Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Kasi ya kudai Zanzibar huru kwa pamoja bila kujali itikadi iliyokuwapo katika mchakato wa kukusanya maoni, imepotea kabisa na badala yake wajumbe kutoka Zanzibar wamegawanyika! Walau wle wa CUF wameendeleza kasi yao, lakini wale wa CCM wamebadilika na kuishusha nchi yao kiasi cha kusema haiwezi kujiendesha bila ya Bara. Kwa lugha nyingine wajumbe hao wa kutoka visiwani wanasema kwamba Bara imeshikilia roho ya Zanzibar. Kuna mmoja akaonyesha kuwa uchumi wa Zanzibar ulitegemea karafuu, sasa bei imeporomoka na hakuna kitu. Mwingine akasema hawawezi hata kuilipa Tanesco bili za umeme! Mwingine akasema JK alilazimika kuchota kitita cha fedha za Bara ili kufanikisha programme iliyokuwa imeshindwa kutekelezeka kutokana na uhaba wa fedha huko visiwani.

Kwa ujumla Wazanzibari wamejianika kweli kweli kuonyesha utegemezi wao kwa Bara, na bila shaka hawatakuwa na ujeuri wa kusema tena kwamba wao ni nchi sawa na Tanzania Bara ilivyo! Nasubiri bunge liishe nione kama jeuri itaendelea!
 
Ccm hawana uwezo wa kuona mambali wapo kwenye 18 hawatoki mtakuja kuona!!!!!!
 
Akitokea mjumbe wa bunge akasema Issa Shivji ni mhindi arudi kwao, watashangilia hivyo hivyo?
 
Ni kweli mkuu hilo hata mimi nimeliona tunaenda pabaya kama leo tunaanza kubaguwana kwa rangi

Mimi yangu macho
 
HEKOOO JUSSA KWA KUTOJIBU MATUC ,IVI KWELI HAO CCM WA ZNZ HUMO BUNGENI HAWAJUI UMUIMU WA KUWA NA NCHI YAO YENYE MAMLAKA KAMILI?cpati jibu

Hawa wanaowaponda akina Jussa watakuwa salama kweli wakirudi Zanzibar?
 
Alikuwa akiongea kama vile pale inatengenezwa katiba ya tanganyika hajui na znz kuna wavuvi wengi tu
 
dadavua, ubaguzi wa rangi kwa nani? na ilikuwaje?
Nafikiri mleta uzi kasikitika sana kiasi hawezi hata kuandika vizuri!
Hawa ssm ni watu wa ajabu na historia iawaweka wazi kama waleta machauko hapa nchini. Walianza na slogans za 'uislamu na cuf', wenye akili ndogo ndio wanajua kuwa hilo limeisha lakini mizizi ya udini ilishapandwa na tusubiri matunda yake. Wakaja 'uchaga na cdm' na sasa hivi wanadhani eti chama kinakufa lakini mbegu zilishapandwa na tusubiri matunda pia. Sasa sio ajabu kuwa wanaanza 'kuinvest' katika ubaguzi wa rangi......
Cha kukumbuka hapa ni Mwalimu na msemo wake kuwa "ukishakula nyama ya mtu kamwe hutokaa uache".

 
Nilitegemea Membe alipokuwa anazunchangia angejaribu kutumia busara kutuliza mzuka pale bungeni hasa kutokana na wabunge kutoa lugha kali za kutukanana na kukashifiana na kubaguana kimaeneo. Cha ajbu membe naye akaingia kwenye miapsho ya kivyama.

Nilitegemea membe km mtu anayetamani kuliongoza hli taifa aoneshe busara za kiuongozi, hasa kusisitiza na kuonesha umuhimu wa muafaka katika yanayojadiliwa. lakini yeye hajaona kwamba mbele kuna kiza kinene! Kwa maoni yangu membe ameshindwa hata na vijana wadogo km Ezekeilei Miage, jana aliongea vizuri sana bila ushabiki, na zitto leo naye amejitahidi.

Na nimemependa zitto alivyojaribu kuwakumbusha viongozi wakubwa pale bungeni kwamba wana wajbu wa kukemea ubaguzi wa rangi na wa kimaeneo unaondelea pale bungeni badla ya kuwapigia makofi. Nchi inavunjika watu wanashangilia kisa serikali mbili zinatetewa.

Hii nchi imekosa uongozi! Bunge la katibs limekosa uongozi Tutafika kweli ndugu zangu?
 
Nilitegemea Membe alipokuwa anazunchangia angejaribu kutumia busara kutuliza mzuka pale bungeni hasa kutokana na wabunge kutoa lugha kali za kutukanana na kukashifiana na kubaguana kimaeneo. Cha ajbu membe naye akaingia kwenye miapsho ya kivyama.

