Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
... Lakini kumbuka mawazo hayo yanatolewa kwa njia iliyo rasmi na wawakilishi wao waliowaamini!... mawazo kuwa zanzibar haiwezi kujiendesha ni fikra mgando za baadhi ya wajumbe, na nadhani, wazanzibar walio wengi hawatakubariana na mawazo hayo.
Hivi hiyo Maziku anafahamu ni sura ngani zinazojadiliwa? Kwanini asisubiri hizo sura zinazohusu haki za wakulima na wafugaji ndiyo aongee? Kwanini M/kiti anaruhusu wajumbe kuropoka vitu ambavyo viko nje ya maada? SUA 1 na 6 zinaongelea muundo wa muungano, wajumbe wote wanatakiwa michango yao kulenga hapo, hata kama wana AKILI ZAO NI ZA KIKULIMA (no offense intended).
1: Stephen Wasira
2: Masumbuko Lamwai
3: Makongoro Julius Nyerere
Kuna vitu ambavyo ninaweza kumcheka na kumuhukumu navyo ikiwemo misimamo na kauli zake kwani hizo amechagua yeye mwenyewe kuziamini lakini naamini kamwe hajachagua kuwa kipofu. Kwa kumkebehi kuhusu upofu wake tunajishusha kupita kiasi sisi wenyewe pamoaja na hii Forum
bado hujaelewa na kuamini, endelea kusubiri.
Bavicha wengi wanaakili kama zako endeleeni na wehu wenu.Kwa hiyo ina maana yeye Mpanju alimgusa Mungu machoni ndiyo maana akampiga UPOFU wa macho?! Eti Serikali 3 ni kaburi la Muungano! Huyu Mpanju amekuwa mpiga ramli siku hizi? Nafikiri Mungu hakumpiga UPOFU wa mcho tu, bali pia alimpiga UPOFU WA AKILI!
Pima cd4 coz viruses wako wanaonekana kushambulia sehmu za ubongo. Ndio maana unapoteza kumbukumbu kisha uwahi kulala na mazoezi ni muhim
Unapoongea Kumbuka ameenda pale akiwa anawakilisha walemavu wenzie wengi tu ambao wengine hawapendi ccm wala chama kingine chochoteKwani mtu akiwa mlemavu hawezi kuwa mfuasi wa chama cha siasa? Mbona mbunge wa Lindi mjini ni mbunge wa kuchaguliwa kwa tiketi ya CUF?
Alikuwa akiongea kama vile pale inatengenezwa katiba ya tanganyika hajui na znz kuna wavuvi wengi tu
Endelea kuinamishwa na kundi la watoto wa mme wa baba yako!Bavicha wengi wanaakili kama zako endeleeni na wehu wenu.
Tusubiri hyo jioni
Na ham ya kumsikia mtikila na lipumba jamani
Akili yako kama ukawa,umepofuta,hata wewe unaamini sahihi ya Karume ni fake?Mi naishangaa sana Hii serikali tulionayo madarakani kwa kweli wameshindwa kutoa hoja au kujibu hoja zinazotolewa na wajumbe mbalimbali hapa bungeni bali wamebakia tu kusema kuwa anayekejeli waasisi wa muungano wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria mi najua hawataki kuambiwa ukweli na kama ni uongo si hizo sahihi lisu alizozisema walete tu hiyo hati then wajumbe wapewe nafasi ya kuangalia na kufananisha hizo sahihi kama lisu alivyosema na kama ni kweli au uongo si sheria itafuata mkondo wake na siyo serikali kumtishia bhana.
Biguuuuup lisu na bado hawajawa..
Bunge Maalum la katiba linaendelea muda huu na leo wajumbe wataendelea kujadili sura ya kwanza na sita ya rasimu mpya ya katiba.
Mh. Sereweji
kutoka Zanzibar anasema kuwa muundo wa serikali mbili bado unatufaa,wazanzibar tuna kila kitu hapa Tanzania bara.
Anasema wapo bungeni kutafta katiba iliyo bora ya Tanzania na anawasihi wanaosema wataenda Zanzibar kuomba muungano wa mkataba kuwa watakuwa wanavunja sheria.
