Yanayojiri kesi ya "Binti wa Yombo": Daktari aliyempima Binti aliyebakwa na Maafisa wa Jeshi atoa ushahidi Mahakamani

Kwa sasa hawawezi kuona shida, ila wakifika miaka 35-40 popote pale watakapokuwepo ndio wataanza kujutia kila hatua iliyowapelekea kushiriki kile kitendo kiovu.

Ila huyo maza nae sijui kichwani alifikilia nini,sisi madereva tuna kanuni inatuongoza ukiwa barabarani ujue unaendesha magari matatu yani la kwako, la nyuma yako na la mbele yako nikiwa na maana kuwa hata yule binti wa mwanamke mwenzie ilibidi amfikilie kama binti wa kwake.

Kwa yule binti hakika kwa umri ule asaidiwe tu kisaikolojia huko mbele mwenyezi Mungu atamlipa kadri inavyofaa.
 
Hakuna kesi hapo!!
Ni mitandao tu imekuza mambo...
Wanawake tumezidi ushankupe na mahangaiko Tupunguze jamani
 
Update (Agosti 21, 2024)

Mtaalamu wa Mawasiliano, Daktari Watoa Ushahidi Kesi ya Ubakaji wa Binti wa Yombo

Kesi inayowakabili watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa kwa makosa ya ulawiti na ubakaji kwa binti ambaye ni mkazi wa Yombo Dar es salaam, imeendelea kusikilizwa leo Agosti 21,2024, ikiwa ni siku ya tatu toka kesi hiyo ianze kusikilizwa mfululizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Akizungumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa mpaka kesho saa nne asubuhi Wakili wa watuhumiwa Godfrey Mwasonga amesema mwendendo wa kesi hiyo ni tofauti na namna inavyo ongelewa mtandaoni na kusisitiza kwamba ni hamsini kwa hamsini yaani yeyote anaweza kushindwa au kushinda.

Wakili Wasonga amesema shughuli ya leo ilikuwa ni kusikiliza mashahidi wawili.

"Leo tulikua tunamalizia ushahidi wa jana ambapo bwana Alfred alikuwa anaendelea kutoa ushahidi wake, yeye ni mtaalamu wa mambo ya uchunguzi wa kisayansi wa simu [mambo ya mtandao] kutoka makao makuu ya Polisi Dar es Salaam, amemalizia na Mawakili tumepata nafasi ya kumhoji kwa niaba ya washtakiwa," alieleza Godfrey Wasonga.

"Na tulikuwa na shahidi mwingine ambaye ni Daktari, anasema alimpima mgonjwa, yeye tumefanya naye mahojiano kuanzia saa tisa mpaka saa kumi," alifafanua zaidi Wasonga.

Kesi hiyo itaendelea kesho saa nne subuhi. Watuhumiwa waliofikishwa mahakamani ni wanne kati ya sita ambao ni Mt. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, Amin Lord Lema, Nickson Idala Jackson na C. 1693 Praygod Edwin Mushi.

Update (Agosti 20, 2024)

Washitakiwa warejeshwa lumande

Washtakiwa wanne katika kesi ya ulawiti na ubakaji wa binti wa Yombo ambaye video yake ilisambaa mitandaoni akifanyiwa ukatili huo wakiwemo Askari wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Magereza, wamerudishwa rumande mara baada ya kesi yao kusikilizwa kwa mara ya pili hii leo Agosti 20.

Waliofikishwa mahakamani katika kesi hiyo ni askari wa JWTZ - MT.140105 Clinton Damas, askari Magereza - C.1693 Praygod Mushi, Lord Lema na Nickson Jackson.

Update

Shahidi mmoja asikilizwa

Wakili wa upande wa utetezi Meshack Ngamando, wa kesi ya ubakaji na ulawiti wa binti wa Yombo inayowakabili watu wanne wakiwemo Askari wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Magereza, amesema kwamba kesi hiyo imeendelea hii leo na imeanza kwa kusikilizwa kwa shahidi mmoja.

Wakili Ngamando amesema mashahidi kwa siku ya leo walikuwa watano lakini kutokana na muda ni shahidi mmoja pekee ndiye aliyewezwa kusikilizwa.

"Kesi inasikilizwa vizuri na hakuna shida yoyote, wananchi tuwe na utulivu tusikilize kesi nina imani kwamba haki itatendeka," amesema Wakili wa upande wa utetezi.

