Yanayojiri Mgogoro DRC

Yanayojiri Mgogoro DRC

Barabara ya Mbujimayi hadi Kabinda
Keki ya taifa haina gawio sawa kati ya Kinshasa na majimbo yaliyo mbali kiasi raia wanaona ni wakubwa viongozi ndiyo wanajifaidisha

View: https://m.youtube.com/watch?v=Amfh5_Ol8Ic

DRC ni nchi kubwa sana. The largest ukiiondoa Algeria ambayo sehemu yake kubwa ni jangwa. Inahitaji uongoza makini sana kufikisha maendeleo kila sehemu. DRC is more than 2 times the size of Tanzania, huku mvua zikinyesha karibu mwaka mzima kwakuwa ni eneo la kiikweta. Bila kusahau Msitu wa Kongo nk ni challenges zinazohitqji dedication kubwa sana kudeal nazo. Kwa viongozi wetu hawa wa Kiafrika ni ishu kwelikweli.
 
23 February 2025
GOMA, KIVU
DR Congo

MATEKA AMBAO NI POLICE WA SERIKALI YA DR CONGO WAWASILI KWA MELI KUTOKA BIKAVU

View: https://m.youtube.com/watch?v=m4e4aJvcQfQ

Meli iliyojaa askari police ambao yamebwaga silaha zao na kuwa mateka wakati M23 walipoingia mjini Bukavu na kutoa wito wajisalimishe, wamewasilia bandarini Goma

Askari police hao waliwasili kwa meli yenye usajili wa Emmanuel 2 inayopiga kazi katika ziwa Kivu. Mateka hao watapitishwa katika programu maalum ya kuwapata mafunzo ya kuondoa propaganda mbaya na itikadi hasi walizofundishwa na serikali ya Kinshasa.

Baada ya programu hiyo watajumuishwa katika M23, na kabla ya kushuka wakihojiwa walitendwa vipi wakiwa mateka, askari polisi hao wamesema wamepewa haki zao zote za msingi kama mateka ambao ni raia wa Congo, na kuwa wanashauku kuigizwa katika programu ya M23 ya vuguvugu la movement ya kuwakomboa wacongomani na haki sawa kwa wote bila kujali kabila au nasaba za raia wote wa Congo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=-lnwaaGs0uU

Kimsingi hapa wengi walikuwa watumishi wa M23! Askari mtiifu huwezi kukubali ukapigane upande wa pili
 
DRC ni nchi kubwa sana. The largest ukiiondoa Algeria ambayo sehemu yake kubwa ni jangwa. Inahitaji uongoza makini sana kufikisha maendeleo kila sehemu. DRC is more than 2 times the size of Tanzania, huku mvua zikinyesha karibu mwaka mzima kwakuwa ni eneo la kiikweta. Bila kusahau Msitu wa Kongo nk ni challenges zinazohitqji dedication kubwa sana kudeal nazo. Kwa viongozi wetu hawa wa Kiafrika ni ishu kwelikweli.
Kwasasa wameshachelewa, pale mawili kupitisha upanga wa vita iingie mpaka Rwanda na Kagame apigwe kwelikweli ampaka akimbie nchi au Congo wakubali kuigawa 2 state lakini wajue wanaenda kumnufaisha rasmi Rwanda na hiyo Congo ya 2 itaendelea kubaki maskini tu
 
DRC ni nchi kubwa sana. The largest ukiiondoa Algeria ambayo sehemu yake kubwa ni jangwa. Inahitaji uongoza makini sana kufikisha maendeleo kila sehemu. DRC is more than 2 times the size of Tanzania, huku mvua zikinyesha karibu mwaka mzima kwakuwa ni eneo la kiikweta. Bila kusahau Msitu wa Kongo nk ni challenges zinazohitqji dedication kubwa sana kudeal nazo. Kwa viongozi wetu hawa wa Kiafrika ni ishu kwelikweli.

Utawala wa Kinshasa na ule wa majimbo wote wameshindwa, suala siyo ukubwa wa nchi bali utawala bora.
 