Anasema mapinduzi yamefanyika Zanzibar unguja ila pemba imepelekwa bendera tu baada ya mapinduzi.
Anaunga mkono hoja ya serikali mbili.
Mh. Gaudensia Kabaka,
Ameanza kwa kuipongeza tume kwa kazi kubwa iliyoifanya ila akaishauri ilete na yale maoni ya mabaraza ya katiba.
Kwa ujumla yeye anapendekeza muundo wa serikali 2 ambazo hazimo kwenye rasimu.
Anaongezea kwa kusema kuwa serikali ya shirikisho itakua serikali hewa.
Kwa ujumla msimamo wa Kabaka ni serikali 2.
Mh. Mohamad Sanya,
anaanza kwa kusema ni muumini wa serikal tatu na atatetea kwa busara muungano huo.
Anasema Lipumba alionesha jinsi usamehevu wa kodi ulivyo mkubwa hapa na kudidimisha maendeleo.
Anasema hataki huu muungano wa sasa,na wanataka muungano utakaoondosha kero kwenye muungano wa sehemu mbili.
Anasema wasilete kisingizio kuwa wazanzibar hawana mafuta na gesi ndo maana wanataka muungano ila wanaweza kujenga nyumba zao bila utegemezi.
Anasema wapo hapa kuzungumzia mustakabali wa muungano huu na sio vyama vya siasa.
Anasema wawape nafasi waone watakavyoinua uchumi na hata kusaidia upande huu mwingine wa muungano.
Anasema rada kijeshi na mawasiliano ni za muungano lakini baada ya chenji ya rada kurudishwa zanzibar hawakunufaika na chenji hiyo.Wazanzibar wamechoshwa na muungano huu na wanataka mamlaka kamili ili waweze kuamua mambo yao wenyewe.
Anasema kwa muungano huu ccm wataendelea kupoteza kura nyingi visiwani maana wanajali matumbo yao na sio wazanzibar.
Zanzibar wana matatizo makubwa lakini hayatatuliwi,anasema kuna watu wa tanzania bara wana uwezo wa kufungua vitega uchumi zanzibar lakini hawaji bali watu wasio na mwelekeo kama wauza karanga ndo wanakuja zanzibar.
Anasema zanzibar wakiwa na mamlaka kamili wanaweza kuibadili zanzibar kuwa Hong Kong ya afrika mashariki.
Anamalizia kwa kusema serikali tatu ipo na italeta maendeleo baina ya pande zote mbili.
Mh. Diana Chilolo,
Anaanza kwa kusema yupo kamati no 12,na anaamini serikali mbili bado zinafaa kufanya kazi katika muungano huu.
Anasema hayaelewa hii rasimu kila akiisoma na kuitafakari mpaka alkafika wakati akakasiri.
Anasema labda jaji Warioba kaweka utashi wake na kwanini aweke utashi wake kwenye maslahi ya watanzania kwa kuwaongezea watanzania mzigo wa serikali tatu.
Wizara ya muungano ipo chini ya makamo wa rais aliye mzanzibar,na anasema kweli watu hawa hawajui kero za muungano?Wanazijua ndo maana kati mya kero 27 zimebaki kero saba.
Anamshangaa tundu lissu kuwa alikuwa hawataki wazanzibar hata bungeni lakini anashangaa unafiki wake sasa ni rafiki wa zanzibar na kuwapigania.
Anasema kero ya watanzania sio serikali tatu bali huduma nzuri,mishahara iboreshwe na maendeleo mengine.
Anawashangaa cuf kwa kutaka kurudisha usultani zanzibar.
Anasema kinachotakiwa hapa ni kuboresha muundo huu wa serikali mbili.
Anamuomba makamu mwenyekiti kuwa kwanini hawa wanaowakashifu waasisi wetu kwanini wasisimame mbele ya bunge waombe radhi maana watanzania wana hasira na watanzania hawapo tayari waasisi wao kudharauliwa. Anasema watu kama hawa usishangae wakawakana wazazi wao.
