Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,780
Wadau, leo tutaendelea kuwaletea kila kinachojiri kwenye semina ya Bunge Maalum hapa Dodoma. Kazi kubwa itakayofanyika leo ni kupitisha vile vifungu vilivyoachwa kiporo kwa siku ya juzi. Vifungu hivyo ni kuanzia kifungu cha 32 hadi 43 ambavyo vilifanyiwa ukarabati mkubwa. Wabunge wamepewa muda wa kupitia vifungu hivyo na kuwasilisha majedwali ya marekebisho yao kwa Kamati Teule. Kwa siku ya jana, zoezi la kupitisha kanuni lilienda vizuri hasa wakati wa jioni kwani wabunge walipitiaha vifungu kuanzia cha 58 hadi kifungu cha mwisho cha 87. Hakukuwa na mivutano mikali kama ilivyojitokeza kwenye kikao cha jana asubuhi.
Mara baada ya vifungu vyote kupitishwa, zoezi litakalofuata ni uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambapo hapa pia inatarajiwa kuwa zoezi litakuwa jepesi hasa kutokana na kudhihiri kuwa SAMUEL SITTA ni kama amepita kutokana na kukubalika miongoni wa makundi yote matatu yanayounda Bunge hilo. Uchaguzi wa Mwenyekiti unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi tarehe 8.3.2014
Kwa vile nitakuwa mjengoni, nitawajuza kila kitu kitakachoendelea. Mimi na Simiyu Yetu tunawaakilisha vema na hakika mnapata taarifa sahihi na kwa wakati.
View attachment 143283
View attachment 143284
View attachment 143285