22 February 2025

MGOGORO WA DR Congo : Yaliyokutwa katika ghala la silaha za askari wa Tshisekedi na mipango yake ya kuvamia Rwanda

View: https://m.youtube.com/watch?v=STZBGC_UncE
Mhariri mtendaji James Munyaneza wa The New Times Rwanda atoa ushuhuda wa kina alipopata fursa kuwepo Goma na leo akiwa studio pamoja na mwandishi James Kahuranga kwa njia ya simu akiwa Rusizi kutupa habari za kina...

Inaonesha FARDC walikuwa wamejipanga kuivamia Rwanda kutokana na mpangilio wa zana zilivyopangwa (formation) kuelekea nchi ya Rwanda. Mhariri mtendaji James Munyaneza anasimulia kwa undani hali hiyo alivyokuwa amejipanga Tshisekedi ..

Mhariri mtendaji James Munyaneza alichokiona Goma ni uthibitisho unaoweza kuchukuliwa kuwa kulikuwa na mkakati mpana wa jeshi la Congo FARDC, Burundi kuivamia Rwanda kama tukio la bahati la M23 wasingejitokeza na kutibua mipango hiyo kwa ...

Mhariri mtendaji James Munyaneza aliweza kufika eneo la Airport ya Goma ambapo kilikuwa kitovu cha mapambano makali baina ya FARDC na M23 yaliyotokea wiki mbili zilizopita ....

Mhariri mtendaji James Munyaneza aliweza kufika kambi iliyokuwa na hadhi ya Joint Command Centre iliyokuwa inaratibu mipango ambapo kulikuwa na milingoti minne ya bendera kuwakilisha jeshi la Congo FARDC, jeshi la Burundi, jeshi la SADC SAMIDRC, jeshi la BURUNDI na FDLR - mgambo wa intarahamwe

Na kuwa ...Joint Command Centre hiyo ni kambi ongozi ya Operesheni za kijeshi kuna nyaraka na ramani zilizotokana ukusanyaji wa intelejesia ya kijeshi zinazobainisha maeneo mkakati nyeti ambayo FARDC na FDLR wangeyashambulia Rwanda... zilizoachwa baada ya kambi hizo kukimbiwa kufuatia kipigo kutoka kwa M23

Kilima Nyoka vilikuwepo vikosi special forces wa FARDC wakiwa wamejichimbia wanataza mpaka wa Rwanda na Kanyamahoro kulikuwepo kambi ya FDLR iliyo kilometa 3 tu kutoka mpaka na Rwanda..

Kambi zenye majina ya Satan 2 (shetani) Armageddon (Ziwa la Moto) majina hayo yakiashiria unyama unyama na silaha kali za maangamizi zilizo tayarishwa kuishambulia Rwanda ...

Kambi za mamluki waliosema ni 'wataalamu' kwa kumaanisha wangekuwa wanatoa ujuzi wa kutumia silaha hizo za maangamizi za 'shetani' na 'Ziwa la Moto' kuitia adabu Rwanda ..
1740447728061.jpeg

Kwa hiyo majeshi haya FARDC, kikosi cha ulinzi wa Rais, FLDR, mamluki wote hawa wangejiunga pamoja kuivamia Rwanda kwa kustukiza ... kama M23 wasingeanzisha mashambulizi February 2023..

Makontena yaliyosheheni silaha za mizinga ya masafa marefu ya kila aina , RPG , sniper rifles, kamikaze drones, camera ikionesha ingekuwa vita ya kisasa ...

Masimulizi hayo ya Mhariri mtendaji James Munyaneza yanakwenda na video mwendo ndani ya mahojiano haya ya ushuhuda wa kina..

