Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Kuna wajumbe kila saa lazima waongee.......OLE SENDEKA na yule OLUOCH sijui.......mpaka inaudhi wengine wankaa tu hata sijui kwa nini tumejaza watu mle!

 
Kwa wale marafiki wa Zitto nawaomba sana kama kweli huyu ni rafiki yenu lazima mfanye maamuzi magumu ya kumpeleka kwenye hospitali kwa ajili ya kuangalia akili zake;Huwenda ni mgonjwa wa akili
 
Lazima awanyooshe pandu ni mumini wa serekali 3 ila sifa atuwezi kumwagia nyingi kwa sasa maana hamna kanuni mpaka sasa,matumizi ya kanuni yatatusaidia kujuwa m/kiti ni mbabe au anabusara au anapendelea upande fulani
 
duh hii katiba itapatika bila watu kung'olewa meno kweli hii sidhani...ndio maana mwalimu alikuwa anapitisha sheria zake mwenyewe mwenyewe hakutaka malumbano
 
Zitto ni mpuuzi sana anapenda kubebesha wenzake lawama.

Kukimbia tatizo siyo solution, na mtu anayekimbia matatizo hafai kuwa kiongozi.

Kwa kuwa yeye ni sehemu ya wajumbe alitakiwa aungane na wenzake kutafuta solution.
 
Hili bunge naona liko kama halina utaratibu hata wa kusikilizana na kila mtu anakuja na hoja hafifuhafifu na nawasiwasi na kama kuna katiba ya maana hapa. Litakapokuja suala la vipengele vya udini hapo kuna jambo lisilo la kawaida litatokea yetu macho!!

Ni kweli halina utaratibu na wanachofanya sasa ni kuandaa huo utaratibu yaani Kanuni za kuliongoza. Hopefully, kwa kukosekana utaratibu ndio mapuuzi mengine ynataumia mwanya huo kujianika jinsi yalivyo. Linategemea zaidi busara za Mwenyekiti.
 
Habari za jion wa JF.
Leo nataka kuwauliza hao Wabunge wetu maana siwaelewi, ivi kabla hajaingia Bungeni kwanza wanapita baa kuonja au kutoa aibu au ndio wanataka siku ziishe ili waombe tena muda ili waendelee kula kodi za wananchi?

Km wapo naomba majibu.

Nawasilisha
 
Nimepigiwa simu kwamba Kikao cha asubuhi kimekwisha kwa mabadilishano ya lugha mbaya kati ya Mwansheria mkuu wa Z´bar (ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kanuni), Mwenyekiti na Ole Sendeka. Mwanzo ulikuwa ni Mwanasheria mkuu kumwambia wazi mwenyekiti kwamba anavuruga kikao. Sikusikia vizuri Sendeka aliingiaje ingawa aliingilia kati kumukingia kifua Mwenyekiti baadaye Hii zain yangu kama kawaida imevuruga mawasiliano kabla sijaunganisha matukio.

Hebu tusaidiane kufahamu yaliyofuata maana hawa jamaa ndo wanadai kufukuza waandishi ili uchafu huu tusiusikie.
 
nilisikiliza vizuri sana yaliyozumgumzwa kupitia redio ya kwenye simu yangu.

Nilichogundua ni kuwa baadhi ya wajumbe wanajiona wao ni bora na wenye
akili sana kuliko wengine na mbaya zaidi wanawashambulia wenzao
bila hata kuona aibu kwa wenzao ili waonekane wanasimamia misingi ya
makundi yao.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa na ile hali ya kujivika ujuaji wa sheria
kuliko hata wanasheria wenyewe na pale wanapoelezwa ukweli
kwao inakuwa nongwa.

Ndugu zangu wajumbe,badilikeni kifikra na kuondoa ile dhana ya mimi/sisi
ni zaid ya wengine kwani kuchangia sana kwenye kanuni si kigezo cha
kufanikisha kile mnacho kusudia kiwe sana sana mtajichosha bure mapema
na pengine kudhalaulika kabisa ndani na nje ya bunge.

Kumbukukeni kuwa mmekwenda Dodoma kufanya kazi hiyo kama timu
(team work assignment) na si vinginevyo vinginevyo mtaonekana ni wahujumu
uchumi kwa mwanvuli wa kutunga katiba.

Jamani ebu badilikeni na muwe ni wajumbe wenye nidhamu,uadilifu,uhaminifu,
hekima na busara na pale mnaposhindwa kutuliza jazba zenu ni bora mkawaona
viongozi wa imani zenu waliopo hapo hapo.
 
Ndugu zangu,
Watanzania leo tunavuta pumzi huku tukielekeza
macho na masikio yetu katikati kabisa ya nchi
yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda. Ni Dodoma.
Huko itapatikana leo hatma ya mwelekeo wa
mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya
Nchi Yetu.
Hata hivyo, kuna ishara mbaya kuwa
tuliowatuma Dodoma wako katika hatari ya
kukwamisha mchakato mzima kwa kujikita
kwenye kupigania kisicho na maslahi ya nchi hii
kwa miaka 50 au 100 ijayo.