Anamalizia kwa kutoa mfano kuwa Sitta alipomwoa Magreth alikuwa anaitwa Magreth Simwanza ila baadaye akaitwa Magret Sitta, hoja yake ni kuwa Magret hajamkana baba yake kwa hiyo Tanganyika haijakanwa.
Tunu za taifa anazungunzia kuingiza swala la jinsia maana ni tunu kwa taifa lazima lienziwe 50/50.
Mh. Sixtus Mapunda,
Anaanza kwa kusema kuwa hataweza kuikana kweli, anaendelea kusema kuwa ukizoea kusema uongo huwezi kusema kweli.
Kuna watu walisema hakukuwahi kuwa na hati ya muungano na kuwakashfu wasisi wetu. 25/4 baraza la wawakilishi lilikaa zanzibar na kambona alihudhulia na aliporudi alipokelewa kalimjee akasema yaliyo tokea.
Anaendelea kupangua hoja za Tundu Lissu kuhusu kutokuwepo kwa hati ya muungano, kuhusu kukutana kwa Baraza la Mapinduzi.
Anahoji uhalali wa takwimu za tume ambazo anaona hazikuwa na uhalali kutokana na namna zilivyokusanywa hasa kwa kuacha maoni ya mabaraza ya kata na wilaya.
Anamalizia kwa kusema Tunu za taifa zienziwe.
Mh. Ali Omar Makame:
Anazungumzia umuhimu wa kuweka haki za walemavu katika katiba.
Hii katiba tuliyonayo imerekebishwa mara 11 lakini mambo ya ulemavu hayamo. walemavu tunataka elimu afya mikopo na ajira na mazingira rafiki.
Mimi ni muumini wa serikali mbili. Mimi sikusoma, wasomi watatuelekeza. Je serikali tatu gharama zinakuaje?
Sisi walemavu tunataka huduma, kwanini hizi gharama za serikali ya tatu zisisaidie wenye ulemavu?
Tusaidieni tutoke hapa tulipo sisi walemavu halafu ndo mfikirie kuongeza serikali ya tatu na ya nne.
Watu wenye mahitaji maalum katiba itamke ni watu wenye ulemavu. Vipofu, viziwi viwete ni maneno ya kutudhalilisha.
Kubomoa kunasababisha wajane na yatima,mkibomoa watakaopata tabu sana ni sisi walemavu.
Anaunga mkono serikali mbili.
Mh. Hamis Mnondwa,
anaanza kwa kusema ni muumini wa serikali mbili na ana sababu zake.Anawashangaa wanaoshabikia serikali tatu na anasema kuwa hizi serikali mbili kama zina matatizo basi matatizo yote yanaweza kufanyiwa kazi.
Anasema kuna vijana wengi hawana ajira kwanini hizo gharama za serikali tatu zisiwasaidie vijana.
Anasema serikali tatu ni kuua muungano wa tanzania bara na Zanzibar.
Tukiongeza serikali ya tatu ina maana tanzania bara na zanzibar bye bye.
Sasa hivi zanzibar wanajiuliza jeshi kubwa liko bara, hatuna hela za kugharamia uhamiaji wala hatuna mipaka. Tukiongeza serikali ya tau habari la muungano limekwisha.
Kwanini tusikae tukazungumzia mstakabari wa nchi? Muundo wa serikali tatu ni muundo ambao hauna shida,upo kwa ajiri ya kusimamia majeshi na madaraka.
Tanzania haina ardhi, Je serikali tatu itajenga wapi ofisi?
Je ni nini kitafuata kama sio mapinduzi?
Tutaliwa kodi mpaka ya kichwa na kodi ya kichwa itarudi.
Mh. Zainab Kawawa,
Nataka nizungumze na watanzania leo kwanini sikubaliani na serikali inayoitwa ya shirikisho. Nchi ndio inayozaa uraia na kutengeneza utaifa.
Jamhuri hiyo ya Tanzania haitoi huduma za afya, elimu na huduma zozote,haiwezekani.
Viongozi wa upinzani igeni mfano wa viongozi wa CCM, kwanini chama kimeendelea kuwa imara. Nyie hamna utashi wa kuvumilia na kukosoana.