Update

Saa 6:33 PM (saa kumi na mbili na dk 33) - Mahakama ilisimama kwaajili ya watuhumiwa hao kupata chakula na kuendelea tena 7:30 PM (Saa moja na nusu usiku)

====

Watuhumiwa wanne wakiwamo askari wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Magereza wanaotuhumiwa kwa ubakaji kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti wa Yombo Dovya jijini Da es Salaam, wameingia chumba cha Mahakama.

Kesi hiyo iliyokuwa imepangwa kuanza saa 8:00 mchana wa leo Jumanne, Agosti 20, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, wameingia kwenye chumba cha Mahakama saa 10:20 jioni.

Watuhumiwa hao wanaodaiwa ‘kutumwa na afande’ ni askari wa JWTZ MT.140105 Clinton Damas, askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Lord Lema na Nickson Jackson.

Zaidi soma hapa: Mrakibu Msaidizi wa Polisi Fatuma Kigondo afunguliwa shtaka la kutuma vijana kufanya ukatili kwa binti wa Yombo

Awali, watuhumiwa hao waliingia kwenye chumba cha Mahakama saa 9 alasiri lakini walirudishwa tena ili wazungumze na mawakili wanaowatetea kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi.

Aidha waandishi wa habari wamezuiwa kuingia kwenye chumba cha Mahakama wakati kesi inaendelea wala kupiga picha watuhumiwa wakiwa kwenye korido za mahakamani huku wakiambiwa wasubiri watoke nje ndiyo wawapige picha.

Bado haijajulikana idadi ya mawakili wanaowatetea wala majina yao lakini wameshafika mahakamani kwa ajili ya kuwatetea watuhumiwa hao.

Jana Jumatatu, watuhumiwa hao walipandishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbili binti huyo.

Pia soma: Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Makao Makuu, Renatus Mkude alisema kesi hiyo itasikilizwa kwa siku nne mfululizo kuanza leo hadi Ijumaa, Agosti 23, 2024.
Wasije wakasema ushahid haujitoshelezi
 
Natamani hawa wahuni uchwara wakifika jela tu nao wabakwe hadi akili ziwarudie. Mbwa wakubwa!
 
Mhanga wa ubakaji anatakiwa kupimwa masaa yasizidi 12 baada ya tukio. Miezi mitatu
1000032432.jpg
baada ya Makanda wa Chadema kuibua huu uovu Daktari anapima nini?
 
Mhanga wa ubakaji anatakiwa kupimwa masaa yasizidi 12 baada ya tukio. Miezi mitatu View attachment 3076894baada ya Makanda wa Chadema kuibua huu uovu Daktari anapima nini?
Vyovyote itavyokuwa muhimu haki ipatikane hili si swala la kisiasa mtu yeyeto mwenye utashi hapaswi kulifumbia macho hili swala la kudharirisha wanawake.
 
Ni kweli. Sasa katika kuipata haki ndiyo ushahidi unatakiwa. Swali ni Dr anapima nini? Tusaidieni
 
Mhanga wa ubakaji anatakiwa kupimwa masaa yasizidi 12 baada ya tukio. Miezi mitatu View attachment 3076894baada ya Makanda wa Chadema kuibua huu uovu Daktari anapima nini?
Anapima kama kaingiliwa sasa kaingiliwa na nani ni kazi ya mashahidi wengine, what if kama ingekuwa wanasema kaingiliwa alafu binti akukutwa ni bikra?
 
Ni kweli. Sasa katika kuipata haki ndiyo ushahidi unatakiwa. Swali ni Dr anapima nini? Tusaidieni
Miongoni mwa mengine, pia atapima kama kweli ameingiliwa kinyume na maumbile.
Hata kama ni siku nyingi zilizopita ila madhara yake bado yataonekana.

Nb. Aliyeshikwa na ngozi ndiye mwizi wa ng’ombe.....mpaka itakapodhibitishwa vinginevyo.
 
Ampime nini wkti video ipo? Anyway Kama watu waliolawiti watoto wakafungwa maisha walisamehewa na raisi? sabaya mnyanga'nyi na mtekaji maaruf alisamehewa,sitegemei hawa vijana watakaa jela muda mrefu.. jela za TZ ni kwa ajili ya wezi wa kuku na wafanya fujo baa
 
Tutayasikia na kuyaona mengi sana mwaka huu wa uchaguzi na mwaka ujao.

Nahisi "joto la uchaguzi" limeshaanza ndani na nje ya CCM.
 
Back
Top Bottom