Na haya ndio madhara ya kulelewa na Single mother. Mtoto wa kiume aliyelelewa na mama akikua atafanya anachopenda mama. Mwisho wa siku mwanamke atakayekuja kuolewa na Chibu ajiandae kupendwa na Bi Sandra na si Diamond.
Wanawake wengi hatuoni hii effect ya kulea watoto wa kiume pekee yetu kwa sababu tu tumefarakana na mzazi mwenza tumekuwa wepesi sana kuwatenga watoto na baba zao lakini matokeo ndio kama hayo.
I doubt kama Diamond ni mtu wa kumsikiliza sana mamake linapokuja suala la mapenzi!
Diamond aliishi na Wema kwa takribani miaka 4 huku Wema kila cku akiandamwa na scandal!
Sidhani kama Bi Sandra aliufurahia ule uhusiano lakini Diamond alikomaa na Wema!
Tuje kwa suala la Zari!
Wapo watakaosema Bi Sandra angevumilia yote ya Wema Sepetu ili kumtumia umaarufu wake!
Lakini wakati Zari alipoanza na Diamond; Zari hakuwa na umaarufu kama aliokuwa nao hivi sasa! Zari alifahamika sana Ug na sio Tanzania!
Lakini ile anaanza uhusiano na Diamond tu; kashifa dhidi ya Zari zikaanza kuibuliwa na ku-trend mitandaoni huku Kinara wa kusambaza kashifa hizo akiwa ndugu wa karibu wa Ivan huku Ivan mwenyewe akichekelea tu bila kujali kwamba anayedhalilishwa na ndugu yake ni mama wa watoto wake!!
Kashifa zote za akina Bi Sandra kwa Hamisa; hazijafika hata 10% ya kashifa za King Lawrence kwa Zari!!
Mara Zari ni mzee
Mara Zari ana watoto wakubwa sawa na Diamond....
Zikaanza kuanikwa orodha za wanaume 40 waliolala na Zari!
Kilele cha kashifa kikawa a leaked distance sex video ya Zari!
Instagram ikachafuka!
JF ikatikisika!
Kila mmoja akatamani kuwa na smartphone afuatilie yanayojiri huko Instagram!
Hivi kuna mama wa Kiafrika ambae angependa kuona mtoto wake pekee wa kiume anakuwa na mwanamke wa aina hiyo?!
REMEMBER... wala si kwamba single mother ndivyo walivyo bali akina mama wengi wapo too protective kwa watoto wao wa kiume especially wakiwa na mali!
Leo hii wanaume wawasikilize mama zao basi angalau 50% ya ndoa zinaweza kuvunjika!
Back to issue ya Zari + Diamond mwanzoni mwa uhusiano wao!
Zikazushwa conspiracy theories za kila aina na kwa pamoja zikilenga kuonesha Zari amekuja kwa Diamond kwa lengo la kujipatia mali za Diamond!!
Tusisahau; hata familia ya Diamond, hususani mamake na Esma; wote hawa hawakumpenda Zari! Bila shaka hawa waliamini theory ya Zari kuja kuzengea mali za Diamond!
Diamond nae alitukanwa mitandaoni kwa ajili ya Zari!
Lakini pamoja na yote hayo; bado Diamond alikomaa na Zari! Hakusikiliza la familia yake wala la matusi ya mashabiki wa Wema!
BUT WHY NOW?!
Take it from me!!
Hivi sasa Diamond anaweza kurudiana na Zari wala si kwa sababu ya akina Bi Sandra bali kwa sababu washauri wake wenye akili wanaamini Zari ndie right person!!
Management yake na watu behind the scene wanaamini Zari ndie right person kwake!
Aidha, hoja hii inapata nguvu zaidi kwa sababu Hamisa alishaonesha u-stupid wake hadharani! U-stupid ambao, wakati mwanzoni akina B Sandra waliamini Zari kafuata mali za Diamond; hatimae wakaja kubaini kumbe ni Hamisa ndie aliekaa kimaslahi zaidi kuliko Zari!
Amini usiamini, Diamond hashauriki na hasikilizi la yeyote kwenye issue zake za mapenzi!!
Look at Kifesi! Amekuwa na Diamond for more than 3 years lakini post yenye mstari mmoja tu ya kumshauri boss wake issue za mapenzi; post hiyo hiyo imemfukuzisha kazi!!