Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Anauliza swali kua je kura itakayopigwa ni ya siri au ya wazi? Huyu katokea baa kama sikosei kwakua mwenyekiti kamwambia hiyo ndio faida ya kuchelewa!
 
Wagombea watajieleza mbele ya wajumbe kuomba kura kisha kura za siri zitapigwa kumchagua mwenyekiti
Kama Sitta anachaguliwa kwa kura ya siri, nitashangaa akija kuikubali kura ya wazi
 
Mgombea nafasi ya uenyekiti Hashim Rungwe anasoma waraka wake wa kuwaomba wajumbe kura zao!
 
Samweli Sitta ametakiwa kusubiri nje na ataitwa na watendaji, Joshua Nathari anaomba kutoa ufafanuzi ila kificho anamuhoji kua anaomba ufafanuzi chini ya kifungu kipi cha kanuni.

Kisha Joshua anauliza aina ya kura itayotumika, anajibiwa ni ya siri.

Sasa Hashimu amekaribishwa kujieleza.
Pamoja sana Mkuu. Ila Hashim Rungwe anaboa sana. Ni aibu anasoma maelezo yake ya kuomba kura. Nashangaa anasoma mpaka jina lake
 
Dogo Janja Nassari kaomba kitu kutoka kwa mwenyekiti anaomba ufafanuzi

...aka katoto "Nassari" kamechelewa, alafu kana anza kuuliza yale mambo ambayo yameisha pita!
 
Anasema kuwa amepata shahada ya kwanza katika chuo kikuu huria cha Dar es Salaam Tanzania
 
Rungwe ana mke na watoto watano, kabila lake ni mha ana miaka 66, ana shahada ya kwanza ya sheria.
 
Anasema kuwa yeye ndo mwafrika wa kwanza kuuza magari hapa nchini. Hiyo ilikuwa ni mwaka 1989
 
Rungwe ana miaka 66....ana shahada ya sheria....ni baba wa watoto watano....na ni mwafrika wa kwanza kufungua duka la kuuza magari Tanzania.
 
Rungwe anasema ni Mwafrika wa Kwanza kufungua duka la kuuza magari nchini
 
HASHIM RUNGWE ana jinadi eti mtanzania wa kwanza kufungua duka la kuuza magari! Loh!
 
Anauliza swali kua je kura itakayopigwa ni ya siri au ya wazi? Huyu katokea baa kama sikosei kwakua mwenyekiti kamwambia hiyo ndio faida ya kuchelewa!

Hapana alikuwa na maana yake, na mh. Kificho aliposema hiyo ndo faida ya kuchelewa, akamjibu kuwa ni Siri, sasa kama uliangalia walishangilia sana wabunge wengi. Lengo ni kuweka kumbukumbu sawa!
 
Back
Top Bottom