Mna hadhi gani ya kuvaa koti linalofanana na wasisi wa nchi hii. Wajumbe wameonesha dhamira ya kuvunja muungano wetu.
Hivi ninyi mnaotaka serikali tatu kwa nia mbaya mnaonesha dhamira ya kuuvunja muungano huu,nani asiyejua CHADEMA haina wanachama Zanzibar?
Watanzania ndio wanaogawa uongozi,waroho wa madaraka ninyi na acheni njia za dezo.
Mh. Abubakar,
Anasema katiba ni nini? Katiba ni muelekeo wa baadae, katiba ni dira.
Katika hii katiba yetu kuna mambo mengi ni dhaifu kwa muungano.Katiba inaonesha ina mamraka tatu, ya Zanzibar, Tanganyika iliyotiwa kwenye mamraka ya muungano. katiba haina misingi ya muungano,ibara ya 98[1b].
Bunge inaweza kutunga sheria na kusema tu itumike Zanzibar, haiwezekani Zanzibar ina wawakilishi wake.
Mambo ya nje ina mabalozi kama thelathini kati yao Wazanzibar ni watatu tu, je wazanzibar hawafai.?
Kuna mbolea imetolewa na Japanyenye thamani ya billioni 10 lakini Zanzibar haijapelekwa hata mfuko mmoja,je huo ni muungano?
Lililopo hapa Tanganyika imevaa koti la Tanzania ndo maana ikiletwa mbolea inaenda Songea na Ruvuma. Sasa hili koti livuliwe.
Sisi Zanzibar tunataka serikali ya shirikisho, lakini lakini tumeimesema serikali moja mbili shirikisho hayafai inayofaa ni serikali tatu basi tumekubaliana nao.
Serikali tatu ndiyo zitatoa muelekeo wa swala hili. asanteni.
Mh. Ramadhan Abdallah Shaaban
anaongea sasa. Anasema kuwa mambo mengi yaliyoainishwa kama kero za muungano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba tayari yameshapatiwa ufumbuzi.
Anawataka wajumbe kutumia mjadala huu wa katiba kurekebisha kero zilizopo. Anasema kuwa wanachofanya wapinzani ni kama NDEKWA. kwamba wanatumia madai ya serikali tatu kwa ajenda wanazozijua wenyewe.
Kuhusu uwekezaji anasema kuwa wabara na wazanzibari wanawekeza kila upande. Amezitaja hoteli kama za Sea Cliff ya Subash Patel na Kiwonga inayomilikiwa na watu wa kilimanjaro.
Anapendekeza kurejesha mfumo wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano na ugomvi utakuwa umekwisha.
Anaunga hoja mfumo wa serikali mbili.
Mh. Waziri Rajab Salum,
anasema ni muumini wa serikali mbili si kwa kufuata mkumbo au kubembelezwa na mtu. Mimi ni msomi nimefanya research na kuona serikali mbili ndizo zitatupeleka mbele.
Huwezi kutengeneza shirikisho bila kuwa na washirika. Zanzibar kukubali shirikisho ni kuigeuza Zanzibar kuwa kama Eritrea na Comoro.
Wapinzani wa Zanzibar hawakuanza leo,wapinzani wa uhuru wetu wa 1964 ndo hawa hawa vizazi vyao vinaendelea kuwa wapinzani.
Unapozungumzia Zanzibar unazungumzia Unguja na Pemba. Anasema kuwa wapinzani wa mapinduzi ni hawa hawa wanaopinga muungano hasa kupitia vizazi vyao.
Anasema kuwa Wazanzibari wanaotoka Unguja, wana muingiliano na watu wa bara huku wa Pemba hawana muingiliano wa kidamu zaidi ya ule wa kibiadhara. Wanaotaka Serikali tatu wanataka kuvunja muungano na kuchukua maduka yao na kupeleka Pemba.
Nature ya binadamu yoyote anapoambiwa ukweli lazima akasirike. Kwa vile naunga mkono serikali mbili napendekeza rais wa jamhuri na makamu na rais wa Zanzibar na makamu rais wa kwanza na wa pili wa Zanzibar washirikishwe kwenye jamhuri na watambuliwe kuulinda muungano wetu.
