Chizi Fureshi
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 1,718
- 461
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wawili wameingia kwenye kinyang'anyilo cha kugombea uenyekiti wa kudumu wa wa bunge maalumu la katiba. Watu hao ni Hashim Rungwe na Samuel Sitta.
Kabla ya kuanza upigaji kura wagombea walipewa dakika tatu kila mmoja wao za kutoa maelezo ili mwishoe aombe kura. Wakati hoja ya kuuza magari ikionyesha kuwagusa wajumbe wengi kwa upande wa maelezo ya bwana Rungwe, Sitta alitoa mpya pale aliposema "Nitapambana na wale wachache wanaopinga kuwepo kwa muungano"
Kwa maoni yangu naona Mh. Sitta hakupaswa kusema maneno hayo. Anaonyesha wazi mapema kupambana na wale wenye mtazamo tofauti na wake.
Zoezi la upigaji kura limemalizika tusubiri matokeo.Wagombea wanachagua mawakala.Sita amemchagua mwana mama mh Bahati Ally Abeid na Rungwe amemchagua Rashid Ray kuwa wasimamizi wao. Mwenyekiti wa muda amesema zoezi la kuhesabu kura litachukua muda mfupi hivyo wajumbe wasitoke ukumbini wasubiri matokeo
Wabunge ndiyo watakaoamua kama kauli ya SITTA ni mbaya au la, wewe huozi kuona umuhimu wa Kauli ya SITTA na hapo ndipo tunakosea kuwahukumu watu. Kuna kosa gani SITTA kuonesha msimamo wake? Kura zimepigwa nitashangaa kuona wewe unapingana na kauli ya SITTA wakati anazoa kura zote zikiwemo za wapinzani.
Sitta amemchagua Mhe Bahati kuwa wakala wake wa kuhesabu kura. Makonda kaonekana kukunja uso sijui alidhani atateuliwa yeye? Yaani huyo kijana ni poyoyo kweli kweli.
Sent from my iPad using JamiiForums
Eti sitta vs hashim rungwe huu ni uonevu wa hali ya juu tyson vs matula
uke nyumbani pale kikaz zaidi
Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
Wale wenye nia mbaya ya kuvunja muungano watashughulikiwa, nijuavyo mimi Samuel Sita ni muumini wa Julius K Nyerere..
Angekuwa Rais wengi wa wanaopinga muungano wangekuwa ndani...
Nani kakuambia S3 kuvunja muungano
Mimi kura yangu nimempa SITTA , ni muwazi tu, siri ya nini?
Wabunge ndiyo watakaoamua kama kauli ya SITTA ni mbaya au la, wewe huozi kuona umuhimu wa Kauli ya SITTA na hapo ndipo tunakosea kuwahukumu watu. Kuna kosa gani SITTA kuonesha msimamo wake? Kura zimepigwa nitashangaa kuona wewe unapingana na kauli ya SITTA wakati anazoa kura zote zikiwemo za wapinzani.