Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Jumatano, Tarehe 26 Novemba, 2014

Status
Not open for further replies.
wakuu hivi report ya PAC imewasilishwa mezani au hakuna maana mnanichanganya!!
 
Yericko muda unazidi kwenda ni maswali tu.Lete update tegeta saa ngapi!?
 
Mijitu ya Tanesco mpaka sasa wameshakata umeme mikoa kadhaa. Hapa lengo ni kuwafanya watanzania wasiweze kufuatilia mjadala wa ESCROW. Hii nchi sijui tunaipeleka wapi....

Mii nimeingia NMB baada ya MASENGEREMA kukata Umeme ofisini kwetu, siondoki humu
 
Wakati kipindi cha maswali na majibu kikiendelea bungeni, watangazaji wa Star Tv walikuwa wakijadili haya
 
Binafsi nimewasikia ila sikuweza kuelewa nini walikuwa wanaongea wakati matangazo ya bunge nayo yakiendelea.Naona walijisahau tu kwa bahati mbaya.
 
Kwa maeneo ambapo umeme umekata, kwa wale watu wa kuonyesha mpira wawashe majenereta tutatoa viingilio hata ikiwa buku tano.
 
Walikuwa wanamsema Kafulila kuwa katishiwa maisha kuwa atafurahoa ndoa yake kaburini. Wakawa wanastema ndoa yake bado changa. Walijisahau kuzima maiki zao nadhani.
 
Tanesko washenzi kweli yani washakata umeme baadhi ya maeneo Moshi.. Ila tunawaambia tuko makin kweli na siku zao zinahesabika..
 
Huu mpira naona utakuwa ni wa dk120, ila kama watakubali bunge likaliwe na mahakama tena kichwani hii itakuwa record mbaya ya bunge toka limeanzishwa..

Na huenda ikwawa kashifa mbaya zaidi kutokea toka historia ya bunge kuanza, ninaona uaminifu wa wananchi kwa vyombo vya nchi vikuu kupungua, mwisho nchi itakosa mwenyewe...
 
hapa naona hakuna jipya, kunadalili zote zikapigwa danadana tu! Watu wanafanya umafia kulizuia hili sakata ngoja tusubiri!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…