Matokeo
Wajumbe wa Bunge la Kitaifa wamepiga kura ya kumwondoa Naibu Rais, Rigathi Gachagua madarakani ambapo zilihitajika Theluthi mbili (2/3) ya kura za Wabunge wote, sawa na Wabunge 233, ili kufanikisha kupitishwa kwa hoja hiyo
Gachagua alisomewa mashtaka 11 yakiwemo ya Ufisadi, Ukabila na Matumizi mabaya ya Madaraka, ambapo licha ya kujitetea, Bunge limemkuta na hatia
Hatima ya Gachagua sasa iko mikononi mwa Seneti, ambayo inatarajiwa kuchunguza mashtaka hayo. Spika wa Bunge la Taifa, Moses Wetangโula amesema kuwa Spika wa Seneti, Amason Kingi atapokea taarifa rasmi ya uamuzi huo ndani ya Siku 7 na kuitisha Kikao cha Seneti kujadili suala hilo