Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Hapo ndipo utakapojua kuwa mtu anayejiamni hapaswi kuogopa kupiga kura ya WAzi, SITTA amekuwa muazi bila kujali atapoteza kura au la. Na huo ndiyo msimamo unaotakiwa siyo woga woga usiyo na maana

Sita kawahadaa wabunge wa ccm ili wampe kura. Hayo mambo kwake hayana nafasi kabisa. Muungano ndo hautaki. Tusubiri tuone
 
Kwa kauli hii ya mh. Sitta kwamba WATAWASHUGHULIKIA wale wote wenye nia ya wazi ili wavunje muungano (wafuasi wa serikali 3) ni ya kulaani vikali popote tulipo, unguja, pemba, bara.
Naona huyu mzee kaanza kwa kujitia dole au doa sehemu ngumu kama hii.
Mùunganano wetu unajadiliwa kwa nini tulazimishwe?
 
Uko Sahihi kabisa Sitta is just another stupid man. Angalia alipokuwa spika ndo mtu wa kwanza kupandisha allowance za wabunge kwa kudai kwamba mbunge hastahili kuishi kwa shida. aliachiwa na leo hii ndo hayo! Leo tena amedokeza dalili kwamba mwishoni lazima kuwe na kiinua mgongo kwa wabunge.

Kwa tabia hiyo, huyu ndo anapendwa na hilo group la wabunge washangiliaji.
Kwa maoni yangu mzee six kaongea hivyo ili hata baadhi ya wajumbe kutoka CCM wanaompinga wampe kujihakikishia nafasi ya uspika. Lakini six anafaaa kuliongoza hili bunge.
 
SITA akileta misimamo ya chama chake Bunge litamshinda, hawezi kuviburuza hivyo vichwa vyote.
 
Kwa msimamo aliouonyesha mapema namna hii hakika natabiri atapata shida sana huko mbeleni....na hili bunge litavunjikia mikononi mwake. Kulikuwa hakuna haja ya kuropoka mambo ya muungano kwa sasa.

Sifa zimemponza mapema,

Alipaswa kumuonba M/Mungu ili ampe subra na busara juu ya kulijibu ulizo la yule kijana wa Mbozi "DAVID SILINDE", badali yake ati awatishia watu kwa dhereu kama zile...!!

Tulifahamu sisi wazee kuwa yeye ndo atapewa hiyo nafasi ya kuendesha hilo BUNGE, sasa kesha vuruga "CV" ya uongozi wake.

Naunga nawe juu ya mzozo wa pale katika kipengele cha Muungano.

Naamini tayari vitwa vishaanza kupanga mashambulizi ya kujitetea.

Akumbuke kuwa pale watu hawatizami ilimu ya mtu bali wanatizama "BUSARA" na kipengele hicho cha dhereu na ubabe umeigharimu CCM, CHADEMA, na chama chochote kile kitacholeta jeuri na dhereu juu ya mambo ya msingi.

Ingelikuwa kigezo ni "ILIMU" basi mwanzo kabisa pale wa kumpata Mwenyekiti wa muda angelipewa yule Prof. Mahalu lakini badali yake akapawa yule Mzee Pandu A. Kificho.
 
Wabunge wanaendelea kupiga kura. Mtikila naye amepiga ila sina hakika kama amepiga kisawasawa. Tutasikia idadi ya kura zilizoharibika na yeye atakuwa miongoni mwa walioharibu kura hizo. Ni mawaao yangu tu wadau

hata me nina wasiwasi huo!
Naona kapiga kura kwa kujificha sana.
 
Wabunge wanaendelea kupiga kura. Mtikila naye amepiga ila sina hakika kama amepiga kisawasawa. Tutasikia idadi ya kura zilizoharibika na yeye atakuwa miongoni mwa walioharibu kura hizo. Ni mawaao yangu tu wadau

Nadhani MTIKILA hakustahili kwenda BUNGENI, ana mambo ya kijiweni sana yeye na RUNGWE.
 
Hapo ndipo utakapojua kuwa mtu anayejiamni hapaswi kuogopa kupiga kura ya WAzi, SITTA amekuwa muazi bila kujali atapoteza kura au la. Na huo ndiyo msimamo unaotakiwa siyo woga woga usiyo na maana

Unatoa msimamo katika wakati muafaka na eneo husika (at a right time and space) pale unaomba kuwa judge wa watu wenye hisia na mawazo tofauti, katika hatua za mwanzo tu unaonyesha uko upande wa X na wale wa upande Y si wako!
 
Rungwe amemteua Rashidi Ray....kama wakala wake....6 amemteua Bahati Ali
 
Hapo ndipo utakapojua kuwa mtu anayejiamni hapaswi kuogopa kupiga kura ya WAzi, SITTA amekuwa muazi bila kujali atapoteza kura au la. Na huo ndiyo msimamo unaotakiwa siyo woga woga usiyo na maana

Kabisaaa...
 
Mheshimiwa Rashid Rai ametwuliwa kuwa wakala wa Hashim Rungwe. Na Bahati Ali Abeid ameteuliwa kuwa wakala wa Sitta
 
Sitta amchagua Bahati Ally Abeid kumhesabia kura wakati Hashim Rungwe amemchagua Rashid Rai
 
Back
Top Bottom