyu, ameyatoa ndani ya bunge sasa akiasa juu ya vurugu zilizotokea leo bungeni.

Ni maneno makini yenye ustarabu, yaliozamilia kutoaa wingu la kutokuelewana kwa wajumbe

Asante Prof Mwandosya.
 
Bunge maalumu la katiba limeanza vizuri Jioni hii,..
 

Kulitokea nini mkuu, tujuze wengine tuko mbali na TV..

Kwani waligombana au kupigana?

Kama mtakumbuka vizuri, katika semina ya leo asubuhi, kulitokea tofauti baina ya Sendeka na Abubakar Hamisi Bakari. Tofauti ilitokana na Mwenyekiti kuwaruhusu Sendeka na Ummy Mwalimu kuchangia kanuni ya 58 ya Rasimu ya Kanuni za Bunge maalum. Wakati mwenyekiti Kificho akiwa anasoma majina ya akina Sendeka, alisimama Abubakar na kusema kuwa majina yanayosomwa hayamo kwenye jedwali la marekebisho walilonalo. Kutokana na hali hiyo alisema kuwa mwenyekiti atasababisha bunge hilo likae kwa zaidi ya kiezi sita. Baada ya hapo. Alisimama Ole Sendeka na kumshutumu Abubakar kuwa anafanya kazi kwa maslahi ya CUF na kwamba hana uzoefu na kanuni. Kutokana na maneno hayo, Abubakar alikuja juu na kusema kuwa ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 tofauti na Ole Sendeka ambaye ametoka Simanjiro na ana umri wa miaka 10 tu hivyo hawezi kumbabaisha. Baada ya maneno hayo ndipo mvutano ulipojitokeza na badala ya kuwa mgogoro wa watu wawili, ukageuka kuwa mgogoro wa wengi na ulionekana ni ama baina ya CCM na CUF au baina ya Watanzania Bara na Wazanzibari
 
Ameanza kuonge james mbatia ameongelea yule prof mmoja hv wa ufaransa aliefanya research ktk utungwaji wa katiba. Mwenyekiti wa bunge anapigia chapuo hayo maandiko ya prof kwamba km vp wajumbe wapatiwe nakala
 
Maneno gani wengine hatujajua nini kimetokea
Nalog off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…