Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatatu 17 machi 2014-Viapo kwa wajumbe, Jaji Warioba Kuwasilisha Rasimu

kwani huyo anaetakiwa kuja kuzindua bunge la katiba yukowapi? Analipa umuhimu gani hili jambo mpaka ashindwe kuliweka kwenye vipao mbele vyake vya ratiba? Je inawezekanaje kuwakilisha katiba kwenye bunge ambalo halijazinduliwa?
Ni kweli mtu huyu alieweza kutoa msafara toka uswis na kukatiza ziara kuja kumzika bwanamdogo marehemu mbungei kumuandalia njia nzuri mwanae tena ikijua akizika tu anarudi adis kwenye mkutano haoni kama ipo haja kuzindua bunge? Haoni kama hili ni muhimu kuliko lala salama bwana mdogo umuachie mwanangu jimbo?
Ni ubinafsi, mtindio wa fikra, kupuuzia au ni nini?

Najiuliza aina ya mtawala tulienae.
mkuu hoja yako nzuri lakini umeiweka si mahali pake!
Hapa ni kanuni zimebutuliwa ili warioba amtangulie huyu mzaramo ilhali uhalisia anatakiwa azindue ,na warioba awasilishe katiba mpira uanze
 
wadau labda naomba mnisaidie kuna jipya gani ambalo hawa UKAWA wanatarajia endapo Mh. Rais atakuja kuzinduwa hilo bunge? kwa ufupi kuna tija ipi hapo??

Tatizo sio jipya gani, tatizo ni kuvunjwa kanuni za Bunge kwa maslai ya ccm.!
 
nathani tatizo ni kwamba sheria inasema rais azindue bunge ndio warioba awasilishe ila ccm wakalazimisha warioba awasilishe kwanza ili rais amjibu. Wapinzani wamegoma

wote wasiojua kiini cha vurugu wasome hapa!
 
Haya sasa Mzee wa standard na speed katolewa speed yeye mwenyewe, anadhani wabunge wote ni kama wanae nyumbani. ile siku ya kuchaguliwa alitangaza vita rasmi kua atawakomesha wote wanaotaka kuvunja muungano. battle imeanza sasa ajipange kweli kweli
 
Ohoooo! Kumbe hoja yao ni rais ahutubie kwanza! Mimi nilidhani asubuhi waliridhiana na Kiti baada ya maelezo aliyoyatoa kabla ya kuliahirisha Bunge. Kumbe waliburuzwa! Hapo patamu, Sita akae sawa hata kwa maswala yenye utata.

Anamatatizo makubwa sana ya uono wa uongozi.
 
Sitta anataka kuleta hasara kama alivyofanya kwenye issue y Richmond. Kwa week 3 bunge maalum limetumia mamilioni, fedha ya mlala hoi, kitunga kanuni za bunge, halafu yeye (Sitta) analeta ubabe na kupindua kanuni? Kulikuwa na umuhimu gani wa kukaa week tatu kutunga kanuni kama hazifuatwi?

Hay sasa kamvunjia heshma mzee wa waru Warioba. Na.nani atalipa gharama za kumpeleka Warioba Dodoma wakati hatakiwi kwa leo? Nadhani wachukue posho ya Sitta ifidie huu ubabe wake.
 
Chabruma Chabruma sikusomi vzr mkuu, hebu lete dondoo, nini kinaendelea baada ya 6 kukwamishwa na wajumbe hadi kusitisha shughuli kwa muda?
 
Last edited by a moderator:
Unajua katika mabunge muhimu kama haya haina haja ya mwenyekiti kujifanya mzoefu saaana au anajua sana sheria hapa rungu ni busara na hekima kama za mfalme suleiman ubabe hauna nafasi katika mambo yanayogusa maslai ya jamii
 
Hii nchi ngumu mkuu hapa mzee wa viwango tayari maji ya shingo!!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app

Huu mtego hata lowassa aliupenda sana siku Sita ameukubali. ni hili zigo ndilo litammaliza mzee Sitta kisiasa. Akiweza kuwashawishi watanzania CCM tayari haitaki la watanzania. Akiwapendeza CCM hana political future mbele ya watanzania (ikumbukwe ameishakuwa speaker he can't aim lower than that) so he will zero in on the opponents and blame them for everything.
 
Anamatatizo makubwa sana ya uono wa uongozi.

Ni kiongozi mzuri ila naona yuko hapo kwaajili ya kutumika katika mwamvuli wa yeye ni kiongozi wa speed na viwango! Anajikomba kwa anaotaka kuwatumikia. Ngoja tuone saga hilo litaishaje.
 
Hii ni nzuri kuliko kutoka nje ya ukumbi wa Bunge. Ubunifu huu wa kupiga makofi ya mbao ni mzuri
 
tatizo inaonekana ni wajumbe kutoka vyama vya chadema,cuf,nccr na wale wengine wa upinzani na makundi ya kiraia hawakubaliani na mabadiliko ya kanuni yaliyofanywa na mwenyekiti yanayomtaka jaji warioba kusoma rasmu ya pili ya katiba kabla ya rais kuhutubia bunge hilo.Kwa wao wanataka kwanza rais ahutubie bunge hilo ndipo jaji warioba apewe wasaa wa kuwasilisha rasmu ya katiba bungeni.

Mkuu tenda haki. Hao wapinzani na makundi ya kijamii wanapinga kanuni kuvunjwa. Wanasimamia utaratibu unavyopaswa kuwa na si matakwa binafsi.
 
Back
Top Bottom