Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wabunge wamekuwa kila mara wanapewa muda wa kupumzika ili wasome makabrasha wayaelewe yaliyomo. Ajabu kumbe hata hawasomi. Katika bunge hili tutajionea mengi. Haleluya!
Mama Mdogo tumeshajionea tayari ni majanga matupuWabunge wamekuwa kila mara wanapewa muda wa kupumzika ili wasome makabrasha wayaelewe yaliyomo. Ajabu kumbe hata hawasomi. Katika bunge hili tutajionea mengi. Haleluya!
Wabunge wamekuwa kila mara wanapewa muda wa kupumzika ili wasome makabrasha wayaelewe yaliyomo. Ajabu kumbe hata hawasomi. Katika bunge hili tutajionea mengi. Haleluya!
Pale aliposema kuusu kanuni ya mjumbe atakapofariki gharama anabeba nani..?
Kumbe kuna kanuni inasema kabisa kua bunge ndo litabeba gharama zote
Tundu lisu akamuumbua akasema mh mwenyekiti tumebewa vitabu ivi ili tuvisome na akamsomea sheria inasema vipi kuusu ilo swala
Kweli mkuu. Hakuna kitu muhimu zaidi ya maoni ya wenye nchi.Kiboko ya wote ni Livingstone Lusinde, yeye anasema Tanganyika ndio nini maana ilikuwepo yeye hajazaliwa. Na kama Nyerere aliikataa basi wao ndio Nyerere wa kizazi hiki. Yaani ni aibu "kiazi" kama kile eti kipo kututengenezea katiba.
Sent from my iPad using JamiiForums
Leo mtoto hatumwi dukani.Leo, asiye na mwana aeleke jiwe.Leo,ukigeuka nyuma unakuwa jiwe la chumvi.Leo,macho mbele kama tochi. Leo,masikio na macho ni marafiki muhimu. Leo, kila kitu kina watu;wale wastaarabu na fyatu.Usisubiri kusimuliwa.Jionee au sikiliza mwenyewe leo.
Kwa nyaraka zilizopo,shughuli hiyo itakuwa jioni.Leo,Bunge la Katiba linafikia vifungu vya 37,38 na 39 vya Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo ili kuvipitisha.Vifungu tajwa,pamoja na mambo mengine, vinazungumzia namna ya upigaji kura wa kupitisha Rasimu ya Katiba utakavyokuwa ndani ya Bunge hilo.Wapo wa KURA YA SIRI na KURA YA WAZI/DHAHIRI. Leo watajulikana vyema.
Lazima leo Bunge liamue kupitisha au kuviondosha vipengele hivyo vya Kanuni. Ni leo.Si kesho. Lakini, kupitisha SIRI au DHAHIRI kutafanywa kwa SIRI au DHAHIRI? Mwenyekiti wa muda ataongozwa na Kanuni au Taratibu zipi leo kuamua kuendesha kura za SIRI au DHAHIRI wakati itakapojitokeza haja ya kufanya hivyo? Leo kitaeleweka tu.Zege halilali!
KAZI IPO