Muda mfupi uliopita mh. Zitto Kabwe amechangia katika bunge maalumu la katiba na kukemea baadhi ya wajumbe wanaotumia lugha ya matusi, vitisho pamoja na kejeli na kutoa rai kuwa cha muhimu ni kufikia maridhiano kwa kile alichokiita "Muungano ni Imani"
Aliongeza kuwa muundo wowote wa serikali huweza kuvunja muungano, iwe moja, mbili au tatu na pia akatoa mifano ya nchi mbalimbali zilizokuwa na miundo tofauti ya serikali lakini ikavunjika. Nchi kama vile Sudan na Somalia.
Mwisho kabisa akamalizia kwa kuwasisitiza wajumbe wajitahidi kutokutumia lugha za vitisho, ubaguzi na hata kejeli...