Nilitegemea membe km mtu anayetamani kuliongoza hli taifa aoneshe busara za kiuongozi, hasa kusisitiza na kuonesha umuhimu wa muafaka katika yanayojadiliwa. lakini yeye hajaona kwamba mbele kuna kiza kinene! Kwa maoni yangu membe ameshindwa hata na vijana wadogo km Ezekeilei Miage, jana aliongea vizuri sana bila ushabiki, na zitto leo naye amejitahidi.

Na nimemependa zitto alivyojaribu kuwakumbusha viongozi wakubwa pale bungeni kwamba wana wajbu wa kukemea ubaguzi wa rangi na wa kimaeneo unaondelea pale bungeni badla ya kuwapigia makofi. Nchi inavunjika watu wanashangilia kisa serikali mbili zinatetewa.
Sitta naye yupo kimya tu. Hivi wanajua haya mambo yanaweza kusababisha umwagaji mkubwa wa damu katika nchi hii?

Hii nchi imekosa uongozi! Bunge la katibs limekosa uongozi Tutafika kweli ndugu zangu?
 
Mawazo ya wajumbe wa bunge la katiba, mengi hayana tafiti, na hivyo siyo lazima yawe sahihi. Nimesikiliza hoja za ZZK, hoja zenye mashiko, nasikitika CDM kutomtumia katika kuwajengea hoja, ila mawazo kuwa zanzibar haiwezi kujiendesha ni fikra mgando za baadhi ya wajumbe, na nadhani, wazanzibar walio wengi hawatakubariana na mawazo hayo.
 
Hee wewe unaangalia bunge gani? Hivi matusi ya Lisu ndio hoja na usomi, kama hujui huo ni upumbafu na kifo kisiasa.

Kamtukana nani acha ushabiki wa kizamani sikiliza hoja zilizofanyiwa utafiti.
 
Huyu aliyesema jinsia iwe tunu ya taifa anazidi kudhihirisha jinsi gani ccm ilivyojaza oil chafu bungeni maana hata maana ya tunu haelewi
 
na hutaamini na kuelewa kamwe with reference kwa kil huyo kipofu alichokisema leo,juzi na siku za nyuma kwenye bunge hili la katiba.!

Kuna vitu ambavyo ninaweza kumcheka na kumuhukumu navyo ikiwemo misimamo na kauli zake kwani hizo amechagua yeye mwenyewe kuziamini lakini naamini kamwe hajachagua kuwa kipofu. Kwa kumkebehi kuhusu upofu wake tunajishusha kupita kiasi sisi wenyewe pamoaja na hii Forum
 
Maneno matupu hayavunji mfupa. Vitendo ambavyo vimetokea baada ya Mwl. Nyerere kung'atuka na baadae kufariki vinaonyesha ni jinsi gani serikali za ccm zilizofuatia zilivyowavunjia heshima waasisi wetu.

Mwl. Nyerere ameonyesha kusikitishwa kwake kwa viongozi wa ccm katika kitabu chake Our Leadership and the Destiny of Tanzania (1995) p.14-15 kwa jinsi walivyoua Azimio la Arusha na kuondoa miiko ya uongozi.

Tunachokiona sasa ni muendelezo wa kutaka hali hiyo ya kuasi maadili ya waasisi iendelee. Ni wakati huo baada ya Mwalimu tumeona ni jinsi gani Mtanzania wa kawaida alivyozidi kuwa masikini, huduma za jamii kupungua au kuisha kabisa na usalama wa raia kuwa tete. Sambamba na hilo, tumeona ni jinsi gani rushwa, dhuluma, wizi, upendeleo, usultani, ukosefu wa maadili, uuzaji wa madawa ya kulevya, ujangili (nikitaja vichache tu), vilivyo endelea na kufanywa na hao hao viongozi wa ccm.

Ikumbukwe kwamba Mwl. Nyerere alishatamka kuwa alishafanya makosa, na kama Watanzania wako tayari kuyarekebisha, wanaweza kuyafanya marekebisho bila pingamizi lolote. Huwezi kufanya marekebisho yeyote bila kutambua ni wapi kuna hitilafu na kuitamka wazi. Hivyo basi, kutambua makosa yaliyopita ili kurekebisha hali kuwa nzuri si kukosa heshima.

Hata hivyo, kufumbia macho makosa ambayo yataleta madhara makubwa, kwa ajili tu ya faida ya watu wachache binafsi ni ukosefu wa heshima na unafiki mkubwa.
 
Mi naishangaa sana Hii serikali tulionayo madarakani kwa kweli wameshindwa kutoa hoja au kujibu hoja zinazotolewa na wajumbe mbalimbali hapa bungeni bali wamebakia tu kusema kuwa anayekejeli waasisi wa muungano wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria mi najua hawataki kuambiwa ukweli na kama ni uongo si hizo sahihi lisu alizozisema walete tu hiyo hati then wajumbe wapewe nafasi ya kuangalia na kufananisha hizo sahihi kama lisu alivyosema na kama ni kweli au uongo si sheria itafuata mkondo wake na siyo serikali kumtishia bhana.
Biguuuuup lisu na bado hawajawa..
 
Back
Top Bottom