Mkuu, naendelea kufuatilia taarifa kwa vile muda huu sipo ofisi za bunge. Pindi nikipata nitakujuza mkuu na watanzania wote watajua kinachoendeleaTuko pamoja! Saa nne ndo hii muda wa mwisho wa kurudisha fomu tupe majina ya waliorudisha fomu!
Ndugu mwananchi hapo wamejazana wabunge wa chama chetu na katiba yao ya Lumumba kibindoni, hawataki kusikia serikali tatu (logic) Mtanganyika Mtikila angeingilia wapi?!Mkuu, mchakato ulikuwa wazi na hakuna mtu aliyekatazwa kuchukua fomu
Mbona wagombea wengine wana kwashakoo mvuto hawana wanatuaribia mechi ya leo
Hujanitaja mimi,zaidi umewarusha wana lumumba
Sawasawa ndugu, kwanza huyu mnafiki Sita ndiye aliyezuia mjadala mpana na ulioshiba juu ya Richmond (akisaidiana na Mwakyembe) mpaka leo hatumjui aliyekuwa akimtuma Lowasa afanye kuburi dhidi ya maamuzi ya baraza la mawaziri ni nani?Hili bunge haliitaji m/kiti mwenye degree ya sheria tu ama masters linahitaji mtu mwenye sifa na skills za kuendesha mihadhara iliyoshiba...
Dah! Mkuu, hakika ni swali gumu sana hilo kwangu. Labda wadau wengine watasaidia kulijibu
Tangu Bunge maalumu la katiba limeanza ,Wajumbe wanawake bunge la katiba wamekuwa wakionesha ushirikiano ulio na mashaka na kudai eti wanadai haki zao, Leo hii atakuwepo Mgombea Mwanamama mwenzao ktk. Uenyekiti wa kudumu (Terezia Uviza) na Sifa na vigezo anavyo, HAYA SASA MPENI KULA ZENU ZOTE tushuhudie maneno na dhamira zenu kama ni za kweli, nategemea kura zaidi 200.
Hakika mkuu. Ila kwa bahati nzuri ni kwamba hakuna aliyelazimishwa kuchukua fomu. Wote wamechukua kwa utashi wao na wanajiamini kuwa wanaweza kutumikia vema nafasi waliyoombakaka chabruma tunakutegea kwa update makini zisizo na uchama chama. Mimi nionavyo kumshindanisha mzee wa viwango na kasi na hao wengine hakuna balance mzee Sitta yupo juu sana. nasikia amesema anayo tiba ya namna ya upigaji kura ya maamuzi.