Tupo hapa kama taifa moja,tuache ushabiki tuambizane ukweli.
Mh. Issa Gafu,
Anasema Naunga mkono mapendekezo ya wengi ya kamati namba 11. Tuendelee kubaki kwenye mfumo wa serikali mbili.
Ulinzi na usalama zinahitaji fedha nyingi,usalama na ulinzi upo kwenye serikali ya tatu ya muungano ambao hauna vyanzo vya mapato.
Zanzibar imetuchukua miaka 40 bila hawa wanasiasa kuyatambua mapinduzi tukufu ya zanzibar. kama anaweza kubana uhuru wako hawezi kukupa uhuru wa kuuukubali muungano.
Tatizo la zanzibar sio mfumo wa serikali bali uchumi. vinginevyo tukitaka serikali tatu ina maana tunataka kuuvunja muungano jambo ambalo sipo tayari kufanya hivyo.
Faida za muungano zipo nyingi tu. Bila muungano kusingekuwepo na sherehe za mapinduzi, maadui wa mapinduzi bado wapo. Shindanisha maendeleo ya miaka 200 tuliyo tawaliwa na miaka 50 ya muungano.
Hatukua na mtaalamu hata mmoja lakini sasa hivi tuna wataalamu wengi.
Nawaomba wabunge tukisimama tujisemee sisi wenyewe sio kuwasemea watanzania eti wamewatuma.
Mh. Tundu Lissu
anasema, Naomba nianze kwa kujibu vihoja. Kuna kihoja kinasema Tundu Lissu amemtukana baba wa taifa.
1995 baba wa taifa alihutubia Mbea akasema, asiyekubali kukosolewa hawezi kuwa kiongozi bora.
Baba wa taifa alikuwa binadamu hakuwa Mungu wala malaika alikuwa binadamu na hajawa mtakatifu bado.
Baba wa taifa alishawahi kuunga mkono vita ya BIAFRA wakliotaka kujitenga na Nigeria.
Anasema kuna watu walikimbia ccm na kukimbila nccr Mageuzi na walirudi baada ya Mwl Nyerere kufariki.
Hati ya makubaliano ya muungano haupo.Tumeoneshwa sahihi nenda ulinganishe. Leteni hizo sahihi hapa tuwaonesheni mlivyo waongo.
Zanzibar haijawahi kuridhia muungano mpaka kesho kutwa. Kama mashariti ya muungano hayajatekelezwa kwa miaka 50 ni halali?
Muundo wa shirikisho wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya Nyalali, Kisanga, Walioba na wananchi ndo unafaa.
Ndivyo alivyo pendekeza Mwakyembe miaka 20 iliyopita. Rais wa Tanzania Kikwete sio mkuu wa Zanzibar. Katiba ya Zanzibar inasema rais wa Zanzibar atakua ndio rais mkuu, na mkuu wa vikosi maalum, Ibara ya 26(1) ya katiba ya Zanzibar.
Haya sio maneno ya Tundu Lissu ni maneno ya katiba ya Zanzibar.
Nani anaye weza kusema sisi ni nchi moja. Kikwete akienda Zanzibar anayepigiwa mizinga ni Shein, Kikwete akiwa mbali kabisa. Mkiwa na rais magogoni mwingine mmnazi mmoja wakipishana itakuaje?
Tutengeneze utaratibu mpya baada ya miaka 50 ya kudanganyana. Tusipochukua hatua za haraka mbele ni giza tupu.
Watakaoanzisha muda si hawa wanaoanzisha katiba mpya bali ni wale wanaofumba macho wakati mambo yakiharibika.
Mh. Benard Membe
anasema, Huu ni muungano wa pekee na wa pili duniani uliodumu ukifuatia ule wa Canada.
Tunaweza kuunda muungano wa nchi hizi mbili lakini serikali ya Tanganyika itaua serikali ya muungano na shahidi atakua serikali ya Zanzibar.
Tume ya Warioba italaumiwa kwa kupaga mauaji hayo.
Naungana na CCM kwamba jibu pekee ni serikali mbili.
