Chizi Fureshi
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 1,718
- 461
Last edited by a moderator:
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tanzania eeeee
Ok pia nawe wasilisha rambirambi za marehemu Mwangosi kwa mjane.
Ni neno la leo tu kaka
Hahahahahahahahaaaaaaaaaa...........!!!!Jana bunge liliahirishwa kwakuwa wabunge walidai wamechelewa kupewa nakala ya sheria namba 32 hadi 43. Leo bunge limeahirishwa kwa sababu secretariet imetoa majedwali mawili ambapo jedwali moja halionyeshi majina ya akina Mwalimu na Sendeka.
Kwa vyovyote vile wazembe wanajulikana na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yao.
Kama mwendo huu utaendelea kila siku bunge litakuwa linaahirishwa huku posho zetu waamka taabani zikiendelea kuliwa.
Ushauri wa bure kwa kamati ya kanuni, waandae sheria ya mpito kwamba hapo bungeni yeyote atakaeonekana kuanzisha vurugu asilipwe posho. Na kwa njaa walizonazo hao watu utaona kama watafanya tena fujo.
Kuna tabia nyingine imezuka ya watu kupiga tu kelele za kuzomea hata kama jambo linaweza kuzungumzika na majadiliano yakaendelea. Hili mimi naona linasababishwa na baadhi ya wabunge wanaotaka bunge kiahirishwe ili wakafanye starehe zao. Dawa ya hawa watu ni kuwawekea monitor atakaeandika majina ya wapiga kelele ili yanapotokea mazingira ya hivyo, majina yanasomwa then kama kawaida wanakatwa posho.
Haya yasipofanyika, hakuna rasimu wala katiba mpya hapo mjengoni. Tutarudi mwaka 77 kuendelea na zilipendwa. Kikwete alisema 'mkileta utoto hatutapata katiba mpya. Na kwa vile nchi haiwezi kuendeshwa bila katiba tutarudi kwenye katiba ya zamani'
Dawa ya hawa watu ni kuwawekea monitor atakaeandika majina ya wapiga kelele ili yanapotokea mazingira ya hivyo, majina yanasomwa then kama kawaida wanakatwa posho.
wewe umekata tamaa, kwa hiyo unataka kutuvunja moyo watanzania wote, kaa kimya, hujui kitu.Ukiondoa unafiki wa kawaida wa kibinadamu, kila mtanzania angependa aipate hiyo nafasi ya kuwa mjengoni kwa sasa. Kitu ambacho kingetofautisha ni dhamira, nia ya dhati na mchango wa mtu akiwa pale. Hapo ndo ningetofautiana na wengine. Ningehudhuria vikao vyote hata kama ni usiku wa manane, ningesaini fomu yoyote ya posho inayokatiza kwangu, kura yoyote ya siri nisingeshiriki, na mwisho ningekaa kimya vikao vyote huku nikivuta mkwanja tu. Sababu yake ni kwamba hao wote walioko hapo bungeni ni porojo tu, katiba itatoka kama ambavyo 'wenye mamlaka' watataka iwe. Kinachofanyika hapo ni ulaji na kupotezeana mda.
Hapo penye Red Mkuu naomba nikusahihishe.
1. CV za Mtu ni Cv ya Mtu
2. Kutuonyesha badala ya Kutuonesha
3. Anaejua badala ya Anayejua
4. Anae badala ya neno anaye
Rudi Darasani Mkuu una kiswahili kibovu kama Cha Masai wa Longido
Ukiondoa unafiki wa kawaida wa kibinadamu, kila mtanzania angependa aipate hiyo nafasi ya kuwa mjengoni kwa sasa. Kitu ambacho kingetofautisha ni dhamira, nia ya dhati na mchango wa mtu akiwa pale. Hapo ndo ningetofautiana na wengine. Ningehudhuria vikao vyote hata kama ni usiku wa manane, ningesaini fomu yoyote ya posho inayokatiza kwangu, kura yoyote ya siri nisingeshiriki, na mwisho ningekaa kimya vikao vyote huku nikivuta mkwanja tu. Sababu yake ni kwamba hao wote walioko hapo bungeni ni porojo tu, katiba itatoka kama ambavyo 'wenye mamlaka' watataka iwe. Kinachofanyika hapo ni ulaji na kupotezeana mda.
Mtikila alisema mapema. Bunge la kihuni.