Yanayojiri miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar 26/4/2015

Yanayojiri miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar 26/4/2015

Ni jambo la kushangaza sana kuwa mtawala wa Zanzibar kapoteza na haithamini ID yake hivyo RAIA zake leo wanajitambua kwa jina jipya LA Tanzania bara!!! Lakini mtawaliwa pamoja na kutawaliwa bado yuko na ID yake ya asili na hakuna ambae atathubutu kumnyang'anya hadi mwisho wa dunia hii.

Pamoja na kujifariji kote sijawahi kuona passport ya Zanzibar?!
 
Leo ni maadhimisho ya miaka 51 toka zanzibar na tanganyika waungane Tv nyingi zipo live tufuatilie na tuweke updates zote hapa
=============

Leo tarehe 26 Aprili 2015 ni miaka 51 tangu mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar chini ya viongozi wa mataifa haya mawili, mzee Karume na Mwl Nyerere. Rais Jakaya Kikwete pia kwake itakuwa maadhimisho yake ya mwisho ya kitaifa kama Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania, Sherehe zimeshaanza na wageni wote wameshafika ikiwemo Rais wa Jamhuri.

Kwa sasa kinachoendelea ni kuimba wimbo wa taifa na ada za kadhaa za majeshi yetu

Sasa zinaingia ndege za Jeshi na zinapita juu ya uwanja wa Uhuru, wanapita maafisa wa Jeshi la wananchi mbele ya Rais

Zimepita jumla ya gadi 13 za majeshi mbalimbali ya ulinzi na usalama na sasa wanamalizia "marine special force" kutoka jeshi la wanamaji

Watoto wa halaiki ndio muda wao sasa pamoja na ngoma za asili kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani

Top 20 Most Powerful Militaries In Africa 2015

Mkuu ni kweli tuna jeshi imara,ila soma link utaona somalia,sudan kusini,congo DRC tulioenda kuwasaidia kuwachapa m23 wametupita,zimbawe nao wametupita ,hata 20 bora hatupo,sijui imekuwaje nimebaki nashangaa kama unajua kidogo nieleweshe!
Ukana Shilungo.



 
siasa na Africa kungu sana maalim seif namuona kimya kweli ila akitoka pale anaanza maneno mara ccm hivyi mara vile.
 
Ni swali dogo tu ila ningeomba tujadili hili.
Hivi kuna faida yoyote anayoipata mwanachi wa kawaida kama mfugaji wa kule umasaini, Mkinga mkulima wa miti kule Makete, nakadharika nakadharika.
Binafsi sijawahi wala sitegemei kunufaika na Muungano huu wa Zanzibar na Tanganyika.


Karibuni tujadili.
 
Wakati naangalia maadhimisho ya muungano naomba kufahamishwa ni kwa nini watu wanaotembea pembezoni mwa raisi(walinzi) au viongozi wengine wanavaa miwani mieusi? Na suti nyeusi? Tafadhali naomba ufafanuzi.
 
Na kwanini asipende kucheka wakati katika dunia hii anaishi kama vile yuko peponi!!!

Njaa, kiu na dhiki za maisha kwake ni hadithi za watu wakale.

Hata mimi mungu angalinipa nafasi ya maisha kama aliyonayo yeye basi na mimi ningalicheka hata kumzidi yeye.

Wacha hivyo yule ndie asili yake kwani umewai shuhudia marangap mkapa akichekacheka
 
Top 20 Most Powerful Militaries In Africa 2015 Mkuu ni kweli tuna jeshi imara,ila soma link utaona somalia,sudan kusini,congo DRC tulioenda kuwasaidia kuwachapa m23 wametupita,zimbawe nao wametupita ,hata 20 bora hatupo,sijui imekuwaje nimebaki nashangaa kama unajua kidogo nieleweshe! Ukana Shilungo.
Haha..hujawahi sikia UDSM kipo ktk vyuo bora duniani?je ktk uhasilia unaona hayo?Kweli jeshi letu ni Zuri ktk issue mbalimbali,ila hizo nchi tulizooenda zina shida pia zina vipandevipande...ila ktk vita kuna issue kibao zinazoweza tugeuza kuwa wafu km wengine.
 
ila kuna udhaifu mkubwa sna kwa upande wa ulinzi wa rais yani kwa professional assassinator/sniper hapati shida sana ya kutekeleza jukumu lake na kumtungua rais!!