1988-1990 huu ndo ulikuwa ubishi Urusi.
Kwanini tusijifunze kwa Urusi iliyokufa baada ya mwaka mmoja?.
Nawauliza mpo tayari mkubali Zanzibar na Tanganyika msikusanye kodi, kodi ikusanywe na jamhuri? {wabunge wameitikia ndio}
Serikali gani duniani inayoendeshwa bila kodi?
Mifano niliyoitoa ya Urusi, Spain na Ujerumani inatosha. Tukiunda serikali tatu itaua muungano.
Hakuna nchi duniani ambayo inatukana wasisi wake. Na bunge litakua wa mwisho kuwatukana waasisi. Tuna tatizo la kujifanya wajuaji.
Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayeenda mbele ya hadhara na kuwakejeri.
Hati ya muungano nimeiona na ni halali na ndiyo mtakayoiona hapa na haikuchakachuliwa.
Mh. Khalifa Khalifa
anasema, Kwanini tumefika mahala kwenye chombo kama hiki baada ya kuleta hoja tunatukanana? woga huu wa nini?
Mimi tume ya Warioba naiunga mkono. Hawa walikua 30 sisi tupo 600 na kitu.
Warioba alisema tutenganishe mamraka ya muungano ya Tanganyika na Zanzibar yakae mbali.
Je ni halali mabolozi kutoka Zanzibar wawe wanne tu? je Zanzibar haifai kupata kiongozi mkuu jeshini? Tusikie humu ndani tukatukanana bure hadi kuwatukana viongozi wa nje.
Mtu anaongea ubaguzi wa Unguja na Pemba mnampigia makofi. mtu anakuja huku anajisifia kwa kabila lake mnampigia makofi -------- kama huyu.
Mh. Amon Mpanju anasema; Yanapotokea mafuriko kama haya walemavu tunataabika,yanapotokea mabomu walemavu tunataabika.Sijapendezwa na kauri ya viongozi wanaosema kwamba kama serikali tatu haziruhusiwi tupo tayari kwa lolote. mimi ni mwenyekiti wa walemavu nina wafuasi pia, kuna wakulima wana wafuasi pia. Watanzania wenzangu hatunabudi kuwasusa watu wa namna hii. nawaomba sana vijana tusiwaunge mkono.
Jussa alinambia anapuuza taarifa na mimi ananipuuza. maneno haya yaliwaumiza walemavu. Tusimguse Mungu machoni kwani hakuna aliye amua kuwa mlemavu.
Ibara ya nne kuna mapendekezo yameletwa nami nayaunga mkono. ligha ya alama na lugha ya alama amguso itakua ni ligha ya alama kwa watu wasio ona. haya mabadiliko nayaunga mkono.
Nashangaa sana wanaanza kuhoji na kubeza uhalali wa huu muungano hasa tundu lisu. huu muungano sio wa wanasheria ,huu muungano unatambulika hadi UN. huu muungano una matatizo lakini tunaweza kuyatatua kwa kupitia muundo wa serikali mbili. uanasheria wenu usiwe kero.
Tuache kupotosha watanzania. serikali tatu ni kaburi la Muungano. tuache kuhubiri ubaguzi la sivyo zanzibar watagawana mikoba na huku bara tatagawana mikoba. Tuache kuwapa nafasi wazandiki na wanafiki wa nchi hii. wanasema wana watu wakati hawana watu kalenga na chalinze ilionesha.
Mh. Jussa
anasema, hawezi kujibu matusi kwani akili ndogo ndio inayojadili watu badala ya hoja.
Nasimamia matakwa ya Znz .. tunataka mamlaka kamili.
Anasema wanaosema kuwa serikali mbili zitaleta maendeleo Zanzibar mbona zimeshindwa kuyaleta kwa miaka 50?
tume ya Amina iliorodhesha matatizo lukuki ya serikali na wote walikuwa CCM
Mh. Yahya Kassim,
anasema katika upotoshaji huu kuna haja ya kuzungumza ili wapinzani waelewe.Wengine hawaelewi ukweli ulivyo.
