Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Leo ilikua zamu ya Mh Zitto Kabwe, sikumsoma kabisa uwasilisho wake
 
Maccm hawa wamama mnawatoa wapi? Mbona pumba tupu hata hoja hawana.
 
Zitto lazima tuwe na . muungano unaoeleweka ambao pande zote zitaridhia.
Tukiwa na muungano ambao upande 1 hauridhiki utavunjika tu na gharama yake ya kuulibda ni kubwa

Tatizo huyu jamaa anazunguka sana hataki kubainisha wazi ni Muungano gani wenye manufaa kwa mujibu wa mapendekezo yake sasa cha kuogopa ni nini kama ni tatu sema tatu na kama ni mbili kama wanavyotaka maccm sema mbili sio kujizungusha zungusha bila mwelekeo.

BACK TANGANYIKA
 
wanasiasa wa kitanzania wanatakiwa kuiga mfanano wa zitto kabwe... huezi amin jamaa kafika dar leo asubuh saa 11alfajir akitokea new dealth india.... mpk saa 2 alikuw dodoma.. lakin kaongea vit vya msing tangu mchakato huu uanze zitto na kafulila ni mfano wa kuigwa hatutak malumbano na vijembe vya taarab....
 
Muda mfupi uliopita mh. Zitto Kabwe amechangia katika bunge maalumu la katiba na kukemea baadhi ya wajumbe wanaotumia lugha ya matusi, vitisho pamoja na kejeli na kutoa rai kuwa cha muhimu ni kufikia maridhiano kwa kile alichokiita "Muungano ni Imani"
Aliongeza kuwa muundo wowote wa serikali huweza kuvunja muungano, iwe moja, mbili au tatu na pia akatoa mifano ya nchi mbalimbali zilizokuwa na miundo tofauti ya serikali lakini ikavunjika. Nchi kama vile Sudan na Somalia.
Mwisho kabisa akamalizia kwa kuwasisitiza wajumbe wajitahidi kutokutumia lugha za vitisho, ubaguzi na hata kejeli...
 
Hakuannchi duniani ambayo inatukana wasisi wake. Na bunge litakua wa mwisho kuwatukana wasisi. tunatatizo la kujifanya wajuaji. Hakuna mtu mwenye akili timqamu atakaye enda mbele ya hadhara na kuwakejeri. hati ya muungano nimeiona na nihalali na ndioy mtakayo iona hapa. haikuchakachuliwa.

Inashangaza sana na wakati fulani kutia hasira pale watu fulani ndani ya CCM na Serikali yake wanapojidai na kujinasibu mbele ya umma kuwa wanalinda na kutetea mambo yaliasisiwa na waasisi wa nchi yetu. Kwao wanaona suala la muungano ndiyo kubwa linafaa kutetewa kwa nguvu zote ilhal kuna mambo chungu nzima yaliyoanzishwa na Hayati Mwalimu Nyerere ambayo kwa makusudi na kwa kuendekeza ubinafsi wao wameishia kuyabeza na mengine kuyafuta kabisa jambo linaloonekana wazi kuwa ni matusi na dharau kwa huyo aliyeyaasisi.

Yapo mengi ikiwamo kuuawa kwa Azimio la Arusha, kuuzwa kwa mashirika ya umma; viwanda na hata nyumba za Serikali kwa kivuli cha uwekezaji na uwezeshaji wa wachache. CCM ya wakulima na wafanyakazi aliyoiasisi Mwalimu nayo wameigeuza kuwa chama ama club ya familia na marafiki wa karibu na maficho ya wahalifu, majangili na wahujumu uchumi.

Mbaya zaidi hata huo muungano wanautetea sasa sio ule walioachiwa na Hayati Mwalimu Nyerere kwani mwalimu aliacha muungano uliozaa nchi moja yenye Serikali mbili lakini kwa kushindwa kwao kusimamia viapo na madaraka waliyopewa na umma tuanashuhudia sasa kuwepo kwa muungano wenye nchi mbili na serikali mbili ambayo kwayo watawala wameshindwa kamwe kutoa ufafanuzi juu ya hilo.

Kwa upande mwingine watawala na mashabiki wa CCM wanadai na kudanganya umma kuwa Serikali tatu zitaongeza gharama za uendeshaji lakini wanashindwa kuona wazi kuwa utawala wa awamu ya nne chini ya Kikwete ndiyo utawala pekee ulioongeza gharama za uendeshaji kwa kuongeza kwa kiwango cha juu ukubwa wa Serikali licha ya ushauri mzuri uliotolewa na wataalamu wake. Mfano japo kwa uchache tumeshuhudia awamu ya nne chini ya Kikwete ikiongeza kiholela idadi ya Majaji wa Mahakama, idadi ya wizara za Serikali, idadi ya mikoa na wilaya, Majenerali wa Majeshi ya Wananchi, Wabunge wa kuteuliwa pamoja na Ma-RC na Ma-DC. Yote hayo watawala hawaoni kuwa yanaongeza gharama na yamefanywa kwa utashi binafsi pasipo kujali mzigo mkubwa unaowakabili wananchi wa Tanzania amabao ndiyo walipa kodi na wagharamiaji wakubwa.
 
Cmjui mkuu

kuna mambo mengi yamejificha juu ya huyu mtu.
Kama utapata muda pitia profile yake utajua mengi na kuelewa kwa nini amewekwa hapo ila mwenyezì Mungu aliujua unafiki kabla hajazaliwa ndio maana akampofua.
 
zitto amejitahidi sana kuongea kiungwana, mm ni mzanzibari lkn nimefurahi sana na presentation yake.

nimesikitika sana na wazanzibari wenzangu wenye asili ya kiafrika kama mm kuwatukana na kuwatusi wenye asili nyengine au sehemu nyengine.

mapinduzi lengo lake ni kuondoa dhulma na kuondoa ubaguzi na kuweka misingi ya usawa
 
Serukamba: CCM Tunalo jukumu la kulinda Muungano huu. Muungano utakuwa salama mikononi mwa CCM!
 
serukamba:wapo wanaosema CCM tunang'ang'ania s2 .. ni kwamba sisi tuna dhamana
 
Hivi huyu mama Rita kwel ameisoma rasimu?toka ameanza kuzungumza sijamuelewa
Kwa waliye muelewa anisaidie alikuwa anazungumzia nini?
 
Sitegemei kama kuna Tanzania hata mmoja anayeunga mkono upuuzi unaofanywa na wabunge yaani ni kichefuchefu, MH. Sita kama huna habari wajumbe wako wanaongea mpaka mapovu yanawatoka so kwa ajili ya katiba wanafanya maandalizi ya uchaguzi ujao, wametuibia pesa tu. Indoa Mara moja mkaba wa TBC hatuhitaji kuaikia upuuzi wao umetukifu.
 
Back
Top Bottom