Yanayojiri Bunge Maalum la Katiba leo Tarehe 7.3.2014.

Yanayojiri Bunge Maalum la Katiba leo Tarehe 7.3.2014.

Msingi wetu ni kuwapa ukweli wa mambo bila ushabiki hii ni kwa manufaa ya watanzania waliowengi ambao ndiyo wenye katiba yao.
Kimsingi ccm imedhamiria kuharibu mchakato wa katiba mpya kwa mimi bila kuiona mfumo wa muungano unabadilika itakua ni kupoteza wakati .serikali 1 au 3.Muundo wa serikali 2 umeshindikana
 
Kimsingi ccm imedhamiria kuharibu mchakato wa katiba mpya kwa mimi bila kuiona mfumo wa muungano unabadilika itakua ni kupoteza wakati .serikali 1 au 3.Muundo wa serikali 2 umeshindikana

huu muungano sijui una ajenda gani ya siri !nahisi kuna peoples zinapiga hela kwenye hili koti la muungano!!!!!
 
Taswira ya Ukumbi wa Bunge Robo saa kabla ya kuanza kwa semina
image.jpgimage.jpg
 
Ila ushabiki wenu wa kipuuzi muache kama mmeamua kuripoti kwa ajili ya wote iwe hivyo, sawa?
 
Taswira ya ukumbi wa Bunge saa nne kamili asubuhi
image.jpg
 
Ndugu wana jamvi mwenye macho haambiwi tazama kwa ninavyoona mimi kinachoendelea bunge la katiba ikweli ni kwamba ccm haikuwa radhi tanzania kupata katiba iliyo bora na yenye maslahi ya taifa. Kwa nini nasema hivyo bila kukosea palishaundwa tume za katiba kama tatu kukusanya maoni ya wananchi na shauku ya wananchi ni kutaka serikali 3 angalao kuweza kupata kile walichokosa miaka 50 swali linakuja ninani anawapa hiyo nguvu ya kukinzana na matakwa na wananchi walio wengi ambao ndio wamewatuma kuikamilisha baada ya kutoa maoni yao ? Kwa nini hawataki kura ya siri ambayo itamfanya mtu kuwa huru kiakili kimsingi ccm kuna mchezo wanatuchezea sisi wananchi na hatutakubali watu kujiona miungu watu kuanza kutuchagulia kile tusichokitaka sisi wananchi sisi tumewatuma ninyi wabunge na taasisi nyingine kwenda kuitimiliza katiba nzuri sio kuitengua .
 
Kwa mujibu wa picha hii nahisi kuna kamgomo baridi bungeni
Mkuu, si mgomo bali ni kawaida ya wabunge wa bunge hili kuchelewa kufika. Mwenyekiti amefika mapema kama picha ya hapa chini inavyoonesha ila wajumbe wapo wachache sana
 
Vifungu vya 32 na 43 vinahusu nini? Vifungu vya kura ya wazi ama siri vimepitaje?
 
Taswira ya ukumbi wa Bunge saa 4.05 asubuhi hii
image.jpgimage.jpg
 
Vifungu vya 32 na 43 vinahusu nini? Vifungu vya kura ya wazi ama siri vimepitaje?
Mkuu, vifungu hivyo kwa kiwango kikubwa vinazungumzia ufanywaji wa maamuzi ndani ya Bunge, masuala ya akidi, majukumu ya makati za bunge na mengine mengi. Suala la upigaji kura kwa siri au wazi lipo kwenye vifungu vya 37 na 38 ambavyo ndo vitapitishwa leo
 
Ila ushabiki wenu wa kipuuzi muache kama mmeamua kuripoti kwa ajili ya wote iwe hivyo, sawa?
Sawa mkuu. Hilo usihofu kabisa. Ukweli tutausema daima
 
Hivi hawa wajumbe nao tuwaeleweje? Ya nini kupoteza muda kwa kuchelewa kufika ukumbini? Wanateketeza kodi zetu bila huruma
 
Back
Top Bottom