15 September 2020
Njombe mjini
Tanzania
Hotuba Live ya Tundu Lissu siku ya Kampeni tarehe 15 September 2020
Kwanza mgombea urais Tundu Lissu atoa Shukurani za kipekee kwa marehemu Salim Turky mbunge wa CCM jimbo la Mpendae Zanzibar kwa kutoa dola 100,000 ili ndege imkimbize Tundu Lissu toka Dodoma kwenda Nairobi. Na kuowaomba waTanzania kwa umoja wetu kuwapa pole familia ya marehemu Salim Turky .
Tundu Lissu apokea ripoti ya Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe la wabunge na madiwani kuenguliwa. Wagombea ubunge Kitaifa 244 walichukua forum aa CHADEMA lakini wabunge 55 walienguliwa wakiwemo 3 katika ya 6 ya wagombea ubunge katika mkoa wa Njombe. Kitaifa madiwani wa CHADEMA 1025 wameenguliwa.
CCM ni waoga kushindana kupitia kura hivyo wameamua kuwatumia wasimamizi kuipunguzia wapinzani wagombea. Pia hata wale walioshinda rufaa, Tume ya Uchaguzi imeshindwa kutoa barua za ushindi wa rufaa ili waanze kampeni.
Deo Mwanyika mgombea wa CCM amekiri kukwepa kodi baada ya kupatikana na hatia. Hii ni doa tosha kukuzuia kupitishwa na Tume ya Uchaguzi
Uchaguzi 2020 - Ubunge Njombe Mjini; Emmanuel Masonga amuwekea pingamizi Deodatus Mwanyika baada ya kukiri kosa la jinai . Lakini kwa vile ni mgombea wa CCM ,msimamizi wa uchaguzi na Tume wamempitisha kusimama kama mgombea kupitia CCM .
Tundu Lissu awaombea kura Wagombea wa ubunge na madiwani kupitia CHADEMA.
Ilani ya CHADEMA inamsumbua sana yule Dr. Bashiru Ally Kakurwa kuhusu Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu. Dr. Bashiru aelewe uhuru ktk ilani ya CHADEMA ni kuhusu uhuru wa watu kuamua mambo yao wenyewe mfano biashara, kilimo, uvuvi na shughuli zingine za kujiingizia vipato kihalali bila kusahau kuikosoa serikali.
Hali ya kisiasa katika miaka mitano ilivyofikia sasa ni rahisi kumjadili Mungu kuliko kumjadili na kumkosoa John Pombe Magufuli .....