Watapigania yaliyomo kwenye vifungu vya 36
mpaka 37 za Kanuni za kuendesha Bunge hilo
Maalum. Inahusu namna watakavyofikia
maamuzi, kuwa iwe ni kwa kura za faragha au
dhahiri. Ndio, inahusu kura za siri au kura za
wazi. Ni' vifungu vya kifo' maana ndivyo
vitakavyoamua, kwa namna moja au nyingine,
uhai wa mchakato mzima wa kuitafuta Katiba.
Tuliowatuma Dodoma wamejigawa katika
makundi ya ' Sisi' na ' Wao'. Wanatafuta
kushindana na kupata mshindi badala ya kutafuta
muafaka wa Kitaifa. Na hakika, kama alivyopata
kusema Rais wa Nchi, Jakaya Kikwete, kuwa
kwenye kushindana huko hakuna atakayeshinda.
Tutashindwa Sote. Na huo ndio UKWELI.
Hakika, huu ni mtihani mgumu ulio mbele yao
tuliowatuma Dodoma. Wakishindwa mtihani huu,
basi, ishara zinazoonekana ni za mkwamo wa
jumla wa mchakato mzima. NI AIBU.
Tuliowatuma Dodoma hawajachelewa kuitafuta
hekima na busara kutunusuru na aibu kubwa ya
taifa iliyo mbele yetu. Tuliowatuma Dodoma
wawafikirie pia watoto wa kesho na wa vizazi
vijavyo katika nchi yetu tuliyozaliwa na
tunayoipenda.
Na ushauri hapa ni heri kukubaliana
kutokubaliana, na hivyo, kusitisha kwa muda
mchakato huo, kuliko kulazimisha kwenda
mbele. Ni ushauri pia, kuwa ni heri kuyatafuta
maridhiano kwanza kabla ya kuingia kwenye
majadiliano, kuliko kuyatafuta maridhiano baada
ya kuingia kwenye mapigano na kujeruhiana. Ni
busara basi, tuliowatuma Dodoma wakaunda
Kamati Maalum ya kuyatafuta maridhiano wa
vifungu hivyo. Na ifahamike, kuwa MARIDHIANO
ndio msingi wa UHALALI wa mchakato na hata
Katiba yenyewe.
Tusipotanguliza busara, hekima na maslahi ya
taifa, yumkini yaweza ikawa kama yale aliyopata
kuyasema miaka 60 iliyopita, mwandishi yule
mahiri, Mtanzania mwenzetu Shaaban Robert,
aliandika; " Wasadikika wana desturi ya kutafuta
fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha
umwa na nyoka wa matendo yetu mabaya ya
zamani.
Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani
kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia
katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema
ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta
kifo.
Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu.
Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea
faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote."-
Shaaban Bin Robert.

kwenye red hapo, naomba utambue kuwa hakuna mjumbe hata mmoja uliyemtuma dodoma kukuandikia katiba. Wote wamejitungia sheria ya kuwa wajumbe, na wengine wamepelekwa na raisi. Husipotoke na wala husipotoshe jamii.
 
Zitto anashauri nini kifanyike sasa?ama inatosha tu kuwaita waliomo wapuuzi ambao ndio wanamwandalia kanuni yeye asiye mpuuzi aje kuzitumia?!!Huu si ustaarabu(us.he.nzi) kwa mtu kama yeye

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mkuu Pasco Mh. Pandu angekuwa na kanuni hata moja nadhani angekwambia huna haja ya kututajia idadi ya TV. Just be straight to the point. Ni Kiongozi mwenye weredi kusema kweli.
 
Last edited by a moderator:
Ni sawa na baba anayeamua kula hotelini kwa sababu nyumbani kwake jiko limeharibika! Kwa nini asipeleke hizo 'busara' zake bungeni ili upuuzi usipate nafasi?
Kweli hata mimi nimeshangaa sana,

Nasikia hayuko bungeni wakati huo huo analaumu wanaomtengenezea kanuni,

anataka wamsafishie njia ili yeye apite bila kuchomwa miba i mean boss akute kanuni tayari.
 
Kama Ccm haotatoka Madarakani hata hiyo katiba mpya ni kazi bure…
 
Kosa lililofanyika kuanzia mwanzo ilikuwa ni kuacha wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania kuwa wajumbe wa Bunge maalum la katiba of which tunaona kila kitu sasa kinatanguliwa na maslahi ya siasa kwanza....its a total drama na bado picha inaendelea ndo kwanza hata robo hatujafika!
 
Kuna wajumbe kila saa lazima waongee.......OLE SENDEKA na yule OLUOCH sijui.......mpaka inaudhi wengine wankaa tu hata sijui kwa nini tumejaza watu mle!


Mkuu afadhali oluoch anajenga hoja za maana sendeka yeye kazi yake ni kuropoka tu!na kujenga mazingira ya katiba ya ccm sio ya wananchi akiyamungu huu mchakato hautofikia malengo kama tutakuwa na sendeka 10 tu!
 
Habari za mchana wanajf
Leo nataka kuwauliza Wabunge wetu. Ivi kabla ya kuingia Bungeni wanapitia baa au ndio wanataka muda uishe waombe muda mwingine ili waendele kula kodi za wananchi? Siwaelewi! Bungeni kumekua km sokon!

Km wapo tunaomba majibu

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom