Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Tuko pamoja! Saa nne ndo hii muda wa mwisho wa kurudisha fomu tupe majina ya waliorudisha fomu!
Mkuu, naendelea kufuatilia taarifa kwa vile muda huu sipo ofisi za bunge. Pindi nikipata nitakujuza mkuu na watanzania wote watajua kinachoendelea
 
Mkuu, mchakato ulikuwa wazi na hakuna mtu aliyekatazwa kuchukua fomu
Ndugu mwananchi hapo wamejazana wabunge wa chama chetu na katiba yao ya Lumumba kibindoni, hawataki kusikia serikali tatu (logic) Mtanganyika Mtikila angeingilia wapi?!
Kwamba uchaguzi ni huru na wa haki wakati wabunge wa chama chetu waliojazana humo hawako huru na hawana haki ni kiini macho
 
Mchakato umevurugwa, tusitegemee lolote kutoka BMK ni sawa na kukamua makende ya fahali kupata maziwa!
 
Hili bunge haliitaji m/kiti mwenye degree ya sheria tu ama masters linahitaji mtu mwenye sifa na skills za kuendesha mihadhara iliyoshiba...
 
Hili bunge haliitaji m/kiti mwenye degree ya sheria tu ama masters linahitaji mtu mwenye sifa na skills za kuendesha mihadhara iliyoshiba...
Sawasawa ndugu, kwanza huyu mnafiki Sita ndiye aliyezuia mjadala mpana na ulioshiba juu ya Richmond (akisaidiana na Mwakyembe) mpaka leo hatumjui aliyekuwa akimtuma Lowasa afanye kuburi dhidi ya maamuzi ya baraza la mawaziri ni nani?
Sasa mjadala mkubwa kama huu usiotaka kubembelezana, kupigiana makofi, kuoneana haya ndio atauweza?
 
Hata kama atalazwa itabidi aongoze bunge akiwa kitandani@ ni Mzee wa Viwango na kasi
 
Moja ya mijadala mikubwa iliyotawala katika vikao vya Bunge la Katiba wiki iliyopita ilikua ni ulingani wa ‪#‎jinsia‬ katika kushika nafasi za juu katika kuongoza Bunge hilo, hususani kwenye ngazi ya Uenyekiti au makamu wake ambapo baadhi ya wajumbe walisema, moja ikiwa imeshikwa na mwanaume, msaidizi wake awe mwanamke, au kinyume chake.

Nini maoni yako katika hili?
 
kwa hili kwanini wasichukue form na kupigiwa kura za wazi tuone unafiki wa wanawake!!!!
 
Mimi naona ni sawa kuwa na ulinganifu, maana ukiangalia vyama vingi wanaume ndiyo wengi na hasa ccm, hivyo njia pekee ambayo angalao itawabeba wakinamama ni kupitia utaratibu huo.
 
Wadau mida ndo inazidi kuyoyoma na taarifa nilizonazo ni kuwa Wagombea wote waliochukua fomu wametimiza sharti la kuzirejesha kwa wakati. Sina hakika na taarifa hii ila kama mdau aliyemiambia yupo sahihi, ni wazi kuwa leo jioni mchuano utakuwa baina ya wagombea hao wanne
 
Mkuu Chabruma hebu tupatie sifa za hawa wagombea wengine ukiachana na Mzee wa viwango
 
Tangu Bunge maalumu la katiba limeanza ,Wajumbe wanawake bunge la katiba wamekuwa wakionesha ushirikiano ulio na mashaka na kudai eti wanadai haki zao, Leo hii atakuwepo Mgombea Mwanamama mwenzao ktk. Uenyekiti wa kudumu (Terezia Uviza) na Sifa na vigezo anavyo, HAYA SASA MPENI KULA ZENU ZOTE tushuhudie maneno na dhamira zenu kama ni za kweli, nategemea kura zaidi 200.
 
Dah! Mkuu, hakika ni swali gumu sana hilo kwangu. Labda wadau wengine watasaidia kulijibu

kaka chabruma tunakutegea kwa update makini zisizo na uchama chama. Mimi nionavyo kumshindanisha mzee wa viwango na kasi na hao wengine hakuna balance mzee Sitta yupo juu sana. nasikia amesema anayo tiba ya namna ya upigaji kura ya maamuzi.
 
Tangu Bunge maalumu la katiba limeanza ,Wajumbe wanawake bunge la katiba wamekuwa wakionesha ushirikiano ulio na mashaka na kudai eti wanadai haki zao, Leo hii atakuwepo Mgombea Mwanamama mwenzao ktk. Uenyekiti wa kudumu (Terezia Uviza) na Sifa na vigezo anavyo, HAYA SASA MPENI KULA ZENU ZOTE tushuhudie maneno na dhamira zenu kama ni za kweli, nategemea kura zaidi 200.

Theresa Huvisa ni YAI VIZA linatumika KUVIZA yai nzima (read Sitta). M/kti wa Bunge maalumu hachaguliwa kwasababu ya KE yake bali uwezo wake.
 
Hivi huyu Huviza ndio aliebaraswa uwaziri hivi karibuni?
 
kaka chabruma tunakutegea kwa update makini zisizo na uchama chama. Mimi nionavyo kumshindanisha mzee wa viwango na kasi na hao wengine hakuna balance mzee Sitta yupo juu sana. nasikia amesema anayo tiba ya namna ya upigaji kura ya maamuzi.
Hakika mkuu. Ila kwa bahati nzuri ni kwamba hakuna aliyelazimishwa kuchukua fomu. Wote wamechukua kwa utashi wao na wanajiamini kuwa wanaweza kutumikia vema nafasi waliyoomba
 
Back
Top Bottom