Zanzibar imepatikana kwa mapinduzi na bara kwa kura na waliowaondoa hawapo.
Anasema zanzibar kweli wana uwoga,mana siku ya uchaguzi pia ni waoga kusema kuwa mwisho wa utawala wa weusi ni mwisho.
Kuja waarabu zanzibar wanakuja wanasema ardhi hii ya baba yangu anaitaka,je tutaishi wapi?
Anasema yeye ni muumini wa serikali mbili kwasababu katika rasimu hii hakuna mtu zanzibar aliyesema anataka serikali tatu,zanzibar walisema wanataka serikali mbili na ya mkataba.
Mh. Fathyiha Zahara Salum,
anasema kuwa wazanzibari walichoka kuuliwa ndo maana wakaamua serikali ya umoja wa kitaifa.
Kila siku watu wanauana na kuchinjana humu humu Tanzania chini ya s2.. tusitishane.
Mheshimiwa sana Zitto Kabwe,
Anasema kuwa mchakato huu ambao ulipaswa kujenga maridhiano, unajenga hali ya ubaguzi na kuna lugha na kauli za kibaguzi zinatoka huku watu wakishangilia.
Anasema kuwa tujadiliane kwa hoja, watu wajadiliane na wamue na kitakachoamuliwa ndicho kitakachoenda kwa wananchi
Anasema kuwa hakuna uhusiano wa muundo wa muungano na uimara wa serikali.
Muundo wowote wa Muungano, uwe wa serikali 1, 2 au 3 bila maridhiano utavunjika tu!
Hakuna utafiti wowote wa kitaalam unaothibitisha kuwa Serikali tatu zitaongeza gharama!
Tunaweza tukawa na rais mmoja wa Serikali kuu na wakuu wa nchi washirika.
Kuna jumla ya 2.3tril kila mwaka hazikusanywi kama mapato ya Taifa! Tunao uwezo wa kuendesha aina yoyote ya Muungano!
Anasema kuwa tunao uwezo wa kuendesha muungano wowote kama tukiamua kukusanya kodi ipasavyo.
Zitto anasema kuwa ikiwa muungano utavunjika, gharama za kuzilinda nchi zake ni kubwa zaidi kuliko gharama za mfumo wa serikali tatu.
Mh. Ritha Mlaki, Anasema anapendekeza S2
Mh. Serukamba, CCM Tunalo jukumu la kulinda Muungano huu. Muungano utakuwa salama mikononi mwa CCM!
Wapo wanaosema CCM tunang'ang'ania s2, ni kwamba sisi tuna dhamana.
serukamba:Lissu alisema uongo wa miaka 50 umefika mwisho..Mwl ameleta uhuru na amani na muungano
Mnataka kuudumisha Muungano gani ambao mnadai hati zake zimegushiwa?
Mnaotaka s3 mnasema mnataka muungano imara lakini mnataka kuvunja muungano.
Anasema Jussa anataka Zanzibar yenye Mamlaka kamili. Anamaanisha TUUVUNJE MUUNGANO!
===============
Makamu mwenyekiti anatoa matangazo ya wageni wa wajumbe wa bunge maalum la katiba pamoja na wageni wengine waalikwa.
Anasema amepokea hati ya makubaliano ya muungano na ni certified copy.
Anamkaribisha mh. Wassira aweze kutoa neno kuhusu hati hiyo.
Mh. Steven Wassira, anasema hati hiyo ipo na ni halisi na ipo katika hali nzuri hata baada ya kusainiwa miaka hamsini iliyopita.
Anasema kuwa Tundu Lissu na wenzake walikutana baada ya kujua hati ipo na wakakubaliana waseme saini ya Sheikh Karume sio ya kweli.
Anasema watanzania tujihadhari na mawakala wa shetani.
Anasema waasisi wetu wametukanwa sana mpaka kuitwa madikteta na hali hii haivumiliki kwa watanzania wote.
Anasema heshima ya waasisi wetu hailindwi na vyama bali inalindwa na italindwa na watanzania wote.
Makamu mwenyekiti,
Bunge litaendelea Saa kumi jioni.
Anasitisha kikao cha bunge maalum la katiba.