Yanayojiri Bungeni Kenya: Wabunge 281 wapiga kura ya kumuondoa madarakani Gachagua

Yanayojiri Bungeni Kenya: Wabunge 281 wapiga kura ya kumuondoa madarakani Gachagua

Wakuu,

Wabunge 281 wapiga kura ya ndio kumuondoa aliyekuwa Naibu Rais Kenya, Rigathi Gachagua madarakani.

~ Waliopiga kura ya hapana - 44
~ Ambao hawakuchagua kokote - 1

Tanzania tutachukua muda gani kufikia huku?🌚


===

Tukio linaloendelea bungeni Kenya ni upigaji kura ili kuamua hatma ya Naibu Rais Kenya, Rigathi Gachagua kama atabaki kwenye nafasi hiyo au lah


---

Matokeo
Wajumbe wa Bunge la Kitaifa wamepiga kura ya kumwondoa Naibu Rais, Rigathi Gachagua madarakani ambapo zilihitajika Theluthi mbili (2/3) ya kura za Wabunge wote, sawa na Wabunge 233, ili kufanikisha kupitishwa kwa hoja hiyo

Gachagua alisomewa mashtaka 11 yakiwemo ya Ufisadi, Ukabila na Matumizi mabaya ya Madaraka, ambapo licha ya kujitetea, Bunge limemkuta na hatia

Hatima ya Gachagua sasa iko mikononi mwa Seneti, ambayo inatarajiwa kuchunguza mashtaka hayo. Spika wa Bunge la Taifa, Moses Wetang’ula amesema kuwa Spika wa Seneti, Amason Kingi atapokea taarifa rasmi ya uamuzi huo ndani ya Siku 7 na kuitisha Kikao cha Seneti kujadili suala hilo

Pia soma: Yanayojiri hoja ya kumuondoa Naibu Rais Rigath Gachagua leo Oktoba 1, 2024

Gachagia ataenda Court mtaumbuka
 
Duuh. Majirani hawana mchezo mchezo.
Wana mchezo wa chuki, ukabila na wanatumia muda mrefu kwa upumbavu huku wakigawana kodi za wananchi.

Gachagua hata akiondolewa, hakuna kitakachobadilika, ataingia fisadi tu kula hela za wakenya
 
Hiyo ndio Nairobi!
Mpango yeye anapiga suti na kula Kodi za watanganyika.
 
Sasa hapo akishinda huko mahakamani SI yanaweza kujirudia Yale Yale ya Ruto na Kenyatta? Alafu baadae unakuta Gachagwa ni president elect Kenya waachwe aisee
 
Back
Top Bottom