WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA FANYENI LILILO WAPELEKA
Inasikitisha sana kuona wajumbe wa bunge maalum wakisahau jambo moja tu lililowapeleka, ambalo ni kuandaa katiba mpya. Haiwezekani kabisa watu kwenda huku hawajui nini umuhimu wa jambo wanalolifanya kwa TAIFA lao. Yapo mengi yameendelea yanayokatisha tamaa, na kusababisha tuliowengi kukosa imani na bunge hili katika uandaaji na upatikanaji wa KATIBA ILIYO HAKI NA KWELI. Naamini kabisa utakubaliana na mimi kuwa TANZANIA ya sasa imetawaliwa na siasa ambayo ni ya vyama vingi, ambapo tunapata vyama vikuu viwili yani CCM na CHADEMA, na nje ya vyama hivi vipo CUF,NCCR,UDP,TLP, N.K ambavyo ni dhahiri kuwa wanachama wake wamegawanyika wengine wakiwa wafuasi wa CCM na wengine CHADEMA. Jambo hili lio wazi na ni dhahiri kabisa ingawaje wapo watakaokataa kwa sababu moja tu ya kuwagusa.
Wajumbe halikadhalika nao wamegawanyika katika makundi makuu mawili yaani wafuasi wa itikadi za kivyama ambao ni wafuasi wa itikadi za CHADEMA na wafuasi wa itikadi za CCM.Awe ni mwenyekiti, awe ni mlemavu, awe ni kutoka NGOS, awe ni padre, awe ni sheikh, awe ni mpagani wootee itikadi zao zimelala katika vyama hivyo vikuu viwili. Hii ni sababu kuu iliyonipelekea mimi kuandika huu ujumbe kwa wajumbe wa bunge maalum. Hakuna haja ya kudanganyana ni dhahiri watu wametawaliwa na uvyama ndani ya bunge hili. Na hi indo sababu kuu itakayo pelekea watanzania tushindwe kupata KATIBA ILIYO HAKI kama hali itaendelea hivi. Kila mmoja anataka kuvutia kwake na kusahau kuwa hawapo pale kwa ajili ya maslahi ya vyama vyao. Hivi si vikao vya vyama, na kama umetumwa kuja kuwakilisha chama chako na misimamo yake fanya hivo kwa kuzingatia na kuongezea akili zako ili ujue ni yepi yaliyo misimamo ya chama chako yana maslahi kwa Watanzania wote na yepi yana maslahi kwa wafuasi wa chama chako tu, kisha ufanye maamuzi.
Haupo bunge maalum kwa ajili ya maslahi ya CCM au CHADEMA, upo kwa maslahi ya wote haijalishi mtu katokea kijijini au laa, ila katiba mnayoiandaa lazima iguse watu wote kwa haki na kweli. Najua waliowengi wana imani kubwa sana na vyama vyao, na wengine ni wanafiki na waoga, na ingawaje wanaona kabisa misimamo ya vyama vyao haina tija kwa taifa bado hawadhubutu kuipinga. Ewe mjumbe lazima utambue kuwa si kila kinasemwacho na kuungwa mkono na CCM ni sahihi, kwani wakati mwingine kinaweza kuwa hakina maana, na pia si kila kisemwacho na CHADEMA ni sahihi wakati mwngine kinaweza kuwa hakina maana. Nikiwa na maana kuwa eti kwa kuwa jambo limesemwa na mtu wa CHADEMA basi wewe wa CCM yakupasa kulipinga kivyovyote vile hata kama wajua lina umuhimu, thats nonsense and stupidity. Na wewe wa CHADEMA kwa kuwa jambo limesemwa na mtu toka CCM basi wewe wapaswa kulipinga tu hata kama wajua lina umuhimu thats is a shame. Na kwa misingi hiyo hatutopata kamwe katiba ya haki na kweli kama wajumbe hawatakuwa tayari kuwa wazalendo wa TANZANIA rather than been CCM or CHADEMA. FANYENI LILILO WAPELEKA acheni kufanya mambo ya AIBU, kupitisha mambo kwa kuwa tu, yameletwa na kuungwa mkono na chama chako bali yana manufaa gani kwa watanzaniaa.
Zilindwe haki za watanzania wote, walemavu,wakina mama, watoto,waandishi wa habari na pia bila kusahau watu muhimu sana katika jamii yaani WASANIi. Naamini muda bado upo, mwakilishi anaweza kupatikana au kwa njia yeyote ile haki zao zihakikishwe zinawekwa kwenye katiba na pia kwa yale yaliopitishwa kimabavu, wanaharakati mpo, nafasi ya kuyatetea ipo, kwani haitoshi tu kujiita mtetezi au mwanaharakati bali lazima utetezi wako uonekane na upatikane kwa haki na kwa kufanya ivo tutakua mmewatendea haki watanzania kwa kuwaletea rasimu ambayo itakua imebeba mambo yanayo wanufaisha na sii kuaandaa rasimu ambayo mnajua kabisa kwenye referendum haitapita kwa vyovyote vile. Na nimalizie kwa kusema kuwa
Ni bora kulinda heshima yako kama kiongozi katika kusimamia haki na kweli KULIKO kulinda madaraka yako kama kiongozi kwa kusimamia unafiki na udhalimu katika jamii