Hatujafika huko wacha kuyaongelea hayo mambo ndugu
 
Wakati maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya muungano yanaendelea kule uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, watanzania wanashuhudia ufahari wa kupindukia wa viongozi wetu na wake zao wakiingia kila mmoja na gari la kifahari lilojazwa mafuta kwa fedha za umma huku wakishangiliwa. Ninajiuliza, hivi taifa limegharimika kwa kiasi gani kuandaa sherehe kama hizi ikiwepo ile ya rais kukabidhiwa katiba inayopendekezwa iliyofanyika mwezi Oktoba mwaka jana. Hivi ni watanzania wangapi wanakufa hospitalini kwa kukosadawa? Ni miradi mingapi imesimama kwa kukosa fedha? Ni watanzania wangapi wameshindwa kusafirisha bidhaa ikiwapo mazao ya wakulima kwenda sokoni kwa ubovu wa miundo mbinu ikiwapo barabara na reli? Orodha ya matatizo ya watanzania ni ndefu ikiwapo elimu ya awali hadi ya juu. Je gharama hizi za sherehe zisingeweza kupunguza baadhi ya matatizo haya ktk nchi ambayo watu wake wanaishi kwa stail ya kufunga mikanda? Hivi tunaweza kusema serikali yetu nayo imefunga mikanda? Au tuseme inajali? Tujadiliane!
 
Leo kwenye sherehe za muungano raisi alipoenda kukagua gwaride la vikosi walinzi wake wa usalama wa taifa walimfuata hasa yule mmoja alikua anaenda nae kila sehemu. Je wale askari wanaompeleka raisi akakague hawaaminiki mpaka mpaka usalama nao wamsindikize? Hapa nashindwa kuelewa uaminifu katika vikosi vyetu vya ulinzi na usalama.


Kuna mgawanyo wa majukumu hapo, kila mtu anatimiza jukumu lake
 
Aisee, nafuatilia sherehe za Muungano lupitia runinga hapa ila nimepata mshtuko kidogo Amiri Jeshi Mkuu Ndg Jakaya Mrisho Kikwete amepitiliza sijui alinogewa mpaka kamuacha aliyekuwa anamuelekeza wakati alitakiwa kukata kona yeye akanyoosha ikabidi arudi tena.

Ndgduh

Ukiangalia vizuri ni kama alichanganywa na yule jamaa mlinzi wa usalama wa taifa aliyembana zaidi upande wa kulia.Kimsingi jamaa alikosea sana kwani Wakati wa ukaguzi wa gwaride haruhusiwi mtu mwingine kupita mbele upande wa kulia,zaidi ya rais. baadae nadhani Afande Mwamunyange alimshtua Huyo mlinzi aondoke, akaondoka.
 
Ni swali dogo tu ila ningeomba tujadili hili.
Hivi kuna faida yoyote anayoipata mwanachi wa kawaida kama mfugaji wa kule umasaini, Mkinga mkulima wa miti kule Makete, nakadharika nakadharika.
Binafsi sijawahi wala sitegemei kunufaika na Muungano huu wa Zanzibar na Tanganyika.


Karibuni tujadili.
Hakuna manufaa yoyote kwa mtanganyika, una manufaa kwa wazanzibar. Tazama walivyolowea huku kuanzia kina Aboud Jumbe hadi kina Rashid hamad, sijui kwanini hawapataki kwao.
 
Napata kuamini hili kwamba Muungano ulipo sasa ni wa kinafiki na anganya toto kwa Watanzania kwamba kuna Muungano wakati in real sense ni usanii tu. Turudi kwenye mada ni kwamba Zanzibar ni Koloni la Tanzania bara, YES, Napata kuamini hivi kwa mambo yafuatayo:

1. Rais wa Tanzania Bara ndo mgeni rasmi kwenye sehrehe za Muungano
2. Rais wa Tanzania Bara ndo anapigiwa mizinga 21 kwenye sherehe hizi
3. Rais wa Tanzania Bara ndo anaimbiwa wimbo wa Taifa.
4. Rais wa Tanzania Bara ndo anakagua parade ya jeshi letu.
5. Rais wa Tanzania Bara anapewa heshima zote kwenye sherehe hizi.
6. Gwaride la heshima linapita mbele kwaajili ya Rais wa Tanzania Bara na sio wa Zanzibar
7. Huku Rais wa Zanzibar akitoa udenda pale jukwaani kwa yale anayofanyiwa Rais wa Bara.
8. Akili za viongozi wa Zanzibar zikiwa zimeshikiwa Bara.
9. Kwa haya yote Napata kuamini hakuna Muungano bali, Zanzibar ni Koloni la Tanzania Bara huku kiongozi wa Zanzibar akiwa kama Mayor wa kufanikisha unyonyaji huu.

WATANGANYIKA TUFURAHIE MIAKA 51 MUUNGANO TANGANYIKA NA KOLONI LETU (ZANZIBAR)


Pia ni muungano wa Nchi mbili, Kwanini kila siku sherehe zinafanyika huku Bara, kumbuka hata mwaka jana wavunja matofali ilikuwa hapo hapo shamba la bibi bara
 
Back
Top Bottom