Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Tupeni updates wadau..

Wanajadili suala la vazi rasmi kufaa kuvaliwa ndani ya bunge.

Inaonekana kwa upande wa wanaume vazi la suti ndiyo lipo katika mjadala zaidi.

Mh. Sarungi anaomba utamaduni uzingatiwe akipinga si lazima shati na tai.....

Mh. Simbachawene ametoa ufafanuzi na kanuni imepita kwa mavazi yaliyo ainishwa. Suti ikichukua nafasi kubwa zaidi.
 
Baadhi ya wachangiaji wametaka kabla ya bunge hilo kuanza na kumaliza basi iwe kwa dua ili wale wenye mashetani akina Olesendeka mashetani hayo yaweze kuondoka vichwani mwao., waislam na wakiristo wataomba kwa dini zao. TBc Live
Umefanya quotation ya wapi ambapo wamesema Olesendeka Ana mashetani? Please. Kuwa na staha Kwa watu.
 
Kitendo cha kupitisha kanuni ya kuzuia mwandishi wa habari atakae andika habari ambazo si sahii kwa mwono wenu(wajumbe wa bunge la katiba) ni kujiwekea madaraka yasiyo yenu.
Tasinia ya habari inayomamlaka yake inayoweza fanya kazi hiyo, halikadhalika kama kutakuwa na kitu kikubwa cha kuwakwaza sana serikali kupitia mamlaka husika wataona nini cha kufanya. Napenda kuwakumbusha kazi yenu si kuwafatilia watu watakao wakosoeni au kueleza muono wao juu ya kazi zenu. ikumbukwe Bunge la katiba si muhimili hapa nchini hivyo liheshimu mihimili iliyopo hivyo si busara kujiwekea madaraka ambayo halina, kama kuna ambaye atawakwaza pelekeni taarifa mamlaka husika.
Tafadhalini! heshimuni kazi tuliyo wapa na tuna uhuru wa kupata taarifa yeyote ya yanayojiri humo ndani ili mwisho wa kazi yenu tukubali au tukatae kama wananchi.
SISI WANANCHI NDO WENYE MAAMUZI YA MWISHO SI NYINYI MSIJISAHAU.
Majukumu mema ya kuleta katiba bora.
 
Baadhi ya wachangiaji wametaka kabla ya bunge hilo kuanza na kumaliza basi iwe kwa dua ili wale wenye mashetani akina Olesendeka mashetani hayo yaweze kuondoka vichwani mwao., waislam na wakiristo wataomba kwa dini zao. TBc Live
Mkuu hayo maombi yatahusu na wale wenye matatizo ya akili kama fulani?
 
Kwa nini mkuu unatetea mwandishi kuandika habari zilizopotoshwa halafu unafurahia na kushangilia uko sawa kweli mkuu.
 
Mnyika kachangia kuhusu mavazi rasmi kachangia vazi la kitenge liongezwe mwenyekiti wa kamati ya kanunii kamkubalia. duuu bi kiroboto kaibuka anachangia anamkrash mnyika kwamba mavazi ya vitenge yasiruhusiwe kachangia pumba infact bi kiroboto yuko shallow.

kuna jamaa kakrash skafu kamtolea mfano. savimbi wa bongo. Mmoja kaibuka na vazi la kimasai nalo vipi liruhusiwe? Bi. sarungi kaja na mambo ya urembo wa asili nazani anamaanisha aruhusiwe kuvaa culture zake. Yaani kuna vituko kidogo.

Nassari kaongelea kwamba unadhifu ni kuvaa kimagharubi vazi la kitenge lisiruhusiwe labda huko kwenye kamati.
 
Jamani eti sasa wanapoteza muda eti wanagombea mavazi. Ili iwe nini kwa watanzania wanaotaka Katiba nzuri. Mkivaa suti ndio mtaongeza kufikiri! Hopeless!
 
Sijui kwa nini umeshindwa kuwakanya na kuwashauri wanahabari wasiandike habari zilizopotoshwa ili kuepuka kuwapotosha watanzania badala yake unashabikia sijui kama unajua madhara ya habari iliyopotoshwa.
 
Kwa nini mkuu unatetea mwandishi kuandika habari zilizopotoshwa halafu unafurahia na kushangilia uko sawa kweli mkuu.
kupotoshwa kwa habari mpaka ionekane na ijadiliwe athari zake na mamlaka husika, tusipokuwa makini tunaweza kubana uhuru wa waandishi wa habari.
Pili ni busara hakimu awe mtu mwingine na si yule mlalamikaji ili kupata usawa
 
Kulikuwa na mjadala mkali Bungeni kuhusiana na aina ya mavazi wanayopaswa kuvaa wajumbe. Kwa upande wa akina mama hakukuwa na mjadala na kwa maana hiyo watakuwa huru kuvaa wapendavyo. Hata hivyo akina mama wakiongozwa Mh. Makinda wameamua wanaume wavae suti na hoja imepita kwa akina baba kulazimishwa kuvaa suti. Mchelea mwana kulia, hulia yeye!
 
wadau naandika kwa masikitiko na machungu sana ....leo kwenye semina ya bunge la katiba kuna limama limewasha mike na kusema tuahirishe kikao hyo ilikua asubuhi..yani wanafurahia kuvuta siku mbele waendelee kufuja kodi zetu wameona posho haiongezwi sasa wana prolong mda ili cku ziwe nying ...hili bunge lisije kutuingiza kwenye vita na ww mamb unayeropoka vita vikija nyie ndio wa kwanza mnathirika...hvi kweli nyerere angekuwepo angeruhusu watu walipwe laki 3 kwa cku huku shule hazina vitabu,walimu na hospitali hakuna dawa wala vitanda...
 
Kwa hiyo unataka wabunge wavae kama wako sokoni? WAVAE SMATI!
 
Sasa wakimchagua mchungaji akaanza kutoa mapepo patakalika kweli!!
 
ujue. matoto ya njiwa hajawahi kuwa na mume ndio maana anakadharau flani hivi kwa wanaume.
asamehewe
 
sijui wanadhani pale ni katika posa.....hii ndio shida ya wabunge wenye fikra za kimalaya za CCM..hata waliolewa nao wandhani kazi ni kupangia wanaume wasio waume zao mavazi ili wawakubali
 
Back
Top Bottom