Wataalamu kijeshi, utambuzi (intelejensia) ya kijeshi na intelejensia ya kiraia wanasema mkusanyiko huo wote wa mikakati, silaha, utaalamu, matayarisho mazito ya upande wa serikali ya Tshisekedi jirani na mpaka wa Rwanda. i
The missiom was to topple the Rwandan government and that mission has aborted
Inaonesha hayakuwa kujitayarisha kuishughulikia majeshi ya waasi wa M23 bali lengo lilikuwa kukamilisha tamko la Tshisekedi kuwa wataipiga Rwanda na kubadilisha uongozi wa kiserikali uliopo nchini Rwanda..
1740447406246.jpeg

Vifaa vya Tshisekedi vilivyokutwa na M23
 
👆
The report indicates that the arsenal included advanced artillery, armored vehicles, and stockpiles of ammunition, far exceeding what would be necessary for operations against the M23.

1740447795700.jpeg

1740447835253.jpeg

1740447977167.jpeg

1740478169531.jpeg

1740506760497.jpeg

All above Photos courtesy of The New Times Rwanda
1740475942354.jpeg
 
25 February 2025
Dar es Salaam, Tanzania

Hakuna jeshi lililokuwa na ndege yenye uwezo wa kuwasafirisha wanajeshi waliojeruhiwa vitani DRC kurudi nyumbani - Theletsane

View: https://m.youtube.com/watch?v=-SLqLuk8rXg
hayo yamebainishwa katika mahojiano.

Mkurugenzi wa Ogani ya Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa SADC Profesa Kula Theletsane anasema hakuna kikosi chochote cha kijeshi cha nchi katika kanda hiyo ya SADC ikiwa ni pamoja na jeshi la ulinzi la South Africa SANDF, kilikuwa na ndege yenye uwezo wa kuwasafirisha kurudi nyumbani wanajeshi waliojeruhiwa vitani kutoka DRC. Anasema badala yake ilitumiwa ndege ya kibinafsi charter .

Habari zaidi zinasema kuwa jijini Dar es Salaam mkutano wa wakuu wa kijeshi wa nchi za SADC wanakutana kutekeleza maazimio ya mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na EAC uliofanyika Dar es Salaam 08 February 2025 ambapo wakuu hao wa nchi walikubaliana kuwa sahihi ni kufungua jukwaa la mazungumzo kwa kuwa njia za kijeshi pekee haziwezi kumaliza mzozo wa Mashariki ya Congo...

SADC’s Director of Organ on Politics Defence and Security Affairs Professor Kula Theletsane says none of the military units in the region including SANDF, had a plane with the capacity to transport back home the wounded soldiers from DRC. He says a private plane was used instead.
 
25 February 2025

VIONGOZI 3 MASHUHURI WASTAAFU WATEULIWA KUONGOZA JOPO LA MAZUNGUMZO LA WADAU WALIOPO KATIKA MGOGORO WA DR CONGO

1740493139165.jpeg

Picha : Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, rais mstaafu wa Nigeria jenerali mstaafu Olusegun Obasanjo na mheshimiwa Hailemariam Desalegn waziri mkuu wa zamani wa Ethiopia wateuliwa kuongoza maridhiano kwa njia ya mazungumzo, ikiwa no mchakato mpya baada ya ule wa utatuzi wa kijeshi kuonekana siyo suluhu ya kudumu ya kuleta amani DR Congo.

Watatu hao wameteuliwa kufuatia azimio la mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na EAC uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema tarehe 8 February 2025
 
kati ya majeruhi hao, angalau wanajeshi 5 wamejeruhiwa sana (seriously wounded) na wawili ni wajawazito.

Taarifa za wanajeshi wajawazito zimezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii huku raia wa SA wakihoji iweje wanajeshi wapate ujauzito katikati ya mission? Hali hiyo imeibua mjadala mrefu hata kuliko taarifa ya idadi ya majeruhi hao kwa ujumla.
Duh!... jeshi la sasa la Africa kusini sio tishio kama Lile la enzi ya makaburu.

