Yanayojiri katika mahojiano ya Tundu Lissu Star TV leo Februari 16, 2024

Lissu hajakata mzizi wa fitina.........

Yeye amefafanua kuwa ni kweli katika maandishi, ruhusa hiyo ipo, lakini practically Hilo jambo haliwezekaniki.

ushanyoosha maelezo 👆hapo paragraph ya kwanza,paragraph zingine Gekul,DPP huko umepuyanga tu.
 
Ngosha nyanda alijinasibu yeye atamhoji lisu bila hofu ya kupokea maagizo Toka ju, kama wasafi, ila nilichoona yeye BINAFSI amekua na hofu kubwa zaidi pale lisu alipojaribu kuelezea tukio lake Kwa ufupi na Kwa kumtaja makonda kama mshukiwa wake mara moja...then akamtaja informant wake japo SI Kwa jina...Nyanda umeonesha huna balls kama ulivojinasibu Kwa kujaribu kumkatisha lisu asiendelee na kisa kile....na amekwambia muendelee na kipindi wakati mwingine. usiogope mpe nafasi sio mtu mwepesi kama wengine uliozoea...pole nimeona hofu Yako Leo.
 
Mwamba huyu
 
yote kwa yote Tundulisu ana mtu mwenye nguvu nyuma yake. Huyu mtu hii confidence ina kitu nyuma yake si bure.
Ni kweli CCM wameshindwa kumnunua kwa pesa yoyote ?
Mbunge Lusinde aliwahi kusema nenda Youtube kule anasema waliwahi kumfanyia Vikao kwenye Chama wanajadiliana namna ya kumnunua kwa gharama yoyote.

Mh anasema Kamati yoote ilikubalina kwa pamoja kuwa Tundu Lissu ni Mtu Mwaminifu na hana skendo yoyote.

Pili wakakubaliana kwa pamoja kuwa Tundu Lissu ana msimamo na Weledi wa hali ya juu.

Kwa hiyo wakapanga nani amsogelee kwenda kumshawishi?

Mh anasema kila mtu aliogopa na kikao kikaisha bila mafanikio.

Mh Lusinde anasema pamoja na kwamba wanatofautiana kiitikadi yeye Mwenyewe anamkubali sana Tundu Lissu.
 
Ngoja tukae humu kwa leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…