Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Sorry wakuu nimechelewa katika shughuli za kujipatia riziki. Kura imepigwa ya wazi au siri?
 
Hivi rungwe aligombea ki kweli kweli au alikuwa anatania tu!
 
Mkuu Nyange hamna kura ya wazi popote pale ata China ambao wana baraza kuu la kikomunisti kura yao ni ya siri.

Mbona hawakupiga kura ya wazi kama wale jamaa walivyokuwa wanaongea udenda unawatoka? masisiemu mtakufa safari hii
 
Last edited by a moderator:
Nawaona wajumbe wanaendelea kupiga soga hapa wakati kura zikihesabiwa.
 
Dah! Mkuu, hadi kuwa wakala wa uchaguzi lazima uwe na CV? Yatosha tu kusema kuwa ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

Mtu anayeuliza CV kwenye uwakala yapaswa naye tukajua CV yake.
 
Heh! Sitta mbona hakumchagua mkewe kusimamia uhesabu wa kura?
 
Nadhani MTIKILA hakustahili kwenda BUNGENI, ana mambo ya kijiweni sana yeye na RUNGWE.


Mtikila ni mtu anayeweza kujieleza vizuri sana lakini anapokwenda nje anakuwa hatari. Binafsi nampenda kwa kusimamia Tanganyika kwa miaka yote bila kugeuka.

Lakini ndani ya CCM kuna wazembe wa kutisha kuliko hata Mtikila. Hawana mchango wowote!
 
Mheshimiwa 6 yuko sahihi kutangaza msimamo wake mapema ili wajumbe waamue kumchagua au kutomchagua
 
Namwona Zakia Hamdan Meghji ukumbini lakini kapungua sana kwa mwonekano wa mwili.
 
thatha, hii thread unaiharibu...hivi hujaona ajabu mnaochangia ni ninyi hao hao? Sifa kuu ya Mwenyekiti wa kikao muhimu kama hiki ni kutoshabikia upande wowote mapema kama alivyofanya Sitta. Kwa kauli yake hiyo kaonesha hicho kiti kinamzidi kimo na angekuwa na hata chembe cha busara angefuta hiyo kauli na kuwaomba wajumbe msamaha. Lakini ndiyo hivyo tena huo ndio msimamo, kama tunavyoambiwa, wa chama tawala na hivyo tusitegemee mjadala unaotanguliza maslahi ya Watanzania bali ya wana CCM. Of course Sitta ana nafasi nzuri tu ya kuchaguliwa na hiyo ni kwa sababu wajumbe wengi wako mle ndani kuwakilisha matumbo yao na ya waliowateua. Sitta ni moja kati yao watu hao na kwa hakika huu ni muendelezo tu wa kundi la kisanii ndani ya chombo chetu hiki ambacho kwa bahati mbaya maamuzi yake yataacha madhara makubwa kwa taifa letu huko mbeleni, yangu macho.
 
Last edited by a moderator:
Unatoa msimamo katika wakati muafaka na eneo husika (at a right time and space) pale unaomba kuwa judge wa watu wenye hisia na mawazo tofauti, katika hatua za mwanzo tu unaonyesha uko upande wa X na wale wa upande Y si wako!

sijaona tatizo lolote mkuu'kasema hatapenda kuona muungano ukivunjika'Muungano waweza kuwa wa serikali 2 ama serikali 3,means serikali ya Tanganyika,ya Zanzibar na ya Muungano
 
Back
Top Bottom