T14 Armata
 
25 February 2025
Lubero, Province du Nord Kivu
DR Congo

ASKARI WA FARDC WAFIKISHWA KATIKA KORTI YA KIJESHI YA JESHI LA FARDC KWA UTORO

View: https://m.youtube.com/watch?v=Tzn3fmqi8vg
Jeshi la serikali ya Congo limesema halitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu wanajeshi wake wanaotupa silaha na kutoroka ili wakiogopa kukabiliana na waasi wa M23

Leo makumi ya askari walisomewa mashitaka katika korti ya kijeshi ya FARDC (court Marshal) na kushitakiwa kwa utoro, kubwaga silaha, wizi, uporaji na kusababisha taharuki kwa raia wanapoona askari wa FARDC wakitimuka kila upande huku pia wakifanya uhalifu.

Jeshi la waasi la M23 tayari wamefika katika viunga vya nje ya mji wa Lubero vilivyo milimani wakiungalia mji wa Lubero ambao bado kuna vikosi kadhaa vya jeshi la serikali FARDC
 
Kwa nn wanafanya ngono wakiwa vitan??
Huu ni uhuni
Kwani ukiwa vitani unatolewa viungo vya uzazi? Vitani siyo wote wanapigana, wengine kazi Yao ni kuwawezesha wengine wapigane. Pia hata vitani kunawakati wa kupumzika.
 
23 February 2025
GOMA, KIVU
DR Congo

MATEKA AMBAO NI POLICE WA SERIKALI YA DR CONGO WAWASILI KWA MELI KUTOKA BUKAVU

View: https://m.youtube.com/watch?v=m4e4aJvcQfQ

Meli iliyojaa askari police ambao yamebwaga silaha zao na kuwa mateka wakati M23 walipoingia mjini Bukavu na kutoa wito wajisalimishe, wamewasilia bandarini Goma

Askari police hao waliwasili kwa meli yenye usajili wa Emmanuel 2 inayopiga kazi katika ziwa Kivu. Mateka hao watapitishwa katika programu maalum ya kuwapata mafunzo ya kuondoa propaganda mbaya na itikadi hasi walizofundishwa na serikali ya Kinshasa.

Baada ya programu hiyo watajumuishwa katika M23, na kabla ya kushuka wakihojiwa walitendwa vipi wakiwa mateka, askari polisi hao wamesema wamepewa haki zao zote za msingi kama mateka ambao ni raia wa Congo, na kuwa wanashauku kuigizwa katika programu ya M23 ya vuguvugu la movement ya kuwakomboa wacongomani na haki sawa kwa wote bila kujali kabila au nasaba za raia wote wa Congo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=-lnwaaGs0uU

Ila Congo watu wamevurugwa
 
Duh!... jeshi la sasa la Africa kusini sio tishio kama Lile la enzi ya makaburu.

T14 Armata
Jeshi la sasa la Afrika Kusini halina ulazima wa kuwa tishio kama zamani.

Zamani hawakuanza wakiwa tishio, kuna mambo yalisababisha. Ni kama Rhodesia ilivyokuwa na jeshi tishio kuliko Zimbabwe iliyofuatia.

Vilevile wanajeshi kufa sio ajabu. Nashangaa watu wanaoshangaa wanajeshi wa Afrika Kusini kufa, mnajua SA ilipoteza wanajeshi wangapi vita ya Angola? Hao Rwanda wenyewe wanakufa mamia ya wanajeshi huwezi sikia kelele wala mshangao. Whats so special na SA kufiwa wanajeshi.
 
SANDF ya enzi za makaburu ilikuwa hatari kweli kweli...Wacuba na Wasoviet waliokuwepo Angola wanakiri hilo.

SANDF ya sasa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa Bajeti, kushuka Sana kwa professionalism ( ndio maana wapo waliorudi kutoka Drc na ujauzito), Rushwa/ufisadi wa manunuzi ya zana ndio maana hata kule CAR na Drc wamepata fedheha.

Kiufupi SANDF ya sasa ni kivuli tu cha SANDF ya enzi za makaburu
 
Makabulu walikuwa wazungu mkuu kumbuka Hilo.
Ila jeshi la south Africa wapo wachache hata 1000 hawakufika huko drc
 
